Tafuta

Papa Leo XIV,Harissa:tunaweza kutumaini tena kesho,hata katika uchungu wa magumu ya sasa

Papa Leo XIV katika Siku ya Pili akiwa katika Nchi ya Mwerezi,alitembelea Madhabahu ya Maria huko Harissa na kukutana na Maaskofu,Mapadre na waliowekwa wakfu ambao walisimulia historia za mshikamano,vita,uhamiaji na huduma za gerezani.Papa aliwatia moyo:'Tukitaka kujenga amani ni lazima tutitie nanga mbinguni na,tukiwa tumejikita katika mwelekeo huo,tupende bila kuogopa kupoteza vitu hivyo vinavyopita na tutoe bila kipimo.'

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Kulikuwa na shuhuda zilizotolewa katika Mkutano wa Maaskofu, Makleri, watu waliowekwa wakfu na Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa katika Ziara yake ya kwanza ya Kitume nchini Lebanon, ambapo, siku yake ya Pili nchini humo awali alitembelea Kaburi la Mtakatifu Charbel huko Annaya na baadaye kufika katika Madhabahu ya Mtakatifu Paulo II ya Mama Yetu wa Harissa  Jumatatu tarehe 1 Desemba 2025. Kabla ya hotuba yake,  walitoa shuhuda mbalimbali Padre Youhanna-Fouad Fahed, Sr Dima, Loren, Padre Charbel.

Mkutano wa Maaskofu, Watawa na Makleri
Mkutano wa Maaskofu, Watawa na Makleri   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV alianza kusema kuwa ni furaha kubwa kwangu kukutana nanyi wakati wa ziara hii, ambayo kauli mbiu yake ni “Heri wapatanishi” (Mt 5:9). Kanisa la Lebanon, lililoungana katika pande zake mbalimbali, ni taswira ya maneno haya, kama Mtakatifu Yohane Paulo II alivyothibitisha kwa upendo mkubwa kwa watu wenu alisema: “Katika Lebanon ya leo, ninyi ndio mnaowajibika kwa tumaini” (Ujumbe kwa Raia wa Lebanon, 1 Mei 1984); na akaongeza, “Undeni, hapo mnapoishi na kufanya kazi, katikahali ya kidugu. Bila busara, na mujue jinsi ya kuwaamini wengine na kuwa wabunifu ili nguvu ya kuzaliwa upya ya msamaha na huruma ishinde.”

Papa Leo XIV alisema kuwa shuhuda ambazo tumesikia  shukrani kwa kila mmoja wenu! zinatuambia kwamba maneno haya hayakusemwa bure. Kiukweli, yamepokelewa vizuri na kufanyiwa kazi kwa sababu ushirika wa upendo unaendelea kutengenezwa hapa Lebanon. Kwa maneno ya  Patriaki, ambaye ninamshukuru kwa dhati, tunaweza kugundua asili ya uthabiti huu, unaooneshwa na pango la kimya ambalo Mtakatifu Charbel alisali mbele ya Sanamu ya Mama wa Mungu, na kwa uwepo wa Madhabahu ya Harissa, ishara ya umoja kwa watu wote wa Lebanon.

Madhabahuni ya Mama Yetu wa Harissa
Madhabahuni ya Mama Yetu wa Harissa   (@Vatican Media)

Papa alisisitiza kwamba ni katika kuwa na Maria chini ya Msalaba wa Yesu (taz. Yh 19:25) kwamba sala yetu, daraja lisiloonekana linalounganisha mioyo, hutupatia nguvu ya kuendelea kutumaini na kufanya kazi, hata tunapozungukwa na sauti ya silaha na wakati mahitaji muhimu ya maisha ya kila siku yanapokuwa changamoto. Mojawapo ya alama zinazooneshwa katika nembo ya Ziara hii ni nanga. Papa Francisko mara nyingi aliitaja nanga kama ishara ya imani inayoturuhusu kusonga mbele kila wakati, hata katika nyakati za giza zaidi, hadi tufike mbinguni. Alisema: "Imani yetu ni nanga mbinguni. Tumetia nanga maisha yetu mbinguni.

