Papa Leo katika Msikiti wa Bluu,Istanbul kwa kutafakari na kusikiliza!
Vatican News
Papa Leo XIV alitembelea Msikiti kwa ukimya, katika roho ya kutafakari na kusikiliza, kwa heshima kubwa mahali hapo na kwa imani ya wale waliokusanyika hapo kwa maombi. Hii ilikuwa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Vatican kwenye Telegram, ikimaanisha ziara ya Papa Leo XIV kwenye Msikiti wa Sultan Ahmed huko Istanbul, nchini Türkiye-Uturuki, ambao pia unajulikana kama Msikiti wa Bluu, ziara ambayo ilifanyika asubuhi ya Jumamosi tarehe 29 Novemba 2025.
Ni Msikiti wa kipekee kweli, wenye vigae 21,043 vya kauri ya zumaridi vilivyowekwa ndani ya kuta, ndani yake ina dari kubwa iliyoakisiwa na madirisha 260. Ni katika eneo hili lenye hisia kali ambapo Papa Leo XIV alisimama kwa mara ya kwanza katika siku yake ya tatu nchini Uturuki (Türkiye).
Ilikuwa mnamo tarehe 29 Novemba 2014, Papa Francisko aliingia Msikitini bila viatu na akasimama kwa maombi ya kimya kimya kando ya Mufti Mkuu, akirudia kile ambacho Papa Benedikto XVI alichofanya miaka iliyopita, alipofika Uturuki mwaka 2006 baada ya utata uliozunguka kutoeleweka kwa hotuba yake ya Regensburg, ambayo ilitatuliwa kwa ziara yake nchini humo. Papa Francisko aliingia Msikiti wa Bluu mnamo Novemba 30, bila ratiba, na akasali kimya kimya kabla ya "mihrab," sehemu ya marumaru inayoonesha mwelekeo wa Makka, pamoja na Mufti Mkuu wa jiji, Mustafa Kagrici, ambaye alikuwa amemwalika kwenye ishara hiyo tu ya kukumbuka pamoja.
![]()
Papa Francisko alitembelea Msikiti wa Bluu huko Istanbul, 2014
Katika Katekesi ya tarehe 6 Desemba 2006, Papa alizungumzia wakati huo na sala aliyotoa: Katika muktadha wa mazungumzo kati ya dini mbalimbali mapenzi ya Mungu yaliniruhusu, karibu na mwisho wa safari yangu, kufanya ishara ambayo mwanzoni haikutarajiwa, ambayo ilithibitika kuwa muhimu sana: ziara ya Msikiti maarufu wa Bluu huko Istanbul. Nikisimama kwa dakika chache nikikumbuka mahali hapo pa sala, nilimgeukia Bwana mmoja wa Mbingu na Dunia, Baba mwenye Huruma wa wanadamu wote. Waamini wote wajitambue kama viumbe vyake na washuhudie udugu wa kweli!"
![]()
Kunako 2006 Papa Benedikto XVI alitembelea Msikiti wa bluu
Msikiti wa Bluu ni mojawapo ya misikiti muhimu zaidi huko Istanbul. Ulijengwa (1609–1617) na Sultan Ahmed I, katika sehemu ya eneo la Jumba Kuu la Constantinople, ili kuwa mahali muhimu zaidi pa ibada katika Milki ya Ottoman. Mpango wa ujenzi ulielezewa kwa uangalifu katika vitabu nane, ambavyo sasa zimehifadhiwa katika Maktaba ya Topkapi. Msikiti wa Bluu ndiyo pekee ulio na minara sita, ikilinganishwa na minne ya kawaida, ikizidiwa tu na Msikiti wa Kaaba huko Makka, ambao una minara saba.
Upekee huu wa usanifu unatokana, kulingana na historia maarufu, na kutoelewana: Sultan Ahmed I, ambaye hakuweza kulinganisha uzuri wa msikiti wa Sultan Süleymaniye huko Istanbul, hakupata njia bora ya kuutofautisha kuliko minara ya dhahabu. Hata hivyo, mbunifu hakuelewa maneno ya sultani, akielewa "altr" (Kituruki maana yake "sita") badala ya "altin" (dhahabu).
Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui
