Papa atakutana na vijana wa Roma 10 Januari 2026!
Na Angella Rwezaula- Vatican
Tukio hilo la Jumamosi, tarehe 10 Januari 2025, saa 11:00 jioni katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican litakuwa lisilokosekana. Siku chache tu kabla ya mwisho wa Jubilei ambayo itahitimishwa rasmi siku ya Epifania ya Bwana kwa kufungwa Mlango Mtakatifu wa Basilika ya Mtakatifu Petr, vijana wa kike na kiume, barubaru wa Roma watakutana na Papa Leo XIV na kusikiliza maneno yake.
Makundi mengi yatahudhuria
Hili lilitangazwa katika taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Vikariate ya Roma, ambayo inabainisha kuwa vijana wengi watahudhuria: kuanzia wanafunzi wa katekisimu hadi wale wanaokusanyika katika vikundi vya parokia, kutoka wanachama wa harakati na vyama hadi wale waliojiandikisha katika vilabu vya michezo vya Kikatoliki, hadi wanafunzi wa vyuo vikuu, na wale wanaoishi mbali na nyumbani katika vyuo vikuu ndani ya Jimbo Kuu.
Reina:"utakuwa wakati wa furaha"
Ataye wasindikiza katika mkutano huu maalum na Papa atakuwa Kardinali Baldo Reina, Makamu wa Papa Jimbo Kuu la Roma ambaye alitangaza mkutano huo wakati wa kipindi cha maombi cha "Usiku katika Kanisa Kuu" kunako Novemba 21 iliyopita, na ambaye alirejesha mwaliko huo katika barua yake: "Itakuwa wakati wa thamani na furaha," Kardinali aliwaandikia mapadre, "ambao ninawaalika kuhimiza ushiriki wa vijana wa parokia zenu, nikiwahimiza wauone kama fursa muhimu ya kusikiliza maneno ya Askofu wetu."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku, bofya hapa tu:Just click here
