Tafuta

Askofu Mkuu mpya Moth wa Jimbo Kuu la Westminster, Uinhereza. Askofu Mkuu mpya Moth wa Jimbo Kuu la Westminster, Uinhereza.  (AFP or licensors)

Papa Leo amteua Askofu Mkuu Mpya wa Westminster,Uingereza

Askofu Charles Phillip Richard Moth, ambaye kwa sasa ni Askofu wa Arundel na Brighton nchini Uingereza, akimrithi Kardinali Vincent Nichols.

Na Angella Rwezaula- Vatican.

 

Baba Mtakatifu  Leo XIV  tarehe 19 Desemba 2025 amemteua Askofu Mkuu mpya wa Westminster, nchini Uingereza. Charles Phillip Richard Moth ambaye hadi uteuzi huo alikuwa  ni Askofu wa Arundel na Brighton, Jimbo linalogawanyika kati ya Southwark, akimrithi Kardinali Vincent Gerard Nichols, aliyekuwa Askofu Mkuu Katoliki la Westminster tangu 2009, ambaye amewasilisha barua za kung’atuka  kwake uchungaji wa Jimbo hilo.

Alizaliwa  Julai 1958, huko Chingola, Zambia, Askofu mkuu mpya na kukamilisha elimu yake ya msingi na sekondari katika shule za Kikatoliki huko Kent. Alipata malezi yake ya kipadre katika Seminari ya Mtakatifu Yohane huko Wonersh, Surrey, na katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Paul huko Ottawa, ambapo alipata Leseni ya Sheria ya Kanisa. Alipewa daraja la Upadre  tarehe 3 Julai 1982 kwa ajili ya Jimbo Kuu la Southwark. Ameshikilia nafasi zifuatazo: Padre  msaidizi wa parokia; Jaji wa Mahakama ya Jiji la Southwark; Padre Msimamizi  wa Jeshi la Matibabu la Kennington; katibu binafsi wa Askofu mkuu; mkuu wa maadhimisho ya kiliturujia; mkurugenzi wa Ofisi ya Miito na makamu mkuu; na rais wa Mahakama ya Jiji la Southwark.

Mnamo 2001, aliteuliwa kuwa Padre wa Jimbo Kuu la Southwark na Askofu wa Heshima; mnamo 2003, aliteuliwa kuwa Msimamizi wa Parokia ya Msalaba Mtakatifu, Plumsteas; na mnamo 2006, Msimamizi wa Parokia ya Mtakatifu Joseph, Maria, Cray. Mnamo tarehe 25 Julai 2009, alichaguliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jeshi la Uingereza, akipokea wakfu wa kiaskofu mnamo  tarehe 29 Septemba mwaka huo. Mnamo Machi 21, 2015, alihamishiwa kwenye Kiti cha Arundel na Brighton hadi utuezi huu.

 Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku, bofya hapa tu:Just click here

19 Desemba 2025, 17:07