Papa Leo kwa wandishi kwenda Türkiye:Tunatumaini kutangaza umuhimu wa amani duniani kote
Na Salvatore Cernuzio- Uturuki(Türkiye)
"Kwa Wamarekani hapa, katika siku ya kushukuru kwa furaha! Ni siku nzuri ya kusherehekea, na ninataka kuanza kwa kuwashukuru kila mmoja wenu kwa huduma mnayotoa kwa Vatican, Vatican, na mimi mwenyewe, lakini pia kwa ulimwengu mzima." Papa Leo alitabasamu alipozungumza kwenye kipaza sauti, kwa Kiingereza, kwa waandishi wa habari 81, wapiga picha, kutoka takriban vyombo ishirini vya habari vya kimataifa vinavyomsindikiza katika ziara yake ya kwanza ya kitume. Alisimama mbele ya pazia la kijivu la Ndge ya 'ITA Airbus' 320 ambayo iliondoka saa 1:58 asubuhi, masaa ya Ulaya ambapo mtu anaweza kuona, katika kiti cha kwanza, kile kilichohifadhiwa, Picha ya Mama wa shauri jema, picha inayopendwa na wana wa Mtakatifu Agostino ambayo imehifadhiwa katika mji wa Lazio huko Genazzano, ambapo Robert Francis Prevost mara baada ya kuchaguliwa siku mbili tu alikwekwenda huko tarehe 10 Mei 2025.
Sauti yake ilikuwa na ujasiri, lakini uso wake ulionesha hisia kidogo. Kwake, ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Waagostiniani alifanya zaidi ya safari 50 ulimwenguni kote, lakini hii ni mara ya kwanza. Ziara yake ya kwanza nchini Uturuki (Türkiye) na Lebanon; akiwa "kama Papa" kuruka zaidi ya rasi ya Italia. Alielekea Ankara, kisha Istanbul jioni, na kesho anasimama Iznik kusherehekea kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicaea pamoja na mapatriaki na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo. Kuanzia Novemba 30, atasafiri kwenda Lebanon kuwafariji watu waliojeruhiwa na vita na mgogoro na kuomba amani ya haraka katika Mashariki ya Kati.
Amani, ujumbe kwa ulimwengu
"Amani." Papa alirudia hili mara kadhaa katika salamu zake kwa waandishi wa habari, dakika ishirini baada ya kuruka juu. "Safari hii ya Uturuki na Lebanon, kwanza kabisa, ina maana ya umoja, ikiadhimisha kumbukumbu ya miaka 1,700 ya Mtaguso wa Nicaea. Na nimetamani sana safari hii kwa maana yake kwa Wakristo wote, lakini pia ni ujumbe mzuri kwa ulimwengu mzima. Na zaidi ya yote, uwepo wangu, ule wa Kanisa, na wa waamini nchini Uturuki na Lebanon, tunatumaini, utatangaza, utasambaza, na kutangaza umuhimu wa amani duniani kote." Safari ambayo kwa hivyo ni ujumbe, pamoja na mwaliko "wa kutembea pamoja ili kutafuta umoja zaidi, maelewano zaidi, na kuona jinsi wanaume na wanawake wote wanavyoweza kuwa kaka na dada kweli." Kwa sababu, Papa alisisitiza, "zaidi ya tofauti, zaidi ya dini tofauti, imani tofauti, sisi sote ni kaka na dada, na tunatumaini kukuza amani na umoja duniani kote.
![]()
Picha ya Selfie na wafanyakazi wa ndege (@Vatican Media)
Moyo wa Papa wa Amerika Kusini
"Asante kwa kuwa hapa," Leo aliendelea, "asante kwa huduma mtakayotoa siku hizi na kwa kuwa sehemu ya wakati huu wa kihistoria." "Asante" pamoja na "karibu" ulikuwa ujumbe ambao Valentina Alazraki, mwandishi wa habari wa Mexico, kiongozi wa waandishi wote wa habari wa Vatican, alikuwa amemwambia Papa kwa safari 163 za kipapa kwa jina lake, kuanzia na safari yake ya kwanza mwaka wa 1979 kwenda Mexico akiwa na Yohane Paulo II. "Kwa mtangulizi wako Francisko, ambaye huko Buenos Aires alionekana kuwachukia waandishi wa habari, nilisema katika safari yake ya kwanza: 'Karibu kwenye ngome ya simba! Sasa wewe ndiye simba!' Karibu sana!" Mwandishi wa habari alimpatia Papa ishara ya Bikira wa Guadalupe ya mtindo wa Kibyzantine: "Kwa Papa wa kutoka Amerika Kaskazini lakini mwenye roho ya Amerika Kusini."
![]()
Picha ya Bikira Maria wa Guadalupe waliyomzawadia Papa Leo(@Vatican Media)
León de Perú na Leo kutoka Chicago
Kuanzia hapo, mzunguko wa salamu kutoka kiti hadi kiti kingine ulifuatia. Ni utamaduni ulioanzishwa na mtangulizi wake Papa Francisko na sasa ni wakati wa utani, matamko, na maoni ya muda mfupi, picha za kujipiga zilikuwepo, na maombi ya baraka kwa ajili yake mwenyewe au kwa marafiki na familia. Na zaidi ya yote, ni wakati wa kubadilishana zawadi. Jambo hilo hilo lilitokea kwa Papa Leo. Zawadi nyingi zilitolewa na waandishi wa habari. Ya kwanza ni aina mbili za picha muhimu zaidi kutoka makala ya "León de Perú" na "Leo kutoka Chicago," zilizotengenezwa katika miezi ya hivi karibuni na Radio ya Vatican - Vatican News.
