Tafuta

Papa:Yesu anatuita majina,anatuandalia mahali&kutuweka huru

Katika siku ambayo Mama Kanisa anawakumbuka marehemu wote,Papa Leo XIV wakati wa tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwaba katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Novemba 2 alibainisha kuwa "sauti ya Yesu ni ya wakati ujao ambayo inatuweka huru dhidi ya kutokuwa na msaada na ambayo uhatarisha kukata tamaa maishani.Sauti inayojulikana ya Yesu itufikie na iwafikie kila mtu,kwa sababu ndiyo pekee inayotoka katika wakati ujao."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mama Kanisa akiwa anaadhimisha Kumbukumbu ya Marehemu wote, Dominika tarehe 2 Novemba 2025, Baba Mtakatifu ametoa tafakari yake kabla ya sala ya  Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Papa akianza alisema wapendwa kaka na dada, Dominika njema “ Ufufuko wa Yesu kutoka katika wafu, Aliyesulibiwa, unaakisi hatima ya kila mmoja wetu katika siku hizi za mwanzoni mwa Novemba. Yeye mwenyewe alituambia: “Haya ndiyo mapenzi yake aliyenituma, kwamba nisipoteze hata mmoja wa wote alionipa, bali nimfufue siku ya mwisho” (Yh 6:39). Kwa hivyo, kiini cha wasiwasi wa Mungu ni wazi: kwamba hakuna mtu atakayepotea milele, kwamba kila mtu ana nafasi yake na anang'aa katika upekee wake.

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Hili ndilo fumbo tulilosherehekea jana (Mosi Novemba)kwenye Sherehe ya Watakatifu Wote: ushirika wa tofauti ambao, kwa kusema, unapanua maisha ya Mungu kwa binti na wana wote ambao wametamani kuwa sehemu yake. Ni hamu iliyoandikwa moyoni mwa kila mwanadamu, ambayo inahitaji utambuzi, umakini, na furaha. Kama Papa Benedikto XVI alivyoandika, usemi "uzima wa milele" unatafuta kutoa jina kwa matarajio haya yasiyozuilika: sio mfululizo usio na mwisho, bali kuzamishwa katika bahari ya upendo usio na mwisho, ambapo wakati, kabla, na baada ya hapo hazipo tena. Ukamilifu wa maisha na furaha: hivi ndivyo tunavyotumaini na kutarajia ya kuwa kwetu na Kristo (taz. Spe Salvi, 12).

Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Kwa hivyo, Ukumbusho wa Waamini Wote Marehemu unatuletea fumbo karibu zaidi. Papa alisema kuwa, “Hakika, tunapata wasiwasi wa Mungu wa kutopoteza mtu yeyote kila wakati kifo kinapoonekana kutufanya tupoteze milele sauti, uso, na ulimwengu mzima. Kiukweli, kila mtu ni ulimwengu mzima. Kwa hivyo, leo, ni siku inayopinga kumbukumbu ya mwanadamu, yenye thamani na dhaifu sana. Bila kumbukumbu ya Yesuya maisha yake, kifo, na ufufuko, hazina kubwa ya kila maisha imefichuliwa. Hata hivyo, katika kumbukumbu iliyo hai ya Yesu, hata wale ambao hakuna anayewakumbuka, hata wale ambao historia inaonekana kuwa imewafuta, wanaonekana katika hadhi yao isiyo na kikomo. Yesu, jiwe lililokataliwa na waashi sasa ndiye jiwe kuu la pembeni (rej. Mdo 4:11). Hili ni tangazo la Pasaka. Kwa sababu hiyo, Papa Leo alisisitiza, Wakristo wamekuwa wakiwakumbuka marehemu katika kila Ekaristi, na hadi leo wanaomba wapendwa wao watajwe katika Sala ya Ekaristi. Kutokana na tangazo hilo kunaibuka tumaini kwamba hakuna mtu atakayepotea.

Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alisema kwamba “Ziara ya makaburi, ambapo ukimya hukatiza msisimko wa shughuli, iwe kwetu sote mwaliko wa kukumbuka na kusubiri. "Ninasubiri ufufuko wa wafu na uzima wa ulimwengu ujao," tunasema katika kanuni ya Imani. Kwa hivyo, tukumbuke wakati ujao. Hatujafungwa katika yaliyopita, katika machozi ya kumbukumbu za zamani. Wala hatujafungwa katika wakati uliopo, kama kaburini. Sauti inayojulikana ya Yesu itufikie, na iwafikie kila mtu, kwa sababu ndiyo pekee inayotoka katika wakati ujao. Anatuita kwa majina, anatuandalia mahali, anatuweka huru kutokana na hisia ya kutokuwa na msaada ambayo inatufanya tuhatarishe kukata tamaa maishani. Mariamu, mwanamke wa Jumamosi Takatifu, atufundishe tena kutumaini,” Papa alibainisha.

TAFAKARI ANGELUS YA PAPA
02 Novemba 2025, 14:13