Papa Leo XIV:kuanzia 25 al 27 Septemba 2026,Siku ya Watoto Ulimwenguni
Vatican News.
Katekesi ya Papa Leo XIV alitangaza kwamba Siku ya pili ya Watoto Duniani itafanyika Roma kuanzia tarehe 25 hadi 27 Septemba 2026. Siku ya Watoto Duniani, iliyotangazwa na Baraza la Kipapa la Walei, Familia na Maisha, itakuwa wakati wa kukutana, kusali, na kusherehekea watoto na familia zao kutoka ulimwenguni kote. Hata hivyo mwishoni mwa Katekesi hiyo, Majd Bernard mwenye umri wa miaka saba kutoka Gaza na Padre Enzo Fortunato waliwasilisha na kumwonesha Papa bendera yenye nembo rasmi ya Siku ya Watoto Ulimwwenguni ijayo. Kisha Papa akabariki na kusaini bendera, ambayo imekuwa ishara ya safari inayoelekea kwenye tukio la 2026.
Uzuri wa Amani
"Katika Siku ya Watoto Ulimwenguni ijayo, Kanisa linataka tena kuzingatia ulimwengu wa utoto na mazingira asilia ambayo watoto wanaishi na kukua, yaani, familia," alitangaza Kardinali Kevin Farrell, Mwenyekiti wa Baraza la Walei, Familia, na Maisha. "Watoto lazima waoneshwe uzuri wa amani, amani inayopatikana kwanza kabisa ndani ya familia zao, katika mazingira wanayoishi mara kwa mara, na katika ulimwengu kwa ujumla. Watoto wanaelewa thamani ya amani vizuri na wanateseka sana wanapoona mivutano na migogoro inayowazunguka, kuanzia na wazazi wao au katika mazingira yao ya karibu. Kwa hivyo tunatumaini kwamba Siku ya Watoto Ulimwenguni ijayo itakuwa fursa nzuri kwa Kanisa kuonesha ukaribu wake kwa watoto na familia zao, kuwapa matumaini na furaha."
"Ninamshukuru Baba Mtakatifu na Kardinali Kevin Farrell kwa umakini wao na wema wao hadi leo, muhimu sana kwa Kanisa na jamii. Watoto na familia zao watapitia siku zilizojaa kusikiliza na kushiriki.
Pamoja na Papa Leo,” alitangaza Padre Enzo Fortunato, “tutasema kwamba mustakabali bora unawezekana. Data kutoka kwa mashirika ya kimataifa zinasema wazi: Zaidi ya watoto bilioni mbili wanaishi duniani, kila siku takriban watoto 13,000 walio chini ya umri wa miaka mitano hupoteza maisha yao kwa sababu zinazoweza kuzuilika, na mamilioni wanaishi katika maeneo ya migogoro, ambapo vita vinawazuia kujenga mustakabali.
Maana ya Nembo
Alama za mikono katikati ya Nembo zinakumbusha ishara rahisi na halisi za utoto, ishara ya ulimwengu na usafi wa watoto wadogo. Rangi tofauti zinawakilisha wingi wa tamaduni ambazo, zikiungana, huunda maelewano yenye uwezo wa kukumbatia na kuthamini tofauti. Nyayo hizo saba zinarejea mabara saba, huku Paa la Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, linaloashiria makao makuu ya kudumu ya Siku hiyo, likionekana kama kukumbatia kuwakaribisha na kuwalinda watoto kutoka ulimwenguni kote huku msalaba ukikumbusha mateso na ufufuo wa Kristo.
Toleo la kwanza 2024
Toleo la kwanza la Siku ya Watoto Duniani, lililofanyika mwaka 2024, lilishuhudia ushiriki wa takriban watoto 100,000 kutoka mataifa 101. Kwa toleo la pili mwaka 2026, Kanisa linarejea kujitolea kwake kusikiliza na kuthamini sauti za vijana, wahusika wakuu wa ulimwengu unaotamani amani, kukubalika, na mustakabali.
Siku ya Pro Orantibus
Baba Mtakatifu katika salamu zake kwa lugha lakini zaidi katika lugha ya kiitaliana alikumbusha tukio la kumbukumbu ya Kanisa kwamba “tarehe 21 Novemba ni kumbukumbu ya kiliturujia ya Kuwasilishwa Hekaluni kwa Bikira Maria, Siku ya "Pro Orantibus", yaani ya Watawa wa Ndani, ambayo itaadhimishwa Italia yote.” Kwa njia hiyo Papa aliongeza kusema “kaka na dada zetu wote katika maisha ya kutafakari wapokee mshikamano halisi na usaidizi mzuri wa jumuiya ya kikanisa ili kuhakikisha uhai na mwendelezo wa utume wao wa kimya, wenye matunda, na usioweza kubadilishwa.”
Papa aliwakaribisha kwa joto waamini wanaozungumza Kiitaliano, na hasa, ninawasalimu washiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Skauti, Chama cha "Il Testimone del volontariato d'Italia", vikundi vya Klabu ya Propeller ya Italia, Jeshi la Wanamaji la Taranto, Amri ya Kitaifa ya Jeshi la Eneo, wanafunzi wa Shule za Maestre Pie Venerini, kundi la UNITALSI, waumini wa Lauria na wale wa Arena Bianca.
Siku ya Wavuvi Duniani Novemba 21
Vile vile katika kuelekea siku ya Wavuvi duniani inayoadihsimishwa tarehe 21 Novemba, Papa alisema “Natamani kuwakumbuka wavuvi katika Siku ya Uvuvi Duniani, ambayo itaadhimishwa Ijumaa ijayo:” Mariam, Nyota ya Bahari, awalinde wavuvi na familia zao.
Siku ya Watoto Ulimwenguni 25-27 Septemba 2026
Mawazo yangu pia yaliwageukia watoto, ambao atakuwa na furaha ya kukutana nao katika Siku iliyopangwa kwao, a kufanyika 25 -27 Septemba 2026.
Siku Kuu ya Kristo Mfalme sambamba na Siku ya Vijana Duniani 23 Novemba
Mwishowe, aliwakaribisha kwa upendo vijana, wagonjwa, na wenye ndoa wapya. Dominika Ijayo ambayo ni Dominika ya mwisho ya Wakati wa Kawaida, tutasherehekea siku kuu ya Kristo, Mfalme wa Ulimwengu.
“Vijana wapendwa, mwekeni Yesu katikati ya maisha yenu. Kristo, aliyeufanya Msalaba kuwa kiti cha enzi cha kifalme, awafundishe, wagonjwa wapendwa, kuelewa thamani ya ukombozi ya mateso yanayopatikana katika muungano naye. Ninawaalika, wapendwa wenye ndao za karibuni, kumweka Yesu katikati ya safari yenu ya ndoa.” Na kwa kote, baraka zake.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
