Papa Leo XIV akutana na Waziri Mkuu wa Giorgia
Vatican News
Jumatatu asubuhi tarehe 24 Novemba 2025 Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana katika Jumba la Kitume, mjini Vatican na Bwana Irakli Kobakhidze, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Giorgia, ambapo baada ya Mkano huo alikutana na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akisindikizana na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa vatican wa mahusinao na Nchi na Mashirika ya Kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa za Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, ilibanisha kuwa Wakati wa majadiliano ya kirafiki katika Sekretarieti ya Vatican kuridhika kulioneshwa kwa uhusiano mzuri kati ya Vatican na Georgia, na baadhi ya vipengele vya maisha ya Kanisa Katoliki nchini viliakisiwa. Wakati huo huo, umakini ulipewa kwa mada zingine zenye maslahi ya pande zote, hasa masuala yanayohusu uhusiano wa pande mbili, masuala ya kikanda, na changamoto zinazoikabili nchi.
