Bendera ya Australia katikati ya maua na mishumaa ya heshima kuwaenzi waathirika wa shambulio la risasi katika sherehe ya Wayahudi,Dominika Desmba 14 katika Ufukwe wa Bondi,Sydney. Bendera ya Australia katikati ya maua na mishumaa ya heshima kuwaenzi waathirika wa shambulio la risasi katika sherehe ya Wayahudi,Dominika Desmba 14 katika Ufukwe wa Bondi,Sydney.  (REUTERS/Hollie Adams)

Papa Leo XIV kwenye simu na Herzog:alirudia kulaani aina zote za chuki dhidi ya Wayahudi

Papa Leo XIV alipokea simu kutoka kwa rais wa Israeli kabla ya Noeli na siku kuu ya Wayahudi ya Hanukkah.Kwa kuzingatia shambulio la Dominika kwenye Ufukwe wa Bondi,Papa alirudia kulaani vurugu zote dhidi ya Wayahudi na kuelezea matumaini yake kwamba"michakato ya amani itaendelea"katika Mashariki ya Kati na kwamba juhudi za misaada ya kibinadamu zitaendelea na kuimarika.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Papa Leo XIV alirudia kulaani aina zote za chuki dhidi ya Wayahudi, lawama aliyoitoa tayari baada ya shambulio la Sydney dhidi ya jumuiya ya Wayahudi, katika mazungumzo ya simu leo hii Desemba 17 ​​na Rais wa Israeli Isaac Herzog. Papa alirudia wito wake kwa Herzog "kuendelea katika michakato ya amani inayoendelea" katika Mashariki ya Kati na kuongeza juhudi za kibinadamu, hasa kutokana na hali ilivyo huko Gaza, ambapo, baada ya vita, njaa, baridi, na hali mbaya ya hewa sasa vinaua watu.

Shambulio la Sydney

Taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican ilitangaza kwamba Papa "alipokea simu" kutoka kwa kiongozi wa Israeli "wakati wa sherehe zijazo za Noeli na siku kuu ya Kiyahudi ya Hanukkah." Kile kinachoitwa "Tamasha la Taa" ambalo jumuiya ya Wayahudi wa Sydney ilikuwa ikisherehekea Dominika, Desemba 14, kwenye Ufukwe maarufu wa Bondi wakat, i watu wawili wenye bunduki, baba na mtoto wake (mmoja wao aliuawa na polisi), walianza kuwafyatulia risasi watu, na kuwaua watu kumi na tano, akiwemo msichana wa miaka 10, na kuwajeruhi wengine 40. Karibu ishirini kati yao tayari wameruhusiwa kutoka hospitalini. "Kwa kuzingatia shambulio la kigaidi la hivi karibuni huko Sydney," taarifa ya Vatican inasomeka, kwamba "Papa Leo XIV alisisitiza kuhusu Kanisa Katoliki kulaani vikali aina zote za chuki dhidi ya Wayahudi, ambazo zinaendelea kupanda hofu katika jumuiya za Wayahudi na katika jamii ulimwenguni kote."


Papa alikuwa tayari ameelezea ukaribu na jumuiya ya Wayahudi na huzuni kwa waathirika na waliojeruhiwa wakati wa hotuba yake Jumatatu Desemba 15 na wafadhili wa Pango la kuzaliwa kwa Yesu na mti wa Noeli katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. Katika hotuba hiyo hiyo, pia alitoa wito: "Inatosha kwa aina hizi za vurugu dhidi ya Wayahudi! Lazima tuondoe chuki mioyoni mwetu." Kisha, katika telegramu iliyoelekezwa kwa Askofu Mkuu Anthony Fisher, iliyochapishwa siku hiyo hiyo na Mkutano, Papa Leo XIV alilaani "kitendo hiki cha vurugu kisicho na maana" na kuwaomba wale "wanaojaribiwa na vurugu wageuke na kutafuta njia ya amani na mshikamano."

Kudumu katika mchakato wa amani

Wito mwingine kutoka kwa Papa ilielezea simu ya leo hii Desemba 17 na Rais wa Israeli: "Kudumu katika michakato ya amani inayoendelea katika eneo hilo, pia ikisisitiza hitaji la dharura la kuimarisha na kuendeleza juhudi za misaada ya kibinadamu." Kulingana na ripoti kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na mashirika kadhaa ya ndani, dharura inaendelea katika Ukanda wa Gaza, huku vifo vingi na majeruhi kadhaa, ambao wanaona ni vigumu sana kupata matibabu katika hospitali za ndani, ambazo nyingi zimejaa watu kupita kiasi.

Katikesi ya Septemba 4

Haya ni mawasiliano ya pili ya moja kwa moja kati ya Papa Leo na Isaac Herzog, kufuatia Mkutano katika Jumba la Kitume la Vatican mnamo tarehe 4 Septemba 2025. Mkutano wa faragha uliofuatiwa na ule katika Sekretarieti ya Vatican, ambapo "hali ya kisiasa na kijamii katika Mashariki ya Kati ilishughulikiwa," kwa "umakini maalum" kwa hali ya kusikitisha huko Gaza na "marejeo ya kinachoendelea katika Ukingo wa Magharibi na suala muhimu la Jiji la Yerusalemu.

17 Desemba 2025, 17:00