Katika Motu Proprio Immota Manet:Majimbo matano ya Roma yaungana kuwa Sekta moja ya Kati
Vatican News
Kwa barua ya Kitume ya Immota manet iliyochapishwa tarehe 26 Novemba 2025 ya Motu Proprio Baba Mtakatifu, Leone XIV anaanzisha na kuamuru kwamba "Sekta tano, kuanzia 1 hadi 5, zirudi kuwa sehemu ya Sekta moja ya Kati, ambayo kwa hivyo inaongezwa tena kwenye Sekta zingine nne za Jimbo la Roma.” Kuhusu uamuzi huo, Papa alifafanua: “Ingawa motisha, dhana, na mambo ya kuzingatia yaliyowekwa katika Motu Proprio ‘La vera bellezza,’ iliyotolewa tarehe 4 Oktoba 2024, na Mtangulizi wangu hayajabadilika, na kuamini kwamba baadhi ya tafakari zilielekezwa mahususi kwa Mwaka wa Jubilei unaokaribia kuhitimishwa, ambapo, hata hivyo, si tu umahususi pia na umoja wa Sekta ya Kati ya Jimbo la Roma umejitokeza wazi zaidi, kwa Barua hii ya Kitume iliyotolewa ya Motu Proprio, ninaanzisha na kuagiza kwamba Sekta tano, kuanzia I hadi V, zirudi kuwa sehemu ya Sekta moja ya Kati, ambayo kwa hivyo inaongezwa tena kwenye Sekta zingine nne za Jimbo la Roma.
“Ninaamuru kwamba kile kilichoamuliwa katika Waraka huu wa Kitume kitolewe matokeo thabiti na ya kudumu, bila kujali chochote kinyume chake, hata kama kinastahili kutajwa maalum, na kwamba kitangazwe kwa kuchapishwa katika Gazeti la Osservatore Romano, ikianza kutumika siku ya kuchapishwa kwake, na baadaye kuingizwa katika ufafanuzi rasmi wa “Acta Apostolicae Sedis.”