Watawa katika madhabahu huko Harissa
Watawa katika madhabahu huko Harissa   (@Vatican Media)

Tunapaswa kufanya nini? kushikilia kamba… Na tunasonga mbele kwa sababu tuna uhakika kwamba maisha yetu yametia nanga mbinguni, kwenye ufuko ambapo tutafika" (rej. Katekesi, 26 Aprili 2017). Tukitaka kujenga amani ni lazima tutitie nanga mbinguni na, tukiwa tumejikita katika mwelekeo huo, tupende bila kuogopa kupoteza vitu hivyo vinavyopita na tutoe bila kipimo. Kutoka kwenye mizizi hii, yenye nguvu na kina kama ile ya mierezi, upendo hukua na kwa msaada wa Mungu, kazi thabiti na za kudumu za mshikamano huishi.

Padre Youhanna alituambia kuhusu Debbabiyé, kijiji kidogo anachofanya huduma yake. Huko, hata anapokabiliwa na uhitaji mkubwa na kutishiwa na mashambulizi ya mabomu, Wakristo na Waislamu, Walebanon na wakimbizi kutoka nchi zingine, wanaishi pamoja kwa amani na kuwasaidia majirani zao. Kwa njia hiyo Papa alisisitiza kwamba “Tuache kwa muda tufikirie ile picha aliyoitoa: sarafu ya Syria iliyopatikana kwenye sanduku la sadaka pamoja na zile kutoka Lebanon.

Padre Yohanna baada ya kutoa ushuhuda
Padre Yohanna baada ya kutoa ushuhuda   (@Vatican Media)

Ni jambo muhimu. Kwani picha hii inatukumbusha kwamba kila mmoja wetu ana kitu cha kutoa na kupokea kwa upendo, na kwamba zawadi yetu kwa jirani yetu inamtajirisha kila mtu na inatuvuta kwa Mungu. Papa Benedikto XVI, wakati wa ziara yake kwa nchi hiyo, alizungumzia kuhusu nguvu ya kuunganisha upendo hata wakati wa majaribu, akisema: "Ni hapa na sasa ambapo tumeitwa kusherehekea ushindi wa upendo dhidi ya chuki, msamaha dhidi ya kisasi, huduma dhidi ya utawala, unyenyekevu dhidi ya kiburi, na umoja dhidi ya mgawanyiko… kuwa na uwezo wa kubadilisha mateso yetu kuwa tamko la upendo kwa Mungu na huruma kwa jirani yetu" (Hotuba, Ziara ya Basilika ya Mtakatifu Paulo huko Harissa, 14 Septemba 2012). Ni kwa njia hiyo tu tunaweza kujikomboa kutokana na dhuluma na ukandamizaji, hata wakati, kama tulivyosikia, tunasalitiwa na watu na mashirika ambayo hutumia vibaya kukata tamaa kwa wale ambao hawana njia mbadala. Kwa hivyo, tunaweza kutumaini tena kesho, hata katika uchungu wa magumu ya sasa ambayo lazima tukabiliane nayo.

Kukuza Uwepo wa vijana

Katika suala hilo, Papa Leo XIV alikumbusha kuhusu jukumu tunalobeba sote kwa vijana. Ni muhimu kukuza uwepo wao, hata katika miundo ya Kanisa, kuthamini michango yao mipya na kuwapa fursa. Ni muhimu, hata miongoni mwa magofu ya ulimwengu ambao una mapungufu yake yenye uchungu, kuwapa matarajio halisi na yanayowezekana ya kuzaliwa upya na ukuaji wa siku zijazo.

Loren amezungumzia kuhusu kazi yake mwenyewe katika kuwasaidia wahamiaji. Akiwa mhamiaji mwenyewe, kwa muda fulani amekuwa akishughulika katika kuwasaidia wale wanaolazimishwa si kwa hiari bali kwa lazima kuacha kila kitu ili kutafuta mustakabali mpya mbali na nyumbani. Historia aliyosimulia kuhusu James na Lela inatugusa sana na inaonesha hofu ambayo vita husababisha katika maisha ya watu wengi wasio na hatia. Papa Francisko alitukumbusha mara nyingi katika hotuba na maandishi yake kwamba hatuwezi kubaki bila kujali tunapokabiliwa na mikasa kama hiyo, na kwamba huzuni yao inatuhusu na kutupatia changamoto (taz.mahubiri  Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani,29 Septemba 2019).

