Tafuta

Papa Leo XIV: Wakristo wawe wajenzi wa wamani na kuendeleza umoja

Kumekuwa na kutoelewana kwingi na hata migogoro kati ya Wakristo wa Makanisa tofauti hapo awali na bado kuna vikwazo vinavyotuzuia kuwa katika ushirika kamili,lakini hatupaswi kurudi nyuma katika kujitolea kwetu kwa umoja na hatuwezi kuacha kufikiriana kama kaka na dada katika Kristo na kupendana hivyo.Ni katika tafakari ya Papa Leo,Novemba 30 katika Kanisa la Mtakatifu George huko Istanbul,Sikukuu ya Mtakatifu Andrea,Mtume,Msimamizi wa Upatriaki wa Costantinopoli.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu  Leo XIV akiwa katika Ziara yake ya Kwanza ya Kitume, alitoa tafakari yake ya tano katika hitimisho la Liturujia ya Kimungu ya Upatriaki katika Kanisa la Mtakatifu George huko Istanbul, Türkiye, Dominika tarehe 30 Novemba 2025 sambamba na Siku Kuu ya Mtakatifu Andrea, Mtume, Msimamizi wa Upatriaki wa Costantinopoli. Katika misa hiyo Nyimbo za dhati zinazoashiria ibada na miali ya mishumaa, mwanga wa Kristo na ishara ya imani, ilisikika mdundo wa Liturujia Takatifu ya Kiorthodox iliyozama katika mwanga hafifu wa Kanisa la Upatriaki huko Phanar. Mbele ya Patriaki Bartholomew I, Maaskofu, Wajumbe wa Sinodi ya Upatriaki wa Kiekumeni na waamini wengine, ambapo kwa mujibu wa taarifa walikuwa wapatao 400. Papa Leo alianza kusema kuwa Hija yetu katika maeneo ambayo Mtaguso wa Kwanza la Kiekumeni katika historia ya Kanisa ulifanyika,  inakaribia kukamilika kwa Liturujia hii takatifu, ambayo tumemkumbuka Mtume Andrew. Kulingana na mapokeo ya kale, alileta Injili katika mji huu.

Papa katika Kanisa la Mtakatifu George
Papa katika Kanisa la Mtakatifu George   (@Vatican Media)

Imani yake ni sawa na imani yetu, yaani ile iliyofafanuliwa na Mtaguso wa Kiekumeni na unaodaiwa na Kanisa leo hii. Wakati wa sala hii ya kiekumeni, pamoja na Wakuu wa Makanisa na Wawakilishi wa Ulimwengu wa Kikristo tumekumbuka kwamba imani inayodaiwa katika Imani ya Nicea-Constantinopoli inatuunganisha katika ushirika wa kweli na inaturuhusu kutambuana kama kaka na dada. Hapo awali, kumekuwa na kutoelewana kwingi na hata migogoro kati ya Wakristo wa Makanisa tofauti, na bado kuna vikwazo vinavyotuzuia kufikia ushirika kamili. Hata hivyo, hatupaswi kupunguza mwendo katika kujitahidi kuelekea umoja. Ni lazima tuendelee kufikiriana kama kaka na dada katika Kristo na kupendana ipasavyo.

Papa katika kanisa la Mtakatifu George
Papa katika kanisa la Mtakatifu George   (@Vatican Media)

Wakiongozwa na ufahamu huu, miaka sitini iliyopita Papa Paulo VI na Patriaki Athenagoras walitangaza kwa dhati kwamba maamuzi mabaya na matukio ya kusikitisha yaliyosababisha kutengwa kwa pamoja kwa 1054 yanapaswa kuondolewa kwenye kumbukumbu ya Kanisa. Ishara hiyo ya kihistoria ya watangulizi wetu mashuhuri ilizindua njia ya upatanisho, amani na ushirika unaokua kati ya Wakatoliki na Waorthodox, ambao umekuzwa kupitia mawasiliano ya mara kwa mara, mikutano ya kidugu na mazungumzo ya kitaalimungu yenye matumaini. Kwa kuzingatia maendeleo ambayo tayari yamefanywa, hatua muhimu zimechukuliwa katika ngazi za kikanisa na kisheria, na leo tunaitwa zaidi kujitolea kwa urejesho wa ushirika kamili.

