Tafuta

Papa shuleni Castel Gandolfo:"Noeli ni mwaliko wa furaha na amani"

katika wakati wa Noeli ni muhimu kujenga amani na umoja,ndivyo Papa Leo XIV aliwaeleza watoto alioungana nao katika tamasha la Noeli la shule huko Castel Gandolfo na wazazi wao huku akielezea kuhusu zawadi ya upendo wakati wa Siku Kuu ya Kuzaliwa kwa Bwana:"Mungu alipenda kuwasiliana nasi kwa lugha ya zawadi ya upendo."

Na Tiziana Campisi – Vatican.

Ziara maalum iliashiria toleo la kumi na moja la tamasha la Noeli liitwalo “InCanto”, lililofanywa na wanafunzi wa Shule ya Kipapa ya Paulo VI ya Castel Gandolfo, Jumanne tarehe 16 Desmba 2025. Miongoni mwa waliohudhuria alasiri hii alikuwa Papa Leo XIV. Baada ya kuondoka Villa Barberini iliyo karibu, ambapo anakwenda sasa mara kwa mara kila Jumanne, Papa alitembelea shule hiyo na kisha akaukana watoto wa shule ya Msingi na familia zao kwenye ukumbi wa mazoezi kwa ajili ya Tamasha hilo la nyimbo. Tamasha hilo lilikuwa ni fursa watoto kuwatakia kila mtu Noeli  Njemaminayoakaribia, na kusisitiza kwamba utajiri wa kweli haupimwi kwa kile mtu anachopokea, bali kwa amani ambayo mtu anaweza kuzalisha ndani yake na katika uhusiano na wengine.

Watoto wakiimba nyimbo za Noeli
Watoto wakiimba nyimbo za Noeli   (@Vatican Media)

Noeli  huamsha furaha na amani

Wanafunzi, wote wakiwa wamevaa jeans na mashati meupe, walichukua nafasi zao kwenye jukwaa lenye ngazi. Wakitabasamu na kuguswa waziwazi, waliimba nyimbo mbalimbali za Noeli. Midundo ya nyimbo za Adeste fideles, Joy to the World, Noël Noël na Astro del ciel,  ilijaza ukumbi wa mazoezi uliopambwa kwa sherehe, ukiwa umejaa wazazi, walimu, na wafanyakazi wa shule hiyo. Askofu Vincenzo Viva, wa Albano,  na Rais wa Utawala wa Urithi wa Kiti cha Kitume, Monsinyo Giordano Piccinotti, na Papa walikuwa wamekaa katika safu ya mbele.

Papa akiwasalimia watoto
Papa akiwasalimia watoto   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo "Mwishoni mwa tamasha," Papa Leo  XIV alisema, "Ilikuwa nzuri kusikiliza nyimbo za Noeli  kwa lugha ya Kiitaliano, Kilatini, Kiingereza na Kihispania." Papa aliongeza kusema kuwa “kuwasikia watoto wakiimba kwa lugha tofauti husaidia kila mtu kuelewa kwamba Noeli  huamsha furaha na amani katika mioyo ya kila mtu. Papa pia alitoa shukrani zake kwa mwaliko huo, akiongeza, kwa tabasamu, kwamba umefika "kwa njia ya ajabu" na kwamba alifurahi kuukubali mwaliko huo.

Papa akihutubia
Papa akihutubia   (@Vatican Media)

Mwaliko wa kufanya zaidi kwa ajili ya amani

Akitafakari moja ya nyimbo zilizoimbwa, zenye mashairi yanayorejea "Malaika wanaoleta upendo," Papa alibainisha kuwa ni watoto wenyewe malaika  walioleta upendo kupitia muziki wao. Alikumbuka maneno ya Mtakatifu Agostino, ambaye alisema kwamba "yule apendaye huimba," kwa sababu upendo huwezesha moyo kuelewa kile kilicho muhimu kweli.” "Mungu alitaka kutupatia sote zawadi ya upendo: hivi ndivyo Noeli  ilivyo," Papa Leo XIV alisisitiza kwamba Mungu hukaribia wanadamu, hasa kwa wadogo na walio hatarini zaidi. Na alielezea matumaini kwamba roho hiyo, inayosherehekewa wakati wa Noeli, inaweza kuishi si tu katika siku hizi bali mwaka mzima.

Papa akiwahutubia watoto na wazazi
Papa akiwahutubia watoto na wazazi   (@Vatican Media)

Akinukuu kiitikio cha wimbo mwingine, Papa aliongeza, "Kwetu sisi huu ni mwaliko mzuri: kufanya zaidi kutangaza amani, upendo na umoja duniani." Na kumwona Mungu katika jambo dogo kati yetu. Kwa kumalizia, Papa Leo aliwapatia baraka zake watoto na familia zao, akiwatia moyo kusali pamoja na kufungua mioyo yao ili kutambua uwepo wa Mungu, hasa katika wale wadogo. Papa alipokelewa kwa makofi na shangwe za furaha. Alipokea hata  raketi ya tenisi na sare ya shule kama zawadi, na akapiga picha ya ukumbusho na wanafunzi kabla ya kuondoka.

Papa alipokea  zawadi ya Raketi
Papa alipokea zawadi ya Raketi   (@Vatican Media)

Shule ya Kipapa Paulo VI

Shule ya Kipapa Paulo VI ya Castel Gandolfo ni shule ya msingi ya Kikatoliki iliyoko takriban mita 700 kutoka Villa Barberini, nyumba ya Kipapa ya  mapumziko ya Papa. Papa Paulo VI alihamaisha  ujenzi wa jengo hilo  kama zawadi kwa jamii ya wenyeji mahali hapo, na ilizinduliwa na Papa mwenyewe mnamo tarehe 12 Septemba 1968. Katika hafla hiyo, alisisitiza umuhimu wa elimu ya Kikatoliki kwa watoto na vijana. Leo hii, shule inakaribisha kuwa na takriban wanafunzi 300 na inatoa programu ya kielimu iliyoongozwa na kanuni za Kikatoliki, iliyoimarishwa na shughuli za nje ya shule ikiwa ni pamoja na michezo, muziki, lugha za kigeni, elimu ya uraia na elimu ya chakula.

Picha ya Pamoja ya Papa na watoto wa shule
Picha ya Pamoja ya Papa na watoto wa shule   (@Vatican Media)
Papa akiwa anaondoka
Papa akiwa anaondoka   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku,bonyea hapa: Just click here

16 Desemba 2025, 20:29