Ziara ya Papa Leo XIV,kufika Ancara,Turkiye:Ni ziara ya I Kimataifa
Vatican News
Ziara yake ya kwanza ya kitume ya Papa Leo XIV imeanza, Alhamisi 27 Novemba 2025 ikimpeleka kwanza Uturuki (Türkiye), na ambapo atasimama Iznik, katika fursa ya maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Kwanza wa Nicea. Ziara yake ya pili itakuwa Lebanon, kuanzia Dominika 30 Novemba 2025.
![]()
Papa ndani ya ndege, Picha ya Maria, Mama wa Shauri jema ikimsindikiza
Katika Ndege ya ITA Airways iliyomchukua Papa Leo, na msafara wake, na waandishi wa habari wengi, iliondoka saa 1:58 asubuhi masaa ya Ulaya kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Fiumicino. Imepangwa kuwasili Ankara, Turkiye(Uturuki,) saa 6:30 mchana, ambapo ataondoka jioni hiyo kuelekea Istanbul. Pia ndani ya ndege ya Papa kuna Picha ya Maria, Mama wa Shauri Jema iliyohifadhiwa katika Madhabahu ya Genazzano , madhabahi inayohudumiwa na Watawa wa Shirika la Mtakatifu Agostino.
Mnamo tarehe 10 Mei 2025, siku chache baada ya kuchaguliwa kwake, Papa Leo XIV alifanya ziara ya ghafla kwenye Madhabahu hiyo mbali kidogo na Roma. Baada ya kusali mbele ya picha ya Bikira, akiwasalimia wenzake, alisema kwamba ilikuwa ni hamu yake kuwa hapo wakati wa siku za kwanza za huduma mpya "ambayo Kanisa," aliongeza, "limenikabidhi, kuendeleza utume kama Mrithi wa Petro."
![]()
Leo XIV akiwa ndani ya ndege kwa ziara yake ya kwanza ya kitume, kituo cha kwanza Uturuki
Papa aliondoka Vatican yapata saa 1:00 asubuhi majira ya Ulaya na kusafiri kwa kuelekea Uwanja wa Kimataifa wa Ndege huko Fiumicino Roma. Papa Leo XIV anakuwa Papa wa tano kutembelea Turkiye(Uturuki,) na kauli mbiu ya Ziara yake nchini humo ni "Bwana Mmoja, Imani Moja, Ubatizo Mmoja."
Papa anatimiza hamu ya Hayati Papa Francisko ya kwenda Uturuki aliyokuwa akitarajia mnamo Mei 2025, kufuatia ziara yake ya 2014, kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicea.
Kivutio kitakuwa Iznik, katika uchimbaji wa akiolojia wa Basilika ya kale ya Mtakatifu Neophytos, ambapo Papa, pamoja na Patriaki wa Constantinople Bartholomew I, watasali na mapatriaki wapatao ishirini na wawakilishi wa makanisa ya Kikristo mbele ya sanamu za Kristo na Baraza zima.
Telegram kwenda Italia
Wakati wa safari ya ndege, Papa alituma telegram kwa Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, ambapo alisisitiza kwamba safari yake ilikuwa "kukutana na watu hao, hasa kaka na dada katika imani, kwa kuhimiza njia za amani na udugu." Papa Leo XIV anatoa salamu na matashi mema ya dhati kwa maendeleo ya kiroho, kiraia, na kijamii ya nchi hiyo ya Italia.
Kwa upande wake, mkuu wa nchi ya Italia alitoa shukrani zake, akituma ujumbe ambapo alisisitiza kwamba mikutano ijayo ya Papa "inaamsha hisia za matumaini na imani kwa wale wote wanaoshiriki kujitolea kwa heshima ya utu wa binadamu na haki ya msingi ya uhuru wa kidini. Katika misingi hii ya umoja wa mataifa na mazungumzo kati ya imani, matarajio ya kuishi pamoja kwa amani miongoni mwa watu pia yanapata msingi imara."
Rais Mattarella alielezea imani yake kwamba uwepo wa Papa Leo "utawafariji wanawake na wanaume wenye mapenzi mema wanaokataa vurugu na ukandamizaji, wakifanya kazi kila siku kunyamazisha silaha na kuhakikisha kwamba mazungumzo na kutafuta manufaa ya wote vinashinda." "Ni wakati wa kutamani amani na utulivu, unaoshirikishwa na watu wote, kutafsiriwa," Rais wa Jamhuri aliandika, "kuwa mipango thabiti. Uwepo wake nchini Uturuki na Lebanon bila shaka utaimarisha tena sababu ya umoja na undugu wa kibinadamu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku:Just click here
