Tafuta

2025.12.01 Ziara ya Kitume nchini Lebanon-Mkutano wa Kiekumeni na Kidini katika Uwanja wa Mashahidi, Beirut. 2025.12.01 Ziara ya Kitume nchini Lebanon-Mkutano wa Kiekumeni na Kidini katika Uwanja wa Mashahidi, Beirut.  (@Vatican Media)

Mkutano wa Viongozi wa Kidini:Nchi ya Mierezi ni daraja kati ya Mashariki na Magharibi

Katika hema lililowekwa katika Uwanja wa Mashahidi huko Beirut kwa ajili ya mkutano wa kiekumeni na kidini na Papa Leo XIV,wawakilishi Wakristo na Waislamu walibadilishana mawazo wakisisitiza hitaji la kuimarishwa kwa umoja wa kitaifa nchini Lebanoni.Nchi ya Mierezi ni taifa la kuishi pamoja na wingi wa kidini,ambalo huimarisha maisha ya kila siku..Vita bandia kwa kutumia dini havioneshi ukweli wa dini ambao umejengwa juu ya utakatifu wa mwanadamu.

Tiziana Campis na Angella Rwezaula - Vatican.

Katika mkutano wa kiekumeni na kidini na Papa katika Uwanja wa Mashahidi wa Beirut, ishara ya upinzani wa Lebanon wakati wa uasi dhidi ya Waturuki wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia na mojawapo ya maeneo makuu ya maandamano ya kupinga serikali mwaka wa 2019, Patriaki Mkatoliki wa Syria, Ignatius Youssif III Younan, alimkaribisha Papa. Alionesha matumaini, kwanza kabisa, "kwamba ziara yake inaweza kusaidia kuanzisha amani na utulivu" nchini Lebanon na nchi zingine za Mashariki ya Karibu, na akakumbuka kwamba "inaambatana na matukio mawili ya kihistoria": maadhimisho ya miaka 1700 ya Mtaguso wa Nicaea, ambapo Makanisa ya Lebanon "yaliandaa mikutano ya kiekumeni," na maadhimisho ya miaka 60 ya Nostra aetate  na mwaliko wake wa mazungumzo ya kidini.

Mkutano wa kiekumeni na kidini
Mkutano wa kiekumeni na kidini   (@Vatican Media)

"Watu wetu, zaidi ya yote, wanatamani utulivu wa kisiasa, amani yenye kujenga, na udugu halisi wa kibinadamu miongoni mwa raia wote," alisema Patriaki wa Syria, akiwa na uhakika kwamba uwepo wa Papa Leo "utatutia moyo kuimarisha" kujitolea kwetu kuishi pamoja katika roho ya mazungumzo ya dhati kati ya dini, tukisema ukweli kwa upendo na heshima ya pande zote, kwa uaminifu kwa mizizi yetu. Kwa hivyo kujitolea "kutembea pamoja," "kuongozwa na matumaini," na "kuwa wajenzi wa amani halisi nchini Lebanon na katika nchi zote za Mashariki ya Kati."

"Heri wapatanishi"

Salamu ya Patriaki wa Kikatoliki wa Syria ilifuatiwa na nyimbo kutoka Injili na Quran, ikifuatiwa na onesho la makala yenye kichwa "Heri wapatanishi," ikionesha mipango, uzoefu, na historia za maisha zinazoonesha jinsi kuishi kwa pamoja kwa dini tofauti, kama ile iliyopatikana Lebanon, "ni uzoefu mzuri kwa wanadamu wote." Video hiyo ilielezea matumaini kwamba, baada ya migogoro kadhaa, nchi inaweza kufikia "utakaso kamili wa kumbukumbu, uponyaji wa kumbukumbu ya Lebanon kutokana na vita." Matumaini ni kwamba ziara ya Papa Leo "itakuwa chachu ya kweli kwa safari hii ya kujenga mustakabali thabiti."

Video hiyo ilionesha mfululizo wa watu wanaosimulia maisha yao ya kila siku, hawa wakiwa Wakristo na Waislamu wanaoishi pamoja na wanaota mazungumzo mapana na kuishi pamoja kwa amani zaidi. Miongoni mwa mipango inayolenga kuboresha kuishi pamoja, mpango wa elimu ya uraia hai unaokumbatia utofauti shuleni pia ulioneshwa.

Il Papa tra i leader religiosi

Papa Leo VI kati ya Viongozi wa kidini (@Vatican Media)

Kueneza ujumbe wa Hati kuhusu Udugu wa Kibinadamu

Viongozi nane wa kidini  baadaye walizungumza kwa zamu. Kutoka kwa Patriaki wa Kiorthodox wa Ugiriki ya Antiokia, Yohanna X Yazigi, ambaye alifuatilia kwa ufupi historia ya Kikristo ya Lebanon na majimbo jirani, alisema kuwa Papa alikaribishwa  katika taifa "linalopumua kwa mapafu yake mawili, Kiislamu na Kikristo," "nchi ya kuishi pamoja," "ambapo vipengele hivyo vinakamilishana na kufanana, kiukweli, vinaungana kuunda Lebanon." Wakati huo huo, Sheikh Abdullatif Darian, Mufti wa Jamhuri ya Lebanon na kiongozi wa Sunni, alisisitiza kwamba Nchi ya Mierezi ni taifa "la kuishi pamoja na la wingi na utofauti wa maungamo," na kwamba Muhammad, katika Quran, aliandika kwamba Mungu aliagiza "kutekeleza dini na kutogawanya umoja wake."

Mwakilishi huyo wa Sunni kisha alikumbuka makaribisho ambayo Waislamu walipokea kutoka kwa Negus, mfalme Mkristo wa Abyssinia, na Mkataba wa Medina, ambao, kwa msingi wa dola ya kwanza ya Kiislamu, "ulianzisha kwamba waamini Wayahudi na Wakristo, pamoja na Waislamu, walikuwa taifa moja." Kiongozi huyo alitaka Hati ya 'Udugu wa Kibinadamu  (Documento sulla Fratellanza Umana, ) ulitoatiwa saini mnamo 2019  na Imam Mkuu wa  Al-Azhar, Aḥmad al-Ṭayyib, na Papa Francisko akikisitiza ujumbe wake. "Tunajiona kuwa tumepewa jukumu la pamoja, kidini, kimaadili na kama taifa, kubeba nuru ya ujumbe huu, ili usalama na amani viweze kutawala duniani na upendo uweze kutawala miongoni mwa mataifa na watu wote," alihitimisha.

Lo sceicco Abdullatif Darian, mufti della Repubblica del Libano, leader sunnita

Sheikh Abdullatif Darian, Mufti wa Jamhuri ya Lebanon na kiongozi wa Sunni(@Vatican Media)

Nchi ya Mierezi: Daraja Kati ya Mashariki na Magharibi

Akizungumza kwa upole, Patriaki  Aram I, anayewakilisha Waorthodox wa Armenia katika hafla hiyo katika Uwanja wa Mashahidi, alisisitiza utajiri unaotokana na kukutana kwa utofauti katika Nchi ya Mierezi. Alibainisha kuwa utofauti hujidhihirisha katika umoja, ambao huhifadhi na kuimarisha utofauti huu katika huduma ya Lebanon iliyoungana, huru, na huru. Kwa kiongozi wa Waorthodox wa Armenia, ndani ya taifa, "umoja wa Kiislamu-Kikristo ndio msingi," "kipengele tofauti," cha upekee wake, na kwa upande mwingine, umoja katika utofauti na roho ya kuishi pamoja" vinavyoitofautisha huifanya kuwa "daraja kati ya Mashariki na Magharibi." Changamoto inayowakabili watu wa Lebanon ni kudumisha utofauti wao "na kudumisha umoja imara wa Kiislamu-Kikristo, huku wakati huo huo wakiimarisha na kuelezea kwa uthabiti" umoja wa kitaifa.

Il Catholicos Aram I, leader armeno-ortodosso

Patriaki Aram I, Kiongozi wa Waarmenia Waorthodox (@Vatican Media)

Dunia na iisaidie Lebanon kujikomboa kutokana na migogoro iliyokusanyika.

