Tafuta

2025.11.24 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Watumishi wa Maria. 2025.11.24 Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Watumishi wa Maria.  (@Vatican Media)

Papa kwa Watumishi wa Maria:ishara ya amani na udugu

Papa Leo XIV akikutana Shirika la Watumishi wa Maria,aliwaalika warudi kwenye vyanzo ili kutazama vyema wakati ujao,kusikiliza kilio cha maskini,kuishi kulingana na Injili,kukuza ikolojia fungamani na kujitolea kwa Bikira.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV akikutana na mjini Vatican tarehe 24 Novemba 2025 na Washiriki wa Mkutano Mkuu wa 215 wa Shirika la Watumishi wa Maria aliwahutubia kwa kusisitizia njia za kufuata: “Udugu, huduma, na hali ya kiroho ya Maria.” Papa alisema kuwa wao wameitwa kuwa wabebaji wa urafiki na amani.  Na zaidi alisisitiza kwamba kurudi kwao mara ya pili ni katika Kanuni ya Mtakatifu Agostino, Katiba, na urithi wa kiroho unaotokana na historia yao. Vyanzo hivi vinawapatia, kwa maana fulani, ufunguo wa ufafanuzi ambao, kwa msaada wa Roho, unawawezesha kusoma na kutafsiri kile ambacho Neno la Mungu linawaambia.

Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Watumishi wa Maria
Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Shirika la Watumishi wa Maria   (@Vatican Media)

Katika hotuba yake, aliwasifu watawa  hawa kwa imani na huduma yao, akisisitiza umuhimu wa kurudi kwenye mizizi yao huku wakionesha juhudi zao kuelekea wakati ujao. Ili kuendelea kutajirisha Kanisa, Papa Leo XIV aliwataka kukumbatia Injili na Uongozi wa Mtakatifu Agostino, na kusikiliza kilio cha maskini. Katika muktadha huo, alikumbuka jinsi ambavyo Mtakatifu Paulo alivyoshangazwa na uzuri wa kuishi kwa ajili ya Kristo na kujishikamanisha na Neno lake na mfano wake. Utawala wa Mtakatifu Agostino na urithi wa kiroho unaotokana na historia yao, ambayo, inawapatia ufunguo wa ufafanuzi' ambao, kwa msaada wa Roho, husoma na kutafsiri kile ambacho Neno la Mungu linawaambia. Kwa kusikiliza kilio cha maskini, huwapatia  watawa wakati wa neema ambapo wanaweza kupata maana kubwa.

Shirika la Watumishi wa Maria
Shirika la Watumishi wa Maria   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akiendelea na hotuba hiyo aidha aliwasihi wafuate njia tatu za kawaida za tamaduni yao, yaani udugu, huduma, na hali ya kiroho ya Maria. Alikumbusha kwamba hizi hazikuanzishwa na mwanzilishi mmoja, bali na watu kadhaa waliofungwa na urafiki imara katika Kristo. Katika ulimwengu kama wetu alisisitiza kuwa,  hii ni ishara ya kazi na wito maalum wa  kuishi na kupeleka udugu, hasa pale ambapo watu wamegawanyika kwa sababu ya migogoro, utajiri, tofauti za kiutamaduni, rangi, au dini.  Katika miktadha hii yote, watawa hawa wa Shirika la Watumishi wa Maria "wanaitwa kuwa wabebaji wa urafiki na amani, kama walivyokuwa wale  "Saba," ambao, katika miji yao wenyewe pia wamegawanyika kwa chuki ya kidugu, wakawa wabebaji wa upatanisho na upendo. Maisha kulingana na Injili, yanahusisha shauku kwa Mungu na kwa mwanadamu, ambayo husababisha kupenda mbingu na dunia kwa nguvu ile ile."

Shirika la Watimishi wa Maria.
Shirika la Watimishi wa Maria.   (@Vatican Media)

Papa Leo alisema kuwa "ni ndani ya muungano huu wa kipekee, ndipo huzaliwa na kukomaa chaguo sahihi ambazo, leo hii kama wakati huo, humruhusu mtu kuwepo mahali ambapo kaka au dada wameumia zaidi, mahali ambapo Bwana anatutaka." Kwa maana hiyo, Papa Leo XIV aliwatia moyo katika kuwahudumia maskini, wakiwemo wahamiaji, wafungwa, na wagonjwa, na pia katika kujitolea kwao kukuza ikolojia fungamni katika ulinzi wa uumbaji na wa watu katika maeneo wanayofanya kazi. Mwishowe, alikumbuka upendo wao mkubwa kwa Mama Yetu na kuwataka waendelee kukuza sala na kujitolea kwake. Kabla ya kutoa Baraka yake ya Kitume, Baba Mtakatifu aliomba kwamba Maria, aliye Msalabani, mwenye nguvu na mwaminifu, awaoneshe jinsi ya kubaki kando ya misalaba isiyohesabika ambapo Kristo bado anateseka katika kaka na dada zake, ili kuwaletea faraja, ushirika, msaada, na mkate wa thamani wa upendo.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

24 Novemba 2025, 15:00