Tafuta

Wakimbizi wa ndani nchini Sudan. Wakimbizi wa ndani nchini Sudan.  (AFP or licensors)

Papa Leo XIV:"Hatuwezi kuzoea vita na uharibifu."

Mara baada ya Tafakari na kusali sala ya Malaika wa Bwana Novemba 16,Papa alitaja mashambulizi dhidi ya jamii na sehemu za ibada nchini Bangladesh,Nigeria,Msumbiji, Sudan na maeneo mengine.Alikumbuka shambulio kubwa la kigaidi huko Kivu,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,ambalo liliua watu wasiopungua ishirini.Aliwaombea watu wa Ukraine,akiwasihi wasizoea"vita na uharibifu na akaelezea ukaribu wake na wale walioathiriwa na ajali ya barabarani hivi karibuni kusini mwa Peru.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana akiwageukia Waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican,  Domika tarehe 16 Novemba 2025, ikiwa ni Jubilei ya Maskini sambamba na Siku ya IX  ya  Maskini  Duniani, Baba Mtakatifu alisema: “ Kama nilivyosema hapo awali katika tafakari yangu kuhusu Injili, hata leo hii, katika sehemu mbalimbali za dunia, Wakristo wanakabiliwa na ubaguzi na mateso. Nafikiria hasa Bangladesh, Nigeria, Msumbiji, Sudan, na nchi zingine, ambazo mara nyingi tunasikia ripoti za mashambulizi dhidi ya jamii na maeneo ya ibada.”

Shambulizi la kigaidi DRC

Baba Mtakatifu alingeza “Mungu ni Baba mwenye huruma na anatamani amani miongoni mwa watoto wake wote! Ninawasindikiza  familia huko Kivu, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambapo katika siku za hivi karibuni kumekuwa na mauaji ya raia, angalau wahanga ishirini wa shambulio la kigaidi. Tuombe kwamba vurugu zote zikome na waumini watafanya kazi pamoja kwa manufaa ya wote.

Mashambulizi huko Ukraine

Papa kadhali aligeukia Nchi ya Ulaya Kaskazini kwamba “Nimesikitishwa na habari za mashambulizi yanayoendelea kuikumba miji mingi ya Ukraine, ikiwa ni pamoja na Kyiv. Yanasababisha vifo na majeraha, ikiwa ni pamoja na watoto, na uharibifu mkubwa wa miundombinu ya raia, na kuacha familia bila makazi kadri hali ya hewa ya baridi inavyoendelea. Ninawahakikishia ukaribu wangu watu walioathiriwa vibaya sana. Hatuwezi kuzoea vita na uharibifu! Tuombe pamoja kwa ajili ya amani ya haki na imara katika Ukraine iliyoteswa.”

Papa wa Roma aliendelea kutazama hali halisi ya dunia tena na kusema “Pia ningependa kuwahakikishia ukaribu wangu waathiriwa wa ajali mbaya ya barabarani iliyotokea Jumatano iliyopita kusini mwa Peru,” na “kwa  maombi yangu Bwana awakaribishe marehemu, awasaidie waliojeruhiwa, na awafariji familia zinazoomboleza.”

Kutangazwa kuwa Mwenyeheri   

Papa amekumbuka tukio jingine la Jumamosi tarehe 15 Novemba 2025,  “huko Bari, Carmelo De Palma, kuhani wa  aliyefariki mwaka wa 1961 baada ya maisha yake kwa ukarimu katika huduma ya Ungamo na mwongozo wa kiroho, alitangazwa kuwa Mwenyeheri. Ushuhuda wake uwatie moyo mapadre kujitoa bila masharti kwa ajili ya kuwahudumia watu watakatifu wa Mungu.”

Siku ya Maskini

Papa akigeukia fursa ya Siku, alisema ““Leo tunaadhimisha Siku ya Maskini Duniani. Ninawashukuru wale walio katika majimbo na parokia ambao wamekuza mipango ya mshikamano na walio katika hali ngumu zaidi. Na vyema, katika Siku hii, ninarudisha Wosia wa Kitume Dilexi te, "Nimekupenda," kuhusu upendo kwa maskini, hati ambayo Papa Francisko alikuwa akiiandaa katika miezi ya mwisho ya maisha yake na ambayo niliikamilisha kwa furaha kubwa.” Katika siku hii, tunawakumbuka pia wale wote waliokufa katika ajali za barabarani, mara nyingi husababishwa na tabia ya kutowajibika. Kila mtu achunguze dhamiri yake kuhusu jambo hili.”

Siku ya kuombea waathriwa wa manusura ya unyanasaji Italia

Pia Papa alipenda “kuungana na Kanisa nchini Italia katika kupendekeza “Siku ya Maombi kwa Waathiriwa na Manusura wa Unyanyasaji, ili utamaduni wa heshima uweze kukua kama dhamana ya kulinda utu wa kila mtu, hasa watoto wadogo na walio katika mazingira magumu zaidi.”

Salamu mbali mbali kwa mahujaji

Badaye Papa aliwasalimia  kwa upendo, Warumi na mahujaji kutoka Italia na kutoka sehemu nyingi za dunia, hasa waamini kutoka Bar huko Montenegro, Valencia huko Hispania, Syros huko Ugiriki, Puerto Rico, Sofia huko Bulgaria, Bismarck huko Marekani, wanafunzi wa Umoja wa Kitaalimungu wa Katoliki wa Chicago, na Kwaya ya "Eintracht Nentershausen" kutoka Ujerumani.

Aliwasalimu mahujaji wa Poland, “nikikumbuka kumbukumbu ya Ujumbe wa Upatanisho uliotolewa na Maaskofu wa Poland kwa Maaskofu wa Ujerumani baada ya Vita vya Pili vya Dunia.”

Na hatimaye Papa alima: “ Mwishowe, ninawasalimu Familia ya Mtakatifu Vincenti di Pauli na vikundi kutoka Lurago ya Erba, Coiano, Cusago, Paderno Dugnano, na Borno. Asanteni nyote na muwe na Dominika njema!”

Mara baada ya Angelus Nov 16

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

16 Novemba 2025, 14:52