Makamu wa rais wa Baraza la Juu la Kiislamu la Washia, Sheikh Ali El-Khatib, anatumaini kwamba kukaa kwa Papa kutasababisha "kuimarika kwa umoja wa kitaifa unaoyumba katika nchi hii, unaokumbwa na uchokozi unaoendelea wa Israeli dhidi ya watu wake na ardhi yake." "Utamaduni wetu wa kiroho umejengwa juu ya udugu wa kibinadamu," aliongeza, akielezea kwamba mrithi wa Muhammad, Imam Ali ibn Ab Ṭalib, alisema kuhusu asili ya uhusiano kati ya wanadamu kwamba wanadamu wanapaswa kuchukuliwa kuwa "ndugu katika imani" au "sawa katika uumbaji." Kiongozi wa Washia pia alibainisha kwamba Uislamu unaona utofauti kuwa sehemu ya asili ya mwanadamu, na alifundisha "kwamba uhusiano kati ya watu tofauti unatawaliwa na mazungumzo, uelewa wa pande zote, na kutokana na ushirikiano katika wema na uchamungu; na kwamba kuishi kwa amani kati ya wafuasi wa dini tofauti ndiyo kanuni na msingi, na kwamba "kinachotokea kwa vita bandia kwa jina la dini" hakioneshi "ukweli wa dini, ambao msingi wake ni utakatifu na hadhi ya mwanadamu." Kwa njia hiyo alisisitiza kuwa "Tuweke suala la Lebanon mikononi mwake," anahitimisha Sheikh Ali El-Khatib, akihutubia Papa Leo, akitumai kwamba "ulimwengu unaweza kusaidia" nchi kujikomboa kutokana na migogoro iliyokusanyika.

La struttura che ha ospitato l'incontro ecumenico e interreligioso

Muundo uliokaribisha Mkutano wa kiekumeni na kidini(@Vatican Media)

Tumaini la Amani Inayotegemea Haki

Kwa Patriaki wa Antiokia na Mashariki Yote na Mkuu Mkuu wa Kanisa la Kiorthodox la kisyria duniani kote, Mar Ignatius Ephraim II, kwa upande wake, hakuficha ukweli kwamba katika miaka ya hivi karibuni, katika nchi za Mashariki ya Kati, "Waislamu na Wakristo wamekuwa wahanga" wa kampeni za kigaidi na vita ambavyo vimesababisha uhamiaji wa kulazimishwa, "changamoto" ambazo "zimeimarisha ushirikiano kati ya Makanisa tofauti" na kusababisha kile ambacho Papa Francisko amekiita "uekumeni wa damu."

Akiwakilisha hisia za kawaida za watu, Patriaki wa Kiorthodox wa Syria alibainisha kwamba kila mtu anatumaini "utulivu, haki, na amani, amani inayotegemea haki, ambayo inalinda utu na uhuru wa binadamu, katika nchi inayotawaliwa na sheria na inayotegemea usawa katika haki na wajibu." Aliona kwamba Wakristo na Waislamu wameishi pamoja Lebanon kwa karne nyingi na wanashiriki "huzuni na matumaini" na hamu "ya kuendelea kuishi pamoja." Na ingawa mazungumzo ya kitaaluma kati ya wawakilishi wa dini ni muhimu, uzoefu unaopatikana katika maisha halisi unabaki kuwa jambo muhimu zaidi katika kuimarisha."

Mar Ignatius Ephraim II anaongeza kwamba huko Lebanon Wakristo na Waislamu wamejifunza kwamba kuishi pamoja kimsingi ni "mazungumzo ya maisha yanayotegemea kukutana kwa dhati na kuheshimiana” na kwamba “mkutano kati ya watoto wa dini tofauti unaweza kujenga jamii yenye mshikamano inayoweza kukabiliana na ushabiki na mgawanyiko, na matumaini yenye kutia moyo.” Katika Taifa la  Mwerezi “Kanisa la Lebanon na Mashariki linabaki kuwa shahidi wa dhamiri ya binadamu, likitaka mazungumzo ya wazi, heshima kwa uhuru wa kidini, na ulinzi wa hadhi ya kila mtu,” Patriaki alihitimisha, akiwa na uhakika kwamba Papa atabeba moyoni mwake “mateso ya Mashariki hii inayoteswa” na atafanya kazi “ili kuyapunguza, na kuhakikisha maisha huru na yenye heshima kwa watoto wake wote.”