Papa akitoa tafakari yake
Papa akitoa tafakari yake   (@Vatican Media)

Katika suala hilo,  Papa alipenda kutoa shukrani zake za  dhati kwake Yeye na Upatriaki wa Kiekuemeni kwa msaada wao unaoendelea kwa Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya Majadiliano ya Kitaalimungu  kati ya Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodox. Pia Papa anatumaini kwamba kila juhudi itafanywa ili kuhakikisha kwamba Makanisa yote ya kiorthodox yenye umbo la pekee yanarudi kushiriki kikamilifu katika juhudi hii. Kwa upande wake, katika mwendelezo wa mafundisho ya Mtaguso wa Pili wa Vatican na watangulizi wake aòipenda  kuthibitisha kwamba, huku akiheshimu tofauti halali, “kutafuta ushirika kamili kati ya wote waliobatizwa kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, ni mojawapo ya vipaumbele vya Kanisa Katoliki.” Hasa, ni mojawapo ya vipaumbele vya huduma yangu kama Askofu wa Roma, ambaye jukumu lake maalum katika Kanisa la ulimwengu wote ni kuwahudumia wote, kujenga na kulinda ushirika na umoja.” Ili kubaki waaminifu kwa hamu ya Bwana ya kutujali si tu kaka na dada zetu katika imani, bali pia wanadamu wote na uumbaji wote, Makanisa yetu lazima yaitikie pamoja misukumo ya Roho Mtakatifu leo.

Papa Leo katika Kanisa la Mtakatifu George
Papa Leo katika Kanisa la Mtakatifu George   (@Vatican Media)

Kwanza kabisa, katika wakati huu wa migogoro na vurugu zilizojaa damu katika maeneo ya karibu na mbali, Wakatoliki na Waorthodox wanaitwa kuwa wapatanishi. Hii hakika ina maana ya kuchukua hatua, kufanya maamuzi na kupitisha ishara zinazojenga amani, huku pia tukikubali kwamba amani si tu tunda la juhudi za kibinadamu, bali ni zawadi kutoka kwa Mungu. Kwa hivyo, amani lazima itafutwe kupitia sala, toba, kutafakari na kukuza uhusiano hai na Bwana, ambaye hutusaidia kutambua ni maneno gani, ishara na matendo gani ya kufanya ili tuweze kuwa wahudumu wa amani kwa dhati. Changamoto nyingine inayokabili Makanisa yetu ni janga la kiikolojia linalotishia, ambalo Patriaki wa kiekumene alisema mara nyingi linatuhitaji sisi uongofu wa kiroho, wa kibinafsi na wa kijamii kwa ajili ya kubadilisha mwelekeo na kulinda uumbaji. Wakatoliki na Waorthodox wameitwa kufanya kazi pamoja katika kukuza mawazo mapya ili kila mtu atambue jukumu la kutunza uumbaji ambao Mungu ametukabidhi.

Tafakari ya Papa
Tafakari ya Papa   (@Vatican Media)

Changamoto ya tatu ambayo akipendoa. kutaja ni matumizi ya teknolojia mpya, hasa katika uwanja wa mawasiliano. Kwa kutambua faida kubwa ambazo zinaweza kuwapa wanadamu, Wakatoliki na Waorthodoksi lazima washirikiane katika kukuza matumizi yao yenye uwajibikaji. Hakika, teknolojia hizi lazima ziwekwe katika huduma ya maendeleofungamani ya binadamu, na zipatikane kwa wote, ili kuhakikisha kwamba faida zake hazijatengwa kwa idadi ndogo ya watu au maslahi ya wachache walio na upendeleo. Katika kushughulikia changamoto hizi, Papa alisema, nina imani kwamba Wakristo wote, wajumbe wa tamaduni zingine za kidini, na wanaume na wanawake wote wenye mapenzi mema wanaweza kushirikiana kwa umoja katika kufanya kazi pamoja kwa manufaa ya wote.

