Papa:Jihadhari na udanganyifu Mpotovu wa AI
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika hotuba yake Baba Mtakatifu Leo Jumatatu tarehe 17 Novemba 2025 katika Ukumbi wa Clementina wa Jumba la Kitume mjini Vatican kwa washiriki wa Semina kuhusu “Maadili katika Usimamizi wa Makampuni ya Huduma za Afya” iliyoongozwa na Askofu Alberto Bochatey, OSA, Askofu Msaidizi wa La Plata, nchini Argentina, ambaye Papa alimsalimia mwanzoni mwa hotuba yake, aliyoitoa kwa lugha ya Kihispania Semina hiyo ilifadhiliwa na Chuo cha Kipapa cha Maisha inayofanyika kuanzia 17 hadi 21 Novemba 2025 jijini Roma katika Taasisi ya Kipapa ya Mababa wa Kanisa Augustinianum.
Kutafakari thamani ya kimaadili
Kama kawaida yake Papa alianza kuwatakia amani, huku akiwashukuru na kuwakaribisha wote kuanzia na Askofu huyo Bochatey, O.S.A., Mkurugenzi wa Semina hii kuhusu Maadili katika Usimamizi wa Afya, na washiriki wote katika semina ambayo wamekusanyika, chini ya usimamizi wa Chuo cha Kipapa cha Maisha, kujadili maadili katika afya, akili bandia, na uvumbuzi wa kiteknolojia na kidijitali. Hata hivyo, unapokaribia makaburi ya Mitume Petro na Paulo wakati wa Mwaka huu wa Jubilei, mkutano wao si wa kujenga tu, bali pia wamefika hija, ambapo kutafakari thamani ya kimaadili ya mapendekezo yetu kunakuwa hatua nzuri katika safari ambayo tumeitwa kuifanya kama jamii na kama Kanisa. Leo hii, Kanisa linawakaribisha kama mahujaji wa matumaini, tukizingatia mbinu, ujuzi, na nia zao mbalimbali kuwa za thamani, ili kuanzisha mazungumzo ya maisha na vitendo katika kazi ya pamoja ya kuwatunza wagonjwa.
Zana zenye ufanisi kama AI zinaweza kubadilishwa, kufunzwa na kuelekezwa
Vipengele vingi vya kuvutia vinaibuka kutoka katika mada watakayojadili, labda nyingi sana kuzungumzia katika salamu hiyo fupi. Hata hivyo, Papa alipenda kuakisi dhana ambayo inaonekana kwangu kuwaunganisha. Hasa kauli inayopotosha, kufupisha, na kwa udanganyifu huondoa mtazamo wetu wa uhalisia wa jamii na wa mgonjwa mahususi, na kusababisha hali ya ukosefu wa haki katika usimamizi wa rasilimali zinazohitajika kwa ajili ya usimamizi sahihi wa huduma ya afya. Ijapokuwa kama watu binafsi na kama jamii tumeitwa kutetea kikamilifu utu usio na shaka wa kila mwanadamu, katika hatua na vipengele vyote vya kuwepo kwake, kwa bahati mbaya, hii si mara zote inaendana na uhalisia. Zana zenye ufanisi kama akili unde(AI) zinaweza kubadilishwa, kufunzwa, na kuelekezwa ili, kwa sababu za manufaa au maslahi, iwe ya kiuchumi, kisiasa, au vinginevyo, upendeleo huu, wakati mwingine usioonekana, uzalishwe katika taarifa, katika usimamizi, na jinsi tunavyojionyesha au kuwakaribia wengine.
Kuunda vifungo vya kujenga madaraja
Kwa hivyo watu watakabiliwa na udanganyifu potofu ambao utawaainisha kulingana na matibabu wanayohitaji na gharama zao, asili ya magonjwa yao, na kuyabadilisha kuwa vitu, data, na takwimu. Papa Leo XIV anaamini njia ya kuepuka hili ni kubadilisha mtazamo wetu, kutambua thamani ya mema kwa maono mapana, kuona, kama Mungu anavyoona, ili tusizingatie faida ya haraka, bali juu ya kile kitakachokuwa bora kwa kila mtu, kujua jinsi ya kuwa mvumilivu, mkarimu, na mwenye usaidizi, kuunda vifungo na kujenga madaraja, kuunganisha mitandao, kuboresha rasilimali, ili kila mtu aweze kuhisi kama wahusika wakuu na wanufaika wa kazi ya kawaida. Wakati huo huo, Mungu anatufundisha kwamba maono haya mapana hayapaswi kamwe kutenganishwa na mahusiano ya kibinadamu, na mabembelezo, na utambuzi wa mtu binafsi, katika udhaifu na hadhi yake. “Ni maono ya kina, maono yanayofikia mioyo ya wengine na kupanua yetu wenyewe. Maono haya mawili yatakuwa suluhisho bora zaidi la kuhakikisha kwamba miundo yetu ya usimamizi haipotezi mtazamo wa jambo muhimu zaidi: mazuri tunayoitwa kuyalinda. Bwana atusaidie kuwa waaminifu katika huduma hii. Asante.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
