Tafuta

2025.11.17 Papa akutana na wahusumu katika nafasi ya kidiplomasia kwenye Balozi za Vatican katika nchi mbali mbali. 2025.11.17 Papa akutana na wahusumu katika nafasi ya kidiplomasia kwenye Balozi za Vatican katika nchi mbali mbali.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Pelekeni Matumaini mahali inapokosekana Amani na haki

Katika hafla ya Jubilei ya wahudumu wa Ofisi za Balozi za Kipapa za Vatican katika nchi mbali mbali Papa Leo XIV alikutana nao tarehe 17 Nvemba,mjini Vatican na kuwashukuru kwa kujitolea kwao kwa thamani,lakini kazi ngumu,katika kuleta utunzaji wa kichungaji wa Kanisa zima hata katika maeneo yanayopitia magumu na ukosefu wa utulivu.Alifafanua kuwa utamadunisho si mtazamo wa kitamaduni na kwa hiyo aliwasihi wasijitenge bali wawe mahujaji wa matumaini mahali walipotumwa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alikutana na  Wahudumu wa Kidiplomasia katika Balozi za Vatican kwenye nchi mbalimbali na Mashirikia ya Kimataifa, tarehe  17 Novemba 2025 katika Ukumbi wa Clementina mjini Vatican. Ni katika muktadha wa  kuadhimisha Jubilei yao ambapo Papa alianza kwa kutoa shukrani kwa  Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin,   kwa maneno yake mazuri, na pia kwa Wakuu wa Sekretarieti ya Vatican hasa Katibu Msaidizi wa Uwakilishi wa Kipapa na kile kinachoitwa Kitengo cha  Tatu cha Vatican katika Masuala ya Mahusiano na Nchi na Mashirika ya Kimataifa, ambacho kiliandaa kwa uangalifu siku hizi za udugu, sala, na mazungumzo.

Papa leo alisema kuwa uwepo wao ni chanzo cha furaha maalum kwa Papa Leo XIV kwa sababu alisema ni  kwa mara ya kwanza awakaribisha wote pamoja. Tukio hili ni muhimu sana: Jubilei ya Matumaini. Wao pia, kama mahujaji wengi, wamefika Roma, kwenye Kaburi la Mtume Petro, ili kuthibitisha imani yao na kupyaisha maazimio yanayohamasisha huduma yao. “Mtu anaweza kusisitiza kweli kwamba tumefanya hivi, nanyi mmefanya hivyo, pamoja na watu wote wa Mungu, na jinsi ilivyo muhimu kutambua kwamba huduma yenu iko pamoja na watu wa Mungu, si tofauti nao. Na hivyo, kufika kwenye hija ni njia ya kutembea pamoja na Kanisa lote,” Papa alisisitiza.

Katibu wa Vatican akitoa hotuba yake kwa Papa
Katibu wa Vatican akitoa hotuba yake kwa Papa   (@VATICAN MEDIA)

“Mwaka Mtakatifu ni fursa ya majaliwa kwetu sote kugundua upya na kuimarisha uelewa wetu wa uzuri wa wito wetu, yaani, wito wetu wa pamoja wa utakatifu, unaotufanya kila siku kuwa mashuhuda wa Kristo, tumaini hai kwa ulimwengu.” Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu awali ya yote alipenda “kuwashukuru kwa sababu, kama Mtume anavyotukumbusha (taz. Flp 3:12), hamkusita mbele ya sauti ya Bwana, anayetualika kumfuata, mkiacha kila kitu nyuma ili kupeleka neno la ukombozi la Injili hadi miisho ya dunia. Wito huu unasikika kwa njia ya pekee kwenu, ambao mmechaguliwa kutekeleza huduma ya kikuhani katika Uwakilishi wa Kipapa: zawadi na kujitolea kuwa uwepo kila mahali kwa Kanisa lote na, hasa, kwa shauku ya kichungaji ya Papa, anayeliongoza kwa upendo.”

Papa alisistiza kuwa, “ Hakika, huduma  yao  maalum ni ngumu na kwa hivyo inahitaji moyo wenye bidii kwa Mungu na wazi kwa wanadamu; inahitaji mafunzo na utaalamu, kujikana na ujasiri; hukua katika kumwamini Yesu na katika unyenyekevu kwa Kanisa ambalo linaoneshwa kupitia utii kwa Wakuu.” Katika nchi wanazofanya kazi, wakikutana na watu na lugha mbalimbali, “wasisahau kwamba ushuhuda wa kwanza unaopaswa kutoa ni ule wa makuhani wanaompenda Kristo na waliojitolea kujenga Mwili wake. Kwa kuhudumia jumuiya za Kanisa, wawe kielelezo cha upendo na ukaribu wa Papa kwa kila mmoja, wakidumisha hisia hai pamoja na Eklesia yaani Kanisa lote.