Kwa kuhitimisha Papa alisema kwamba  kwa mawazo haya ya dhati,  alimpatia Patriaki na ndugu zao wote matashi mema ya afya njema na utulivu wanaposherehekea Sikukuu ya Mtakatifu wao mlinzi. Papa Leo XIV  alipenda  kutoa shukrani zake za dhati kwa makaribisho ya joto na ya kidugu waliyonipa katika siku hizi. Kwa hivyo, aliwakabidhi ypte  kwa maombezi ya Mtume Andrea na kaka yake Mtakatifu Petro, Mtakatifu George Mfiadini Mkuu ambaye Kanisa hilo limetengwa kwake, Mababa Watakatifu wa Mtaguso wa Kwanza la Nicaea na Wachungaji wengi Watakatifu wa Kanisa hilo la kale na tukufu la Constantinopli. Alimwomba Mungu, Baba wa huruma, awabariki sana wote waliokuwapo.

Papa alihitimisha kwa maneno haya Hrònia Pollà!  Ad multos annos!      

Bartholomew I: Umoja wa Kikristo, si anasa bali ni jambo la lazima

Bartholomew I pia alirudi Yerusalemu ya miaka 60 iliyopita. Katika mahubiri yake, alikumbuka kukumbatiana kati ya Paulo VI na Athenagoras kama masika ya kiroho yaliyofuata baridi ya mgawanyiko, akitafuta kushinda tofauti za zamani. Patriaki, akielezea furaha na shukrani yake kwa kumkaribisha Papa, alisisitiza vifungo vya udugu vinavyofunga Makanisa hayo mawili na vinavyoyahitaji kufanya kazi pamoja ili "kutangaza habari njema ya wokovu kwa ulimwengu." Patriaki Bartholomew kisha alisema kwamba ziara ya Papa Leo XIV , kubadilishana wajumbe wakati wa sherehe zao za ufadhili, kila Juni 29, ukumbusho wa kiliturujia wa Watakatifu Petro na Paulo, na kila Novemba 30, sherehe za Mtakatifu Andrea Mtume, ni ishara ya "dhamira thabiti na ya kina ya kibinafsi katika kutafuta umoja wa Kikristo" pamoja na usemi wa "nia ya dhati ya kurejesha ushirika kamili wa kikanisa."

Patriaki Bartholomew
Patriaki Bartholomew   (@Vatican Media)

 

Maadhimisho ya kumbukumbu ya Mtaguso wa Kwanza wa Nicaea, Patriaki anasisitiza zaidi, "hayawezi kupunguzwa kwa njia yoyote kuwa ya kupendezwa na tukio lililopita." Badala yake, yanabaki kuwa "msingi wa harakati zetu za umoja wa Kikristo leo," urithi ambao kupitia huo "Wakristo waliogawanyika watakaribia zaidi na kufikia umoja wao waliotamani kwa muda mrefu." Kwa hivyo, Patriaki Bartholomew, kama alivyokuwa amesema pia Papa Leo XIV, alitambua kazi iliyofanywa na Tume ya Pamoja ya Kimataifa ya Mazungumzo iliyoanzishwa na Papa John Paul II na Patriaki wa Kiekumeni Dimitrios mnamo Novemba 30, miaka 45 iliyopita, ambayo inaruhusu Makanisa "katika wakati huu muhimu katika historia, kushughulikia masuala magumu ya zamani, kuyashinda, na kutuongoza kuelekea urejesho wa ushirika kamili."

 Umoja wa Kikristo "si anasa," Patriaki anahitimisha, lakini ni "lazima," kwa kuwa Wakristo wanatarajiwa kutoa "ujumbe wa pamoja wa matumaini," unaolaani vita na vurugu na kutetea utu na uumbaji wa binadamu. Patriaki aliwasihi Wakristo, hawawezi kushiriki "katika umwagaji damu unaotokea Ukraine na sehemu zingine za dunia, wala kubaki kimya mbele ya kuondoka kwa Wakristo kutoka utoto wa Ukristo," lakini lazima "tutende kama wapatanishi, tujionyeshe kama wale wenye njaa na kiu ya haki, na tutende kama mawakili wazuri wa uumbaji."Baada ya Liturujia hiyo, Papa leo na Patriaki Bartholowew walitoa baraka ya pamoja nje na ndani.

Asante kwa kusoma makala haya. Ukitaka kuendelea kupata taarifa mpya, tafadhali jiandikishe kwa jarida letu: cliccando qui

30 Novemba 2025, 12:03