Tafuta

Papa Leo XIV: US-Venezuela,hakuna suluhisho linalopatikana kupitia vurugu

Papa Leo XIV, aliyekuwa huko Castel Gandolfo,tangu Jumatatu usiku,wakati akitoka alijibu maswali ya waandishi wa habari kuhusu mazungumzo ya Marekani na Venezuela "kufanya kazi pamoja kwa ajili ya haki kwa watu wote"katika Mashariki ya Kati.Kisha alisisitiza kwamba ni "haki ya binadamu kuwa na kazi yenye heshima."

Vatican News.

"Mazungumzo" kati ya Marekani na Venezuela, "haki kwa watu wote" Mashariki ya Kati, wito wa kuheshimiwa kwa "haki za kiroho" za wahamiaji waliokamatwa Marekani, na wasiwasi kuhusu vifo mahali pa kazi. Haya yalikuwa maneno ya Papa Leo XIV nje ya makazi yake huko Castel Gandolfo, akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari waliokuwa wakimsubiri jioni ya tarehe 4 Novemba 2025 nje ya Villa Barberini. Akitoka langoni karibu saa 2:30 usiku, baada ya salamu fupi kwa watu waliokuwa barabarani, Papa alisimama mbele ya Mic na Camera na, kwanza kabisa, akakumbuka Siku ya Jeshi, ambayo iliadhimishwa tarehe 4 Novemba nchini Italia, Papa aliwatakia "Matashi mema! Nchi ina haki ya kuwa na jeshi lake kulinda amani, kujenga amani."

Kwa mtazamo huo, Papa alionesha wasiwasi wa "mvutano" wa siku za hivi karibuni nje ya pwani ya Venezuela, kati ya mapambano dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kupelekwa kwa Wanamaji wa Marekani katika Caribbien, huku tishio la "vita baridi" likiwa limefichwa. "Nadhani hatushindi kwa vurugu," Papa alisema, akielezea kwamba dakika chache mapema alikuwa amesoma ripoti ya habari kuhusu meli za kivita zinazokaribia pwani ya Venezuela. "Jambo la msingi ni kutafuta mazungumzo, ili kupata njia sahihi ya kupata suluhisho za matatizo ambayo yanaweza kuwepo katika baadhi ya nchi."

Amani Mashariki ya Kati

Kisha mwelekeo unaelekea Mashariki ya Kati, huku makubaliano ya amani yakitishiwa na mashambulizi mapya ya Israeli dhidi ya Gaza, pamoja na uchochezi kutoka kwa walowezi kwenye Mlima wa Hekalu na shambulio dhidi ya vijiji kadhaa katika Ukingo wa Magharibi. Mkataba huo "ni dhaifu sana," anasema Leo XIV, akitoa maoni chanya, hata hivyo, kwamba "angalau awamu ya kwanza ya makubaliano ya amani (yaliyosainiwa Oktoba 10) bado yanaendelea." Sasa, hata hivyo, Papa anasisitiza, "lazima tutafute jinsi ya kuhamia awamu ya pili, kushughulikia suala la utawala, jinsi ya kuhakikisha haki za watu wote." "Suala la Ukingo wa Magharibi, la walowezi, ni gumu kweli: Israeli ilisema jambo moja, kisha wakati mwingine hufanya lingine," anasisitiza. Haja ni "kujaribu kufanya kazi pamoja kwa ajili ya haki kwa watu wote."

Kuheshimu Mahitaji ya Kiroho ya Wahamiaji Marekani

Papa Leo pia aliuliza kuhusu Chicago, mji wake wa nyumbani, ambapo mamlaka yamepiga marufuku makuhani Wakatoliki kutoa Komunyo kwa wahamiaji waliofungwa. Kwanza, Papa alikumbuka kwamba "jukumu la Kanisa ni kuhubiri Injili." Alikumbuka Injili ya Mathayo, sura ya 25, "ambapo Yesu anasema waziwazi: mwishoni mwa dunia tutaulizwa: ulimkaribishaje mgeni? Ulimkaribisha na kumkaribisha au la?" Papa alisema "Nadhani kuna tafakari kubwa ya kufanywa kuhusu kinachoendelea." Aidha alibainisha kuwa "Watu wengi ambao wameishi kwa miaka mingi bila kusababisha matatizo wameathiriwa sana na kinachoendelea hivi sasa."

Kwa hivyo mwaliko ni kuzingatia pia haki za kiroho za wafungwa: "Hakika ningewasihi mamlaka kuwaruhusu wafanyakazi wa kichungaji kushughulikia mahitaji ya watu hawa. Mara nyingi wamekuwa wakitenganishwa na familia zao kwa muda mrefu; hakuna anayejua kinachoendelea... lakini mahitaji yao ya kiroho yanapaswa kuheshimiwa."

Kazi, haki ya binadamu

Mahojiano mafupi na waandishi wa habari pia yalijumuisha maoni kuhusu mada ya kazi, kwa kuzingatia Jubilei ijayo ya Ulimwengu wa Kazi na kwa kuzingatia visa vingi vya vifo vya ajali kazini, nchini Italia na kwingineko, hasa mfanyakazi mwenye umri wa miaka 66 ambaye alipoteza maisha yake katika kuanguka kwa Torre dei Conti huko Roma.

"Sauti ya Kanisa ni ya haki. Tunaamini kweli kwamba sote lazima tufanye kazi pamoja. Ni haki ya binadamu kuwa na kazi yenye heshima, ambapo mtu anaweza pia kupata pesa kwa faida ya familia yake," Papa alijibu akisisitiza wasiwasi wake kuhusu usalama na kusema kwamba sherehe ya Jubilei pia inalenga "kutoa matumaini kidogo na kujaribu kuunganisha nguvu ili kupata suluhisho na sio kutoa maoni tu kuhusu matatizo."

Kesi ya Rupnik

Hatimaye, kabla ya kuondoka na kurudi Vatican, swali la mwisho kuhusu aliyekuwa Mjesuit Marko Ivan Rupnik, anayetuhumiwa kwa nynyaso na watawa kadhaa, ambako kesi yao iko katikati ya mchakato mbele ya Baraza la Kipapa la Mafundisho Tanzu ya Kanisa. Papa aliulizwa kuhusu kazi za sanaa za Rupnik, msanii mashuhuri na mpiga picha za kimosaic, ambazo bado zimetawanyika katika sehemu mbalimbali takatifu, ambazo baadhi yake zimefunikwa kufuatia maombi na maandamano kutoka kwa waathiriwa.

Yaya alijibu kuwa, "Hakika, katika sehemu nyingi, hasa kutokana na hitaji la kuwa makini na wale ambao wameripoti kuwa waathiriwa, kazi za sanaa zimefunikwa, kazi za sanaa zimeondolewa kwenye maeneo kadhaa Kwa hivyo suala hili hakika ni jambo tunalolijua."  Papa  Leo XIV, kisha alielezea kwamba "kesi mpya imeanza hivi karibuni" dhidi ya Mjesuit wa zamani: "Majaji wameteuliwa, na michakato ya kimahakama inachukua muda mrefu. Ninajua ni vigumu sana kwa waathiriwa kuwaomba wawe na subira. Lakini Kanisa lazima liheshimu haki za watu wote. Kanuni ya dhana ya kutokuwa na hatia hadi ithibitishwe kuwa na hatia pia inatumika katika Kanisa. Na tunatumai kwamba kesi hii mpya iliyoanzishwa italeta uwazi na haki kwa wote wanaohusika."

Masawali ya waandishi

Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida:cliccando qui.

05 Novemba 2025, 10:10