Papa Leo XIV alisali katika bandari ya Beirut:Ukimya na mkumbatio kwa manusura
Vatican News
Katika siku yake ya Mwisho ya Ziara yake ya Kitume nchini Lebanon, Baba Mtakatifu Leo XIV, Jumatano tarehe 2 Novemba 2025 ilimwona akitembelea mahali ambapo pamekuwa mandhari ya waliokufa katika umbo la maghala makubwa yaliyopuka yakionekana kutokea angani, marundo vifusi, magari yaliyochomwa yakiwa yamerundikana juu ya kila mmoja. Ni katika bandari ya Beirut ambayo Papa Leo aliwasalimia watu manusura na familia za waliokufa katika ajali hiyo mbaya iliyotokea ya mlipuko wa kutisha mnamo Agosti 2020 ambayo iliwaua zaidi ya watu 240 na kujeruhi 7,000.
Kwa hiyo Papa Leo aliwasalimia hawa mmoja baada ya mwingine, huku wakilia au mikono yao ikiwa imefunika midomo yao, wote wakiwa wamejipanga mstari na sura zikionesha huzuni au machozi.
Kwanza, kabisa mara baada ya kufika Papa Leo, alisimama kusali mbele ya Mnara huo wa ukumbusho wa marumaru unaoorodhesha majina yote ya wale ambao maisha yao yaliuawa na mlipuko huo, ili kutoa heshima yao. Papa Leo XIV alisimama kwa muda mrefu akisali kwa kimya, huku mikono yake ikiwa imeshikamana mbele ya nguzo. Katika hatua fulani, alitazama juu na kuanza kutembea kuelekea kwenye mnara.
Alipiga magoti kuweka shada la waridi nyekundu, kisha alisimama tena na kufungua mikono yake, akiinua juu. Sala, baraka, yote kimya kimya. Mdomo wa Papa uliweza kuonekana ukisonga na ananong'ona kitu cha ukimya.
