Papa akutana na Maaskofu wa Hispania:umuhimu wa mazunguzo ya Kanisa la Hispania
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na Tume ya Utendaji ya Baraza la Maaskofu wa Hispania (CEE) katika mkutano uliodumu kwa takriban saa moja. Mkutano huo ulikuwa umeombwa na maaskofu siku chache baada ya kuchaguliwa kwa Papa Leo mnamo Mei 8, na kuthibitishwa mnamo Septemba. Mwishoni mwa mkutano huo, Askofu Mkuu Luis Argüello wa Valladolid na Rais wa CEE, alielezea kwamba Papa na hao wawili walijadili "hatua mbalimbali ambazo Kanisa la Hispania linapitia." Kwa hiyo miongoni mwa mada zilizojadiliwa ni "hamu kubwa ya kutangaza Injili"; "changamoto za kuanzishwa kwa Ukristo"; "mpangilio wa kimaeneo wa majimbo"; kuwasili kwa waamini wengi kutoka nchi zingine; uwepo wa watu wa kawaida katika maisha ya umma; hali ya watawa na waliofungwa, utamaduni "tajiri sana" lakini kwa sasa unaonyeshwa na kupungua kwa idadi.
Askofu huyo pia alitaja "ukweli wa makuhani" nchini Hispania, ulioimarishwa na kuwasili kwa mapadre wapya kutoka Amerika Kusini na Afrika. Kipengele muhimu cha mkutano huo kilihusu kazi iliyoanzishwa na Kanisa la Hispania "kwa kuchochewa na Kiti Kitakatifu" katika nyanja za kuzuia, elimu, na fidia kwa waathiriwa wa unyanyasaji, kupitia mpango unaoitwa PRIVA. Mpango huu unakusudiwa kutoa fidia kamili kwa watu ambao, wakiwa watoto au katika hali kama hiyo, wametendewa vibaya ndani ya majimbo, mashirika ya kitawa, au vyombo vingine vya kikanisa, katika kesi ambazo zimeisha muda wake au ambapo mhalifu amefariki."
Mpango huo," Askofu Argüello alielezea, "umesababisha kuundwa kwa tume ya fidia ambayo, kutokana na tunachokiona, inawapokea waathiriwa kwa kuridhisha." Askofu huyo pia aliripoti kwamba Papa amearifiwa kuhusu hali ya Askofu wa Cadiz na Ceuta, Rafael Zornoza, aliyeshtakiwa kwa unyanyasaji wa kijinsia katika miaka ya 1990 alipokuwa mkurugenzi wa seminari ya Getafe. Baba Mtakatifu anafahamu waziwazi, lakini hakutuambia kitu kingine chochote."
Kulingana na Askofu Argüello, alisema Askofu huyo anaweza kuwasilisha kujiuzulu kwake hivi karibuni. Katika mkutano wao pia kulikuwa fursa ya kusasisha mwaliko kwa Papa kutembelea Hispania. "Tunaondoka tukiwa na matumaini kwamba ziara hiyo inaweza kufanyika hivi karibuni," alisema rais wa CEE, "ili Papa aweze kujifunza kuhusu baadhi ya hali halisi ya Kanisa letu."
Na akijibu maswali ya waandishi wa habari, Askofu Argüello aliongeza kuwa " Papa Leo XIV alisema anajua jinisi ambavyo kuna kuibuka tena kwa maslahi ya kiroho na kidini," hasa yanayoonekana miongoni mwa vijana, hata katika muktadha ambao kijamii hauko mbali na desturi za kikanisa. Kiukweli kuna dalili za ukuaji katika idadi ya mafungo ya kiroho, katika uzoefu wa kijumuiya wenye nguvu zaidi, na katika idadi ya watu wazima wanaoomba Ubatizo.
Maaskofu pia walithibitisha ukweli muhimu kwa Papa: ongezeko la waseminari ikilinganishwa na mwaka 2024. Kulingana na Askofu Argüello, ishara hizi ni sehemu ya tafakari pana iliyofanywa na Papa Leo XIV, aliyejitolea kwa utume wa uinjilisti katika jamii ambayo "sio tu ya kidunia bali ina uwezekano wa kuwa ya kidunia." "Katika hali hii," alisema, "aina mpya za utafiti zinaibuka, ikiwa ni pamoja na utafiti wa kiroho na Injili."
Maaskofu walibainisha ujuzi wa kina wa Papa Leo kuhusu hali ya Hispania, uliokua wakati wa miaka yake kama Mwagostiniani na katika utumishi wake kwa Baraza la Kipapa la Maaskofu. Mada zingine zilizojadiliwa ni pamoja na Jubilei, "hasa Jubilei ya vijana iliyoadhimishwa mapema Agosti mwaka huu." Ujumbe wa EEC ulimpatia Papa Biblia iliyofungwa yenye tafsiri rasmi ya Baraza la Maaskofu, matoleo mawili ya jarida la Ecclesia lililowekwa wakfu kwake, na mchango kwa ajili ya shughuli za Upendo za Papa.
Wakati wa ziara yao Roma, Tume ya Utendaji pia ilikutana na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin. Mkutano huo ulikuwa fursa ya "kuzingatia masuala muhimu katika uhusiano wa Kanisa na Serikali nchini Hispania," ikikumbusha mazungumzo ya hivi karibuni ya Kardinali huyo na Waziri wa Sheria na, hivi karibuni, na Rais Pedro Sánchez kando ya Mkutano wa COP30 nchini Brazil.
