Tafuta

Papa katika moja wapo ya Katekesi yake. Papa katika moja wapo ya Katekesi yake.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:"Nguvu ya Injili."Imani ya Kikristo katika maneno 10

Maandishi ambayo hayajachapishwa ya Papa katika Kitabu kipya cha Nyumba ya Uchapishaji ya Vatican(LEV):"Nguvu ya Injili:Imani ya Kikristo katika Maneno 10,"ni mkusanyiko wa hotuba na Katekesi za Papa Leo XIV zilizopangwa kuzunguka mada muhimu za Kikristo."Hamu ya ushirika,kujitambua kama ndugu,ndiyo dawa ya msimamo mkali wote,"Papa anaandika katika kitabu hicho,kitakachotolewa Novemba 20,ambacho kitawasilishwa katika miji kadhaa ya Italia.

Vatican News

"Hatuwezi tena kuvumilia dhuluma za kimuundo ambapo wale walio na zaidi, wana zaidi na zaidi, na kinyume chake, wale walio na kidogo, wanazidi kuwa maskini." Hivi ndivyo Papa Leo XIV anavyoandika katika utangulizi ambao haujachapishwa wa kitabu chake kipya, Nguvu ya Injili: Imani ya Kikristo katika Maneno 10, ambacho kitachapishwa kwa Kiitaliano mnamo Novemba 20 na Nyumba ya Uchapishaji vitabu ya Vatican(LEV).

Kifuniko cha Kitabu kipya cha LEV cha Papa Leo XIV "Nguvu ya Injili"
Kifuniko cha Kitabu kipya cha LEV cha Papa Leo XIV "Nguvu ya Injili"

Kujitambua kama Ndugu

Kitabu hiki, kilichohaririwa na Lorenzo Fazzini, mkurugenzi wa uhariri wa Nyumba ya Uchapishaji Vitabu, Vatican (LEV) ni mkusanyiko wa hotuba na hoMahbiri ya Papa Leo XIV, zilizopangwa karibu na mada kumi muhimu za Kikristo, zilizowasilishwa kwa mpangilio huu: Kristo, moyo, Kanisa, utume, ushirika, amani, maskini, udhaifu, haki, tumaini. Katika Utangulizi wake, Papa Leo XIV, akiangalia hali ya ulimwengu wa kisasa, anasema: "Hatari ya chuki na vurugu, kama mteremko unaoteleza, kufurika hadi taabu ienee miongoni mwa watu." Akikabiliana na hili, Papa Prevost anabainisha suluhisho linalowezekana kuwa: "Shauku yenyewe ya ushirika, kutambuliwa kwa ndugu zetu, ndiyo dawa ya msimamo mkali wote."

Mawasilisho ya Vitabu nchini Italia

Kitabu cha Nguvu ya Injili kitakuwa mada ya mikutano kadhaa ya hadhara katika siku zijazo katika miji kadhaa ya Italia, iliyoandaliwa na LEV na mashirika kadhaa ya kikanisa na kiutamaduni. Tarehe hizo ni: Novemba 21, Vicenza na Cremona; Novemba 25, Trento; Desemba 1, Verona; Desemba 5, Genova; Desemba 15, Cagliari. Mbali na uwasilishaji wa kitabu, makala "León de Peru" na "Leo kutoka Chicago" ya hivi karibuni yataoneshwa. Makala hizi, zilizotayarishwa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano, zinalenga kazi ya umisionari ya Prevost nchini Peru na asili  yake ya Marekani.

Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui

 

13 Novemba 2025, 18:37