Tafuta

2025.11.20 Ziara ya Papa: Baba Mtakatifu Leo akisali mbele ya kaburi la Mtakatifu Francis wa Assisi. 2025.11.20 Ziara ya Papa: Baba Mtakatifu Leo akisali mbele ya kaburi la Mtakatifu Francis wa Assisi.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV asali katika kaburi la Mt.Francis:"Dunia inatafuta ishara za matumaini"

Leo XIV aliwasili Assisi,Novemba 20,kukutana na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Italia(CEI) waliokusanyika kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa 81.Kabla ya mkutano huo alikwenda katika Basilika ya chini ya Mtakatifu Francis ili kutoa heshima katika Kaburi la Mtakatifu huyo.

Na Benedetta Capelli - Assisi

"Ni baraka kuweza kuja hapa leo katika mahali hapa patakatifu. Tunakaribia maadhimisho ya miaka 800 ya kifo cha Mtakatifu Francis, na hii inatupatia fursa ya kujiandaa kumsherehekea Mtakatifu huyu mkuu, mnyenyekevu, na maskini huku ulimwengu ukitafuta ishara za matumaini." Haya yalikuwa maneno ya kwanza ya hadharani ambayo Papa Leo XIV aliyasema huko Assisi, mbele ya kaburi la Mtakatifu Francis, kituo cha kwanza katika ziara yake katika mji wa Umbria ambapo  Alhamisi tarehe 20 Novemba 2025, anakutana na Maaskofu wa Baraza la  Maaskofu wa Italia(CEI), wakihitimisha Mkutano wao Mkuu wa 81.

Kuwasili Assisi

Papa aliwasili asubuhi kwa helikopta, akitua baada ya kuondoka saa 2:00 na kufika saa 2.30 asubuhi majira ya Ulaya katika Uwanja wa Migaghelli huko Mtakatifu Maria wa Malaika. Kutoka hapo, alikwendesha kwa gari hadi katikati ya jiji la Poverello, yaani Maskini eneo la sanaa, historia, utamaduni, na ibada, mahali pa mamilioni ya mahujaji, wakiwemo Mapapa ishirini ambao wametembelea kwa karne nyingi. Zaidi ya yote, Papa Francisko, ambaye pia alisaini hati ya Fratelli Tutti yaani Wote ni Ndugu mwaka 2020.

Il Papa nella cripta della Basilica inferiore di San Francesco, dinanzi alla tomba del Poverello

Papa akiwa chini ya Kanisa Kuu mahali palipo na Kaburi la Mtakatifu Francis  (@Vatican Media)

Karibu katika Basilika ya Chini

Sasa ni zamu ya Papa Leo XIV. Kabla ya kwenda kwenye Basilika ya Mtakatifu Maria wa Malaika kwa ajili ya Mkutano wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia(CEI,) muda mfupi baada ya saa 8:30 asubuhi majira ya Ulaya, Papa Leo XIV alitembelea kaburi la Mtakatifu Mlinzi wa Italia. Waliomsubiri Papa Leo  katika uwanja huo, chini ya mvua kubwa na halijoto ya baridi kali, kulikuwa na waamini kadhaa waliomkaribisha kwa nyimbo: "Viva il Papa."

Waliokuwepo kwenye mlango wa Basilika walikuwa ni rais wa CEI, Kardinali Matteo Zuppi, na Mkuu wa Konventi Takatifu, Ndugu Marco Moroni. Pamoja na watawa wengine, waliomsindikiza Mrithi wa Petro chini kabisa ya Basilika ya Chini, inayomulikwa na taa kubwa iliyotolewa mwaka huu 2025 na Mkoa wa Abruzzo, kama utamaduni wa Italia, ambapo kumeandikwa maneno kutoka kwa Mwandishi Mkuu Dante katika Andiko la 'Paradiso': "Non è che di suo lume un raggio," yaani: "Ni mwanga tu wa mwanga wake." Hii ni heshima inayokuja tunapokaribia sherehe za kumbukumbu ya miaka 800 ya kifo chake pamoja na kuoneshwa kwa mabaki yake.

Sala kwenye kaburi la 'Poverello'-Maskini

Huko, mbele ya kuta zile za mawe za kale ambazo, moja kwa moja chini ya madhabahu kuu ya Basilika, huhifadhi mwili wa mtakatifu, kulikuwa na wakati wa ukimya na kutafakari. Kisha, Papa alitoa maneno machache, yaliyosikika pia nje kupitia vipaza sauti, yalirudia ujumbe wa matumaini kwamba mtu huyu mdogo lakini mkubwa, karne nyingi baadaye, anaendelea kuenea katika Kanisa na Ulimwengu.

Il saluto del Papa dalla Basilica inferiore di San Francesco

Salamu ya Papa kutoka katika Basilika ya chini ya Mtakatifu Francis(@Vatican Media)

Papa Assisi

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

 

20 Novemba 2025, 10:02