Papa amemteua Askofu Ronald Hicks kuwa Askofu Mkuu wa New York,Marekani
Na Angella Rwezaula- Vatican
Jimbo Kuu la New York, nchini Marekani lina mchungaji mpya Askofu Mkuu Ronald A. Hicks, ambaye alikuwa kwa sasa ni Askofu wa Jimbo la Joliet huko Illinois (Marekani). Papa alimteua tarehe 18 Desemba 2025, baada ya kukubali barua ya maombi kuacha shughuli za kichungaji za jimbo kuu la jiji lililowasilishwa na Kardinali Timothy M. Dolan.
Askofu Mkuu Mteule alizaliwa tarehe 4 Agosti 1967, huko Chicago, Hicks alihudhuria Mafunzo ya Seminari ya Chuo cha Niles, akipata Shahada ya Falsafa kutoka Chuo Kikuu cha Loyola huko Chicago. Alikamilisha masomo yake ya kikanisa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Maria wa Ziwa na Seminari ya Mundelein huko Mundelein, Illinois. Baadaye alipata Shahada ya Uzamivu wa Huduma kutoka chuo kikuu hicho hicho.
Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 21 Mei 1994, kwa ajili ya Jimbo Kuu la Chicago, ambapo alishikilia nyadhifa mbalimbali kama vile: Padre wa parokia ya Mama Yetu wa Huruma huko Chicago (1994–1996) na Mtakatifu Elizabeth Seton huko Orland Hills (1996–1999); mkuu wa malezi katika Seminari ya Chuo cha Mtakatifu Joseph (1999–2005); na huko Mexico na El Salvador kuanzia (2005–2009 alikuwa mkurugenzi wa kikanda wa Shirika la Upendo la (Nuestros Pequeños Hermanos ),kwa maana halisi, “kaka na dada zetu wadogo”, ni Shirika la Upendo ambalo litoa makazi kwa maelfu ya yatima na watoto waliotelekezwa tangu 1954. Kwa sasa kuna nyumba za NPH katika nchi tisa za Amerika Kusini; mjumbe wa kitivo na kisha mkuu wa malezi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Maria wa Ziwa na Seminari ya Mundelein huko Mundelein (2010–2014); na Mkuu wa Shirika (2015–2020). Aliteuliwa kuwa Askofu na msaidizi wa Chicago mnamo tarehe 3 Julai 2018, na akapewa darala la kiaskofu mnamo Septemba 17. Mnamo tarehe 17 Julai 17, 2020, aliteuliwa kuwa Askofu wa la Jimbo la Joliet huko Illinois.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku, bofya hapa tu:Just click here
