Papa Leo XIV:utakatifu haumo katika sifa zetu,bali katika zawadi ya Bwana
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika siku kuu ya kumbukizi ya kutabarukiwa kwa Kanisa Kuu la Roma pia linaitwa Basilika Kuu ya Mwokozi Mtakatifu ambayo kuno tarehe 9 Novemba 324, Papa Sylvester I aliliweka chini ya Ulinzi wa Kristo Mkombozi wa Ulimwengu baada ya ujenzi wake na ufadhili wake na Mfalme Constantine, Baba Mtakatifu Leo aliongoza tafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Akianza tafakari hiyo alisema “Katika siku ya kutabarukiwa kwa Basilika ya laterano, tutafakari fumbo la muungano na umoja na Kanisa la Roma linaloitwa kuwa Mama ambaye kwa upole wake anatunza imani na safari ya wakristo waliotawanyika ulimwenguni.
Baba Mtakatifu aliendelea kudadavua kuwa Kanisa kuu la Jimbo la Roma na Makao makuu ya Mfuasi wa Petro, kama tujuavyo siyo kazi tu maalumu yenye thamani ya kihistoria, kisanaa, na kidini, bali inawakilisha hata kituo kikubwa cha imani iliyokabidhiwa na kulindwa na Mitume na kusambazwa kwake kwa muda mrefu katika kkipindi cha historia. Ukuu wake wa fumbo unaonekana hata katika uzuri wa kisanii, wa jengo ambalo kweli katika katikati yake linakaribisha sanamu kubwa sana za Mitume, wafuasi wa kwanza wa Kristo na mashuhuda wa Injili.
Baba Mtakatifu aliendelea kueleza kuwa hii inatukumbusha mtazamo wa kiroho, ambao unatusaidia kwenda zaidi ya mtazamo wa kijujuu, kwa kupokea katika fumbo la Kanisa zaidi ya kuwa mahali rahisi, nafasi halisi, ya ujenzi uliofanyika kwa mawe; kwa dhati, kama Injili ilivyotukumbusha, katika tukio la kutakaswa kwa Hekalu la Yerusalemu uliotimizwa na Yesu (Yh 2,13-22), ukweli wa hekalu la Mungu ni Kristo aliyekufa na kufufuka. Yeye ndiye mpatanishi pekee wa wokovu, mwokozi pekee, Yule ambaye kwa kuunganishwa na ubinadamu wetu na kutubadilisha kwa upendo wake, anawakilisha mlango(Yh 10,9) na ambaye anafungua wazi na kutupeleka kwa Baba. Na kwa kuungana Naye, hata sisi tunakuwa mawe hai ya jengo hili la kiroho (1Pt 2,4-5). Sisi ni Kanisa la Kristo, Mwili wake, viungo vyake vilivyoitwa kueneza katika Ulimwengu, Injili yake ya huruma, ya kufariji na ya amani, kwa njia ya ibada ya kiroho ambayo inapassa kuangaza zaidi ya yote katika ushuhuda wa maisha yetu.
Ni katika mtazamo huu wa kiroho ambapo tunapaswa kufundisha mioyo yetu. Mara nyingi, udhaifu na makosa ya Wakristo, pamoja na maneno mengi ya kawaida na ubaguzi, hutuzuia kuelewa utajiri wa fumbo la Kanisa; utakatifu wake, kiukweli, haumo katika sifa zetu, bali katika "zawadi ya Bwana, ambayo haijawahi kufutwa," ambaye anaendelea kuchagua "kama chombo cha uwepo wake, kwa upendo wa fumbo, hata na hasa mikono michafu ya wanadamu"(J. RATZINGER, Kuanzishwa kwa Ukristo, Brescia 2005, 331). Kwa kuhitimisha Papa alisema kwamba “tutembee kwa hiyo katika furaha ya kuwa Watu watakatifu ambao Mungu aliwachagua na kumuomba Maria Mama wa Kanisa, ili atusaidie kukaribisha Kristo na atusindikiza kwa maombezi yake .
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