Loren baada ya kutoa ushuhuda
Loren baada ya kutoa ushuhuda   (@Vatican Media)

Kwa upande mmoja, ujasiri wao unatuambia kuhusu nuru ya Mungu ambayo, kama Loren alivyosema, huakisi hata katika nyakati za giza. Kwa upande mwingine, uzoefu wao unatualika kuwa na msimamo ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu mwingine atakayelazimika kukimbia kutoka nchi yake kutokana na migogoro isiyo na maana na ya kikatili, na kwamba yeyote anayebisha hodi kwenye milango ya jamii zetu asihisi kukataliwa kamwe, lakini anakaribishwa kwa maneno ambayo Loren mwenyewe alisema: "Karibu nyumbani!"

Ushuhuda wa Sr Dima unaweza pia kututia moyo. Alipokabiliwa na kuzuka kwa vurugu, alichagua kutoiacha kambi, bali kuweka shule wazi, na kuifanya iwe mahali pa kukaribishwa kwa wakimbizi na kituo cha elimu chenye ufanisi wa ajabu. Hakika, katika vyumba hivyo, zaidi ya kutoa msaada na msaada wa kimwili, mtu hujifunza na kufundisha kushirikisha "mkate, hofu na matumaini;" kupenda katikati ya chuki, kutumikia hata katika uchovu na kuamini katika mustakabali unaozidi kila matarajio.

Sr  Dima baada ya kutoa ushuhuda
Sr Dima baada ya kutoa ushuhuda   (@Vatican Media)

Kanisa nchini Lebanon limekuwa likikuza elimu kila wakati. Papa Leo aliwatia moyo wote kuendelea na kazi hii inayostahili sifa. Waache chaguo zao zinazochochewa na upendo wa ukarimu zaidi, wazitumikie kukidhi mahitaji, zaidi ya yote, ya wale ambao hawawezi kujisaidia wenyewe na wale wanaopatikana katika hali mbaya zaidi. Kwa njia hiyo, uundaji wa akili utaunganishwa kila wakati na elimu ya moyo. Tukumbuke kwamba shule yetu ya kwanza ni Msalaba na kwamba Mwalimu wetu mmoja ni Kristo (taz. Mt. 23:10).

Katika suala hilo, alipozungumzia uzoefu wake katika huduma ya gereza, Padre Charbel alisema kwamba hata pale ambapo ulimwengu unaona kuta na wahalifu pekee, tunaona huruma ya Baba, ambaye hachoki kusamehe, ikionekana machoni pa wafungwa, wakati mwingine wakipotea, wakati mwingine ikiangazwa na tumaini jipya. Na hii ni kweli: tunaona uso wa Yesu ukionekana katika wale wanaoteseka na katika wale wanaorekebisha majeraha ambayo maisha yamesababisha.

Baada ya kutoa ushuhuda
Baada ya kutoa ushuhuda   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV, aliwaeleza kuwa baada ya muda mfupi, ishara ya kuwasilisha Waridi la Dhahabu kwenye  Madhabahu hapo ingefanyika na kwamba “Ni ishara ya kale, ambayo miongoni mwa maana zake mbalimbali inatuhimiza kuwa, pamoja na maisha yetu, harufu ya Kristo (taz. 2 Kor. 2:14). Kabla ya picha hiyo, inakumbushwa harufu inayotoka kwenye meza za Lebanon, maarufu kwa aina nyingi za chakula kinachotolewa na hisia kali ya jumuiya inayopatikana katika kushiriki mlo.

Ni harufu iliyotengenezwa kwa harufu elfu moja ambayo inavutia katika utofauti wa harufu na hata katika mchanganyiko wake. Ndivyo ilivyo pia harufu ya Kristo. Sio bidhaa ghali iliyotengwa kwa ajili ya wachache waliochaguliwa, bali harufu inayotoka kwenye meza nyingi iliyojaa milo tofauti, ambapo wote wameitwa kushiriki. Hii iwe roho ya ibada ambayo tunakaribia kutekeleza, na zaidi ya yote roho ambayo tunajipa changamoto kila siku kuishi tukiwa tumeungana katika upendo.

Picha ya Pamoja na Mapatriaki
Picha ya Pamoja na Mapatriaki   (@Vatican Media)
Ndani ya madhabahu ya Mama Yetu Maria huko Harissa
Ndani ya madhabahu ya Mama Yetu Maria huko Harissa   (@Vatican Media)
Papa akipokea zawadi
Papa akipokea zawadi   (@Vatican Media)
Papa na maaskofu, mapadre na waliowekwa wakfu
Papa akipokea zawadi
Papa akipokea zawadi   (@Vatican Media)
Papa akibariki Jiwe la Msingi
Papa akibariki Jiwe la Msingi   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

01 Desemba 2025, 12:43