Wakati wa salamu mmoja baada ya mwingine
Wakati wa salamu mmoja baada ya mwingine   (@VATICAN MEDIA)

Katika muktadha huo, Papa Leo XIV aliwakumbuka na “Kuwafikiria “hasa wale wenu wanaojikuta katika mazingira ya ugumu, migogoro, na umaskini, ambapo nyakati za kukata tamaa hazikosi. Hasa katika mapambano haya, wakumbuka kwamba Kanisa linawaunga mkono katika sala: kwa hivyo, waimarishe utambulisho wao wa kikuhani kwa kupata nguvu kutoka katika Sakramenti, ushirika wa kidugu, na kutoka katika  unyenyekevu wa kila mara hadi kwa Roho Mtakatifu.” Kwa kukuza fadhila hizo za kibinadamu zinazooneshwa katika maneno na matendo ya kila siku, wajenga uhusiano na kila mtu, wakipinga jaribu la kujitenga. Badala yake, waendelee kupandikizwa katika mwili wa kanisa na katika historia ya watu: katika mahali wanapotoka na mahali wao  wanapotumwa.”

Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na nchi na Mashirika ya Kimataifa
Askofu Mkuu Gallagher Katibu wa Vatican wa Mahusiano na nchi na Mashirika ya Kimataifa   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu amesisitiza kwamba kila taita linawaptia tamaduni zake ili wajulikane, wapendwe, na waheshimiwe, kama vile mkulima anavyoheshimu ardhi na, kwa kuilima, huvuna matunda mema ya kazi yake. Kwa hivyo, Papa ametoa onyo kwamba: “msijitenge, bali muwe wanafunzi wenye shauku wa Kristo, mkijizamisha katika njia ya kiinjili katika mazingira mnayoishi na kufanya kazi.” Wamisionari wakuu wanatukumbusha, kiukweli, kwamba utamaduni si mtazamo wa kitamaduni, kwa sababu unatokana na hamu ya kujitolea kwa ardhi na watu tunaowahudumia. Hisia mpya ya kuwa mali wanayoipata haimaanishi mbadala wa mazingira ya kijamii na ya kikanisa yaliyowazaa. Kwa hivyo ni muhimu kuendelea kukuza, iwezekanavyo, uhusiano na Kanisa lao maalum. Hisia hii ya kuwa mali inapopotea, udhaifu huanza: basi tunakuwa kama miti isiyo na mizizi. Hata hivyo, ikiwa itaendelea kupokea damu ya uhai, mti unaweza hata kupandikizwa mahali pengine na hivyo kuzaa matunda mapya.

Askofu Mkuu Edgar Parra,Katibu Msaidizi wa Vatican wa masuala ya Jumla
Askofu Mkuu Edgar Parra,Katibu Msaidizi wa Vatican wa masuala ya Jumla   (@Vatican Media)

Hata hivyo Papa Leo alibainisha tena kwamba katika nyakati za shida, ambazo wakati mwingine tunapitia, ni vizuri kwetu kuthibitisha tena motisha yetu kwa maneno, kwa mfano, ya Mtakatifu Agostino: «Pondus meum, amor meus» (Maungamo XIII, 9) yaani “Uzito wangu, mpenzi wangu."  Hata nabii mkuu Eliya, wakati fulani, alihisi kwamba kazi yake yote ilikuwa bure. Hata hivyo, Bwana alimwinua, akimwonesha lengo fulani na njia ya uhakika ya kuifuata (taz. 1 Wafalme 19:1-18).  Kwa njia hyo Papa aliwaeleza kwamba hata wao wapande  kila siku hadi Horebu yao ya ndani, yaani, mahali ambapo Roho wa Mungu huzungumza na moyo.

Picha ya pamoja na Papa Leo XIV
Picha ya pamoja na Papa Leo XIV   (@VATICAN MEDIA)

Katika kila Uwakilishi wa Kipapa, Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba “ kuna Kanisa, kitovu cha kweli cha nyumba yao, ambapo kila siku, pamoja na Balozi wa Kitume, watawa na washirika, wanaadhimisha Misa, wakiinua maombi ya sifa na sala kwa Bwana. Mwanga wa Hema hilo uondoe vivuli na wasiwasi, ukiangaza njia wanayoifuata. Hivyo Neno la Bwana Yesu linatimia lisemwalo: “ninyi ni chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu (taz. Mt 5:13-14). Kwa kulinda muujiza huu wa neema, Papa aesisitiza “muwe  wanahija wa matumaini, hasa pale ambapo watu hawana haki na amani.”

Papa akiwagaa
Papa akiwagaa   (@VATICAN MEDIA)

Na ni matumaini ya Baba Mtakatifu Leo XIV kwamba “siku hizi wanazotumia katika udugu na sala zinaweza kufufua maisha yao ya kiroho na kuwasaidia kuendeleza kwa bidii utume ambao Kanisa limewakabidhi.” Papa leo XIV kwa njia hiyo aliowaomba wawafikishie  salamu zake kwa  Viongozi wao wakuu wa  Utume ambao wanashirikiana nao, ambao alikutana  nao mwezi Juni  uliopita( akiwa na Maana ya Mabalozi wa Vatican katika nchi mbali mbali aliokutana nao na pia kwa familia zao.  Kwa kuhitimisha Papa aliwakabidhi wote chini ya usimamizi wa Mitume Watakatifu Petro na Paulo, kupitia maombezi ya Bikira Maria, Mama wa Kanisa, na kwa uchangamfu aliwpatia  Baraka yake ya Kitume.

Wahudumu wa Mabalozi
17 Novemba 2025, 18:50