Tafuta

Serikali ya Shirikisho ya Nigeria iliamuru kufungwa kwa shule kufuatia mashambulizi. Serikali ya Shirikisho ya Nigeria iliamuru kufungwa kwa shule kufuatia mashambulizi.  (ANSA)

Papa Leo XIV:mateka waachiliwe mara moja huko Nigeria na Cameroon

Baada ya Misa ya Sherehe ya Kristo Mfalme,iliyoadhimishwa Novemba 23,katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Papa Leo alitoa wito wa dhati kuachiliwa huru kwa wanafunzi na mapadre waliotekwa nyara katika siku za hivi karibuni huko Nigeria na Cameroon.Papa alikumbusha Siku ya vijana Kimajimbo Ulimwenguni kote na kukumbusha Ziara ijayo ya Kitume nchini Uturuki na Lebanon na kutangaza Waraka wa Kitume:"In unitate fidei"-"Katika umoja wa imani."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Nilipokea kwa huzuni kubwa habari za utekaji nyara wa makuhani, waamini, na wanafunzi nchini Nigeria na Cameroon. Ninahisi uchungu mwingi, hasa kwa vijana wengi waliotekwa nyara na kwa familia zao zenye uchungu. Ninatoa ombi la kutoka moyoni kwa ajili ya kuachiliwa huru mara moja kwa mateka na kuwasihi mamlaka husika kuchukua maamuzi sahihi na kwa wakati unaofaa ili kuhakikisha wanaachiliwa huru. Tuwaombee hawa kaka na dada zetu, na kwamba kila wakati na kila mahali makanisa na shule zibaki kuwa mahali pa usalama na matumaini.”

Papa na mtoto aliyevalia nguo  za kipapa
Papa na mtoto aliyevalia nguo za kipapa   (@Vatican Media)

Huu ni wito wa Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, ya Sherehe za Kristo Mfalme, Jubilei  ya  Kway ana  Siku ya Vijana Kijimbo Ulimwenguni,  Dominika tarehe 23 Novemba 2025.

Jubilei ya Kwaya

Hata hivyo Baba Takatifu kwana alisema kuwa  “Kabla hatujasali pamoja kwa Malaika wa Bwana, ningependa kuwasalimu nyote mlioshiriki katika sherehe hii ya Jubilei, hasa kwaya kutoka kote ulimwenguni. Asante kwa uwepo wenu! Na Bwana abariki huduma yenu! “Ninatoa salamu zangu kwa mahujaji wengine wote, hasa ACLI ya Jimbo la Teramo-Atri na waamini kutoka majimbo kadhaa nchini Ukraine: mpeleke nyumbani mkumbatio  na sala katika Uwanja huu.”

Siku ya vijana duniani

“Leo, ni  Siku ya Vijana Duniani inaadhimishwa katika majimbo  ulimwenguni kote. Ninawabariki na kuwakumbatia kiroho wote wanaoshiriki katika sherehe na mipango mbalimbali. Katika Sherehe  ya Kristo Mfalme, ninaomba kwamba kila kijana agundue uzuri na furaha ya kumfuata Yeye, Bwana, na kujitolea kwa Ufalme Wake wa upendo, haki, na amani!”

Papa akizungukia Uwanja kusalimia mahujaji
Papa akizungukia Uwanja kusalimia mahujaji   (@Vatican Media)

Ziara ya Uturuki

“ Safari yangu ya kitume kwenda Uturuki na Lebanon sasa inakaribia. Maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea yataadhimishwa nchini Uturuki. Kwa hivyo, Waraka wa Kitume wa In unitate fidei yaani “Katika umoja wa imani” unaoadhimisha tukio hili la kihistoria, unachapishwa leo.” Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu aliwaomba kuumgeukia Bikira Maria, tukikabidhi nia hizi zote na maombi yetu ya amani kwa maombezi yake ya mama.”

Baada ya Angelus
23 Novemba 2025, 16:23