Ndege ya Papa Leo XI imeondoka kutoka Istanbul kuelekea Lebanon
Vatican News
Ilikuwa saa 9:01 alasiri (saa za ndani, uturuki,) Dominika tarehe 30 Novemba 2025 ambapo Ndege aina ya "ITA Airbus A320neo" iliyokuwa imembeba Papa Leo XIV awali, pia iliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Atatürk huko Istanbul kuelekea Beirut, mji mkuu wa Lebanon, ambapo Papa ataendelea kuwapo hadi Jumanne, tarehe 2 Desemba 2025, kama sehemu ya Ziara yake ya kwanza ya Kitume kimataifa.
Ziara ya Siku 4 ya Papa nchini Uturuki
Hatua hii inahitimisha ziara ya siku nne ya Papa nchini Uturuki (Türkiye). Miongoni mwa mambo muhimu ya ziara hiyo ni kumbukumbu ya pamoja na Patriaki Bartholomew I na viongozi na wawakilishi wa Makanisa ya Kikristo Ulimwenguni, ya kumbukumbu ya miaka 1,700 ya Mtaguso wa Kwanza la Kiekumeni katika historia, iliyofanyika huko Nicaea, ambapo kwa sasa panaitwa Iznik. Ilikuwa ni sherehe ya utulivu na takatifu, iliyofanyika juu ya magofu ya Basilika ya kale ya Mtakatifu Neophytos, ambapo Papa Leo XIV alihimiza kushinda "kashfa ya mgawanyiko" na kukuza "umoja."
Makaribisho huko Lebanon
Katika uwanja wa ndege wa Beirut, uliopewa jina la Waziri Mkuu wa zamani Rafiq Hariri, ambaye aliuawa pamoja na maafisa wake wa usalama katika shambulio la tarehe 14 Februari 2005, Papa atakaribishwa na Balozi wa Vatican na Mkuu wa Itifaki wa Lebanon.
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa ungependa kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu kwa kubofya hapa: cliccando qui
