Tafuta

Uwanja wa Mtakatifu Petro kuutazama kwa juu. Uwanja wa Mtakatifu Petro kuutazama kwa juu.  (@Vatican Media)

Vatican yachapisha Kanuni za Curia Romana

Papa Leo XIV aidhinisha kuchapishwa kwa Kanuni mpya za Curia Romana,ambazo zinatekeleza mageuzi yaliyowekwa na Katiba ya Kitume ya "Praedicate Evangelium."

Vatican News

Kanuni za Curia Romana na Kanuni za Wafanyakazi wa taasisi hiyo hiyo zimechapishwa Jumatatu, tarehe 24 Novemba 2025. Zilisainiwa Dominika tarehe 23 Novemba 2025  na Baba Mtakatifu Leo XIV, katika Sherehe ya Bwana Wetu Yesu Kristo, Mfalme wa Ulimwengu.  Kanuni za Curia Roma zinatumika katika Taasisi na Ofisi zinazounda Curia Romana, yaani Sekretarieti ya Vatican, Mabaraza ya Kipapa, Mihimili ya Mahakama na Mihili ya Uchumi.

Kanuni za Wafanyakazi zinahusu kanuni za kitabia za taasisi hiyo, nidhamu, na kiuchumi zinazohusiana na uhusiano wa ajira ya wafanyakazi wanaohudumu katika Sekretarieti ya Vatican, Mabaraza ya Kipapa, Mashirika na Ofisi zinazounda Curia Romana pamoja na Taasisi zinazohusiana na Kiti Kitakatifu. Kanuni hizi mpya zinachukua nafasi ya zile zilizoidhinishwa na Papa Mtakatifu Yohane Paulo II mnamo tarehe 15 Aprili 1999, ambazo zilianza kutumika tarehe 1 Julai mwaka huo huo. Zinajumuisha na kutekeleza marekebisho, uvumbuzi, na ishara zilizoletwa na Hayati Papa Francisko na Katiba ya Kitume ya Praedicate Evanglium yaani Hubirini Injili ya tarehe 19 Machi 2022.

Kwa maelezo zaidi unaweza kusoma maandishi kwa lugha yakitaliano bonye hapa:GENERAL REGULATION OF THE PERSONNEL OF THE ROMAN CURIA

KANUNI ZA CURIA ROMANA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku: Just click here

24 Novemba 2025, 16:23