Il Papa e il patriarca di Antiochia e di tutto l’Oriente e capo supremo della Chiesa Siro-Ortodossa nel mondo Mar Ignazio Efraim II

Papa na Patriki wa Antiokia Mar Ignazio Efraim II  (@Vatican Media)

Kufungua Milango ya Upendo na huruma

Katika hotuba yake, Sheikh Al-Aql wa jumuiya ya Druze, Sami Abi Al-Muna, alielekeza Lebanon kama mfano wa utofauti katika umoja. "Tunaamini kwamba taifa letu lazima lijengwe tu juu ya misingi imara na thabiti ya maadili, ambayo inahitaji kila familia ya kiroho kumlinda mwenzake katika nchi yake," kiongozi huyo wa Druze anasisitiza, akiamini kwamba mkutano wa leo kati ya Wakristo na Waislamu unaweza "kuunda mwanga wa matumaini katika hali ya sasa ya giza." Na kwamba Papa anamwalika kila mtu "kufungua milango ya upendo na huruma ," ya upendo wa Kikristo na rehema ya Kiislamu, ili sauti ya amani iwe na nguvu kuliko sauti ya vita.

Il Papa e il cardinale Béchara Boutros Raï, patriarca di Antiochia dei Maroniti

Papa na Kardinali Béchara Boutros Raï, Patriaki wa  Antiokia ya Maroniti   (@Vatican Media)

Umuhimu wa Sinodi

Kwa niaba ya Makanisa ya Kiprotestanti ya Lebanon, Joseph Kassab, Rais wa Baraza Kuu la Jumuiya ya Kiinjili nchini Syria na Lebanon, alizungumza. Alilenga sinodi iliyohamaishwa katika miaka ya hivi karibuni na Kanisa Katoliki, "safari ya kufanywa pamoja, kusikilizana na kugundua sauti ya Roho katika utofauti," ambayo si "suala la kikanisa" tu bali "wito ambao Lebanon yote inaweza kukumbatia." "Ikiwa viongozi wa Lebanon wangetembea pamoja... ikiwa wangesikilizana kwa dhati, ingekuwa rahisi kwetu kuelewa mateso ya watu wetu," alisema, akiongeza kwamba tunaweza kugundua "kwamba njia ya amani si ndoto ngumu, bali ni utaratibu wa kila siku unaoanza na uaminifu." Kwa hivyo matumaini kwamba ziara ya Papa inaweza kuwa "fursa ya kualika jumuiya zote za Lebanon kwenye sinodi ya kitaifa, kutembea pamoja kwa ajili ya Lebanon.

Il Papa all'arrivo fra i leader religiosi

Wakati wa kufika kwa Papa kati kati ya viongozi wakidini (@Vatican Media)

Kuweka maslahi ya taifa juu ya yote

Hatimaye, Sheikh Ali Kaddour, kiongozi wa Alawite, akizungumza kwa niaba ya Baraza la Kiislamu la Alawite, alielezea uwepo wa Papa  Leo XIV nchini Lebanon kama "msaada kwa kila sauti inayoita udugu, ulinzi wa utu wa binadamu, na kushinda majeraha na migawanyiko ambayo yameilemea" nchi na watu wake. "Sote tunaamini kwamba mwanadamu ndiye thamani kuu, kwamba nchi za nyumbani hujengwa kupitia kukutana na si migogoro, kupitia ushiriki na si kutengwa, kupitia heshima ya pande zote na si migogoro," aliendelea, akielezea nia ya Alawite ya kuunga mkono "kila mpango unaoimarisha utulivu, hufufua matumaini mioyoni, huwahimiza watu wa Lebanon kuzungumza na kuelewana, na huweka maslahi ya taifa juu ya mambo mengine yote."

Mkutano wa kiekumeni na kidini

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

01 Desemba 2025, 19:02