Tafuta

Papa Leo XIV: Biblia inatutia moyo kutoa kwa hiari na kwa nia nzuri. Inaonesha kwamba kutoa kwa njia hiyo kunamnufaisha anayepokea na anayetoa pia. Rej. Methali 11:25; Luka 6:38. Papa Leo XIV: Biblia inatutia moyo kutoa kwa hiari na kwa nia nzuri. Inaonesha kwamba kutoa kwa njia hiyo kunamnufaisha anayepokea na anayetoa pia. Rej. Methali 11:25; Luka 6:38.  

Papa Leo XIV: Kuna Furaha Zaidi Katika Kutoa Kuliko Ilivyo Katika Kupokea!

kipindi hiki cha Majilio ni mwaliko kwa waamini kukua katika fadhila ya: uvumilivu na kujikita katika maandalizi ya kukutana na Yesu, anayekuja kwa waamini wake katika: Sakramenti, Sala pamoja na mahusiano na wengine. Hushiriki wa watoto katika maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu, huku taa zikiwa zinawaka ni sehemu ya maandalizi ya kila mmoja wao ili imani, tumaini, na upendo viweze kushinda kila siku, hasa wanaposoma na kutafakari Maandiko Matakatifu.

Na Sr. Christine Masivo, - Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV anafundisha kwamba Kipindi cha Majilio ni mwaliko kwa waamini kukesha, kujikita katika toba, na wongofu wa ndani, kuachana na starehe za ulimwengu ili kufungua mioyo yao kwa ajili ya ujio wa Kristo Yesu. Huu ni mwaliko wa kuwa Kanisa la kitume linalojenga daraja na amani, na kutangaza na kushuhudia mwanga wa Kristo Yesu kwa njia ya: Sala, matendo ya huruma, na ushuhuda wa imani, hasa katika kukabiliana na changamoto mamboleo kama vile: Vita, umaskini, njaa na athari za mabadiliko ya tabianchi. Anawahimiza waamini kutumia fursa ya Kipindi cha Majilio kujitayarisha kiroho, siyo tu kwa ajili ya maadhimisho ya Sherehe za Noeli, bali pia kwa ajili ya Ujio wa pili wa Kristo Yesu atakapokuwa kuwahukumu wazima na wafu na kwamba, Ufalme wake hautakuwa na mwisho, akisisitiza kwamba Yesu atakuja kwa njia ya nuru na upendo.

Kuna furaