Papa azindua Kituo cha Wagonjwa wa Nje cha Mt.Martino mjini Vatican
Vatican News
Kituo kipya kimefunguliwa miaka kumi tu, baada ya uzinduzi wa Zahanati ya Madre di Misercordia yaani "Mama wa Huruma" ambayo pia ipo karibu na Uwanja wa Mtakatifu Petro, kabla ya Siku ya Maskini Ulimwenguni itakayoadhimishwa Dominika, tarehe 16 Novemba 2025. Mara baada ya uzinduzi wa Mwaka wa Masomo katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Lateran, 2025/ 2026, Ijumaa tarehe 14 Novemba, Baba Mtakatifu Leo XIV, alirudi mara moja mjini Vatican, yapata saa sita mchana, na kufikia eneo hilo la Mtakatifu Martino, lililo karibu na nguzo za Bernini, lilojulikana kwa kuwakaribisha maskini. Hapa, kuna mahali pa kuoga kwa wasio na makazi, eneo la kunyolea nywele, na Zahanati ya Mama wa Huruma, ambayo Papa Francisko aliiunga mkono kwa nguvu kutoa huduma kwa wale wasio na hati, fedha, au ufikiaji wa mfumo wa huduma ya afya, kitaifa.
Kituo cha kwanza cha ziara ya Papa Leo XIV kilikuwa Zahanati yenyewe. Akiongozana na Mhudumu Mkuu, yaani Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo, Kardinali Konrad Krajewski, alikutana na Dk. Massimo Ralli, Mkurugenzi wa Zahanati ya Wagonjwa wa Nje ya Baraza la Kipapa la Upendo, na Dk. Luigi Carbone, Mkurugenzi wa Afya na Usafi katika Gavana ya Jiji la Vatican. "Ilikuwa ziara ya faragha," Kardinali alisema, "kwa sababu hakuna mtu aliyeambiwa kwamba Papa anakuja, kwa hivyo ni madaktari waliokuwa tu katika zamu waliokuwepo."
Siku ya Ijumaa asubuhi, Novemba 14, kulikuwa na madaktari wapatao 8, wauguzi 4, na watu 2 wa kujitolea, ambao tayari walikuwa wamewasaidia watu 65 kufikia wakati ambao Baba Mtakatifu aliwasili. Papa Leo XIV aliwasalimia na kuwauliza kuhusu shughuli za Zahanati hiyo.
Huduma ya afya ya akili
Kardinali Krajewski alisisitiza jinsi ambavyo "Papa alivyoshangazwa na ukweli kwamba miongoni mwa madaktari waliokuwepo, pia kulikuwa na wataalamu wa magonjwa ya akili. Maskini wetu pia wanahitaji aina hii ya huduma, ambayo ni ngumu sana, kwa sababu mfupa unapovunjika, tunakimbilia mara moja kwenye chumba cha dharura," alisema, akiongeza kuwa "linapokuja suala la afya ya akili, kila kitu kinakuwa kigumu zaidi."
Madaktari wanatoka Hospitali ya Gemelli na hutoa utaalamu wao kwa kujitolea na uvumilivu. "Wana mengi ya kufanya hapa kwa sababu watu wanawaamini," Kardinali aliongeza. "Hatuombi hati, na labda hiyo inathibitisha heshima yao," alisema, akibainisha kuwa hawaonekani, kama wanavyokuwa mitaani mwa Roma kila wakati, "lakini hapa, msaada unazidi jina na nchi ya asili. Hapa, muhimu ni hitaji lako."
Huduma mpya
"Kazi nzuri, na asante," Papa Leo alisema, huku akitazama nje ya dirisha dogo karibu na bafu, akiwaacha wafanyakazi wakiguswa na ishara yake. Kisha aliwashukuru wale waliofanya kazi katika ukarabati wa Zahanati ya Wagonjwa wa Nje ya Mtakatifu Martino, ambayo, kulingana na taarifa kutoka Baraza la Kipapa la Huduma ya Upendo nsasa ina vyumba viwili vilivyo na teknolojia ya kisasa ya matibabu na idara ya radiolojia, yaani ya Picha au X-ray. Mashine ya X-ray ya kizazi kijacho itafanya iwezekane kugundua haraka na kwa usahihi visa vya nemonia, kuvunjika kwa mifupa, uvimbe, magonjwa ya kuzorota, mawe ya figo, na vizuizi vya utumbo, hali ambazo mara nyingi hupuuzwa miongoni mwa wale wanaoishi katika umaskini. Utambuzi huu wa mapema utawaruhusu madaktari kuanza matibabu yanayofaa haraka iwezekanavyo, na kusababisha ubora wa maisha kwa wale ambao hawana chochote.
Kumwona Yesu katika maskini
Zahanati mpya iliwezekana shukrani kutokana na ushirikiano na Kurugenzi ya Afya na Usafi ya Gavana wa Jiji la Vatican na inatoa huduma kamili kwa wale wanaotafuta msaada wa kimatibabu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