Moja kati ya hizo mbili pia ina picha, ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, ya Prevost kijana sana aliyevaa kama Ndugu wa Blues katika miaka ya 1980, wakati wa kutolewa kwa filamu ya ibada ya John Landis, iliyopigwa Chicago. Papa alielekeza na kucheka kwa furaha: "Ah, nzuri!" Pia alishikilia medali ya Mtakatifu Agostino, wakati huu kutoka Dolton, nyumbani kwake pa utoton ili iweze kumlinda wakati wa safari.
![]()
Mkusanyo wa picha zilizotolewa kwa Papa, na Mwandishi Salvatore Cernuzio akimwonesha picha hizo(@Vatican Media)
Keki zaidi ziliwasilishwa kwa Papa, kuanzia na keki ya maboga, sahani ya kiutamaduni ya Shukrani
Ili kumheshimu Papa wa kwanza wa Marekani katika historia, bidhaa mbili za White Sox pia ziliwasilishwa, timu inayopendwa ya besiboli ya "mvulana" kutoka South Side ambaye alikuwa Papa wa Kanisa la Ulimwengu: urithi wa familia, wa mchezaji maarufu wa miaka ya 1950, Nellie Fox ("Aliwezaje kupitia usalama?" vichekesho Leo), na jozi ya viatu vyeusi na soksi zenye nembo nyeupe ya timu. "Anaweza kuzivaa huko Castel Gandolfo!" alisema mpiga picha Lola Goméz. Papa Leo XIV alionesha zawadi hiyo kwa furaha, ikiwa imewekwa kwenye sanduku la bluu.
![]()
Keki ya Maboga(pumpkin pie)(@Vatican Media)
Mawazo kuhusu Ignacio
Hata hivyo, sura yake inabadilika wakati mwandishi wa habari wa Radio Cope Eva Fernández alimpa barua kutoka kwa Ignacio Gonzálvez, kijana wa Hispania aliyelazwa hospitalini tangu msimu uliopita wa kiangazi katikati ya Jubilei ya Vijana, katika Hospitali ya Bambino Gesù kwa ugonjwa mbaya wa lymphoma ambao alikuwa karibu kufa. Historia hii imeenea sana tangu Papa mwenyewe alipoomba maombi kwa ajili ya kijana huyo kutoka jukwaani huko Tor Vergata, baadaye akaenda katika kitengo cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Bambino Gesù kuwakumbatia wazazi wake, Pedro Pablo na Carmen Gloria, kaka yake, Pedro Pablo Jr., na dada yake, Adela. Papa Leo XIV alidokeza kwamba amearifiwa kuhusu hali ya Ignacio, ambaye bado ni mgonjwa katika hospitali ya Vatican na "atasherehekea" siku yake ya kuzaliwa hapo Jumanne ijayo.
![]()
Nembo ya mababu wa Papa(@Vatican Media)
Eva Fernández, anayejulikana kwa zawadi zake za ajabu kwa mapapa, kwa mara nyingine tena alimkabidhi Papa Leo XIV nembo ya mababu zake wa Hiispania. Utafiti uliofanywa na Kituo (Centro de Estudios Montañeses) kimethibitisha kwamba mababu wa mama wa Papa wanatoka katika mji wa Cantabrian wa Isla, katika manispaa ya Arnuero. Hasa zaidi, ni wanne kati ya babu na bibi wa kizazi cha kumi na moja, hidalgos (makuhani) wa Isla katika karne ya 16. Papa alichukua nembo ya shamba la fedha, pilipili hoho, na kamba nyekundu (sifa za Isla), muhuri, na ishara ya taji ya kifalme ya Hispania. Ni zawadi, ndiyo, lakini zaidi ya yote, ni "kisingizio" kuuliza: "Baba Mtakatifu, utatembelea Hispania lini?" "Hebu tuone!"
![]()
Kasha la viatu na soksi za White Sox(@Vatican Media)
Hamu ya kwenda Algeria
Kwa mwandishi wa habari mwenye asili ya Algeria, alimwambia: "Natumaini kwenda Algeria." Pia karatasi ya ngozi iliyotengenezwa na Kanisa Katoliki la Ugiriki la Ukraine huko Kharkiv ilithaminiwa sana kwa msaada uliotumwa kwa wale waliokuwa mstari wa mbele. Hatimaye, wawakilishi wa vyombo vya habari vya Italia walimpatia Papa barua inayoelezea sababu za kwa nini watajiunga na mgomo wao, Novemba 28. Yaani, kushindwa kusasisha mkataba wao wa uandishi wa habari, ambao uliisha mwaka 2016, licha ya kupunguzwa mbalimbali na hatari za Akili Unde kwa taaluma hiyo.
![]()
Zawadi ya gazeti kwa Papa Leo XIV(@Vatican Media)
Tazama Picha za Papa Leo
2025.11.27 Ziara ya Kitume nchini Turkiye-Makaribisho rasmi katika Uwanja wa Kimataifa wa Ankara-Esenboğa
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
