Papa Leo XIV maombi ya sala zimsindikize katika ziara yake ya Turkiye na Lebanon
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Mara baada ya Katekesi yake, tarehe 26 Novemba 2025 Papa Leo XIV akiwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa waamini na mahujaji waliofikia alieleza juu ya ziara yake ya kitume itakayo muona Nchi za Mashariki ya Kati kuanzaia tarehe 27 Novemba hadi Desemba 2. Kwa njia hiyo Papa alisema: “Kesho nitasafiri kwenda Uturuki na kisha Lebanon kuwatembelea watu wapendwa wa nchi hizo, matajiri katika historia na mambo ya kiroho.” Kwa kuongeza “ Pia itakuwa fursa ya kuadhimisha miaka 1700 ya Mtaguso wa kwanza la Kiekumeni ulioadhimishwa Nicea na kukutana na jumuiya ya Wakatoliki, kaka na dada zetu Wakristo, na wale wa dini zingine. Ninawaomba mnisindikize kwa sala zenu.”
Papa aliwasalimia mahujaji kwa lugha mbali mbali na kawa upande wa kiitalinao alisema: “Ninawakaribisha kwa dhati waamini wanaozungumza Kiitaliano, hasa wale kutoka parokia za Battipaglia, Sapri, na Vico Equense. Ninawasalimu waamini wa Battenti ya Mtakatifu Filomena, Kwaya ya Mikono Mizungu ya Chiavari, Baraza la Kitaifa la Wataalamu wa Viwanda, Chama cha ANSI cha Faenza, na Chama cha ACAI cha Napoli.”
Papa aliongeza kusema kuwa “Ninawahimiza kila mtu kuendelea kwa kujitolea na ukarimu katika shughuli zao husika. Na hatimaye, nawasalimu wagonjwa, wenyendoa wapya, na vijana, hasa wanafunzi wa Mtakatifu Giovanni Rotondo na Triggiano.
Kipindi cha majilio
Dominika ijayo, tarehe 30 Novemba Kanisa litaanza tena mzunguko mpya wa kusherehekea mafumbo ya Kikristo, katika Dominika ya kwanza ya Majilio. “Wakati huu wa mwaka unatuandaa kwa ajili ya Noeli ukiamsha kwa kila mtu hamu ya kukutana na Mungu anayekuja. Baraka zangu kwa wote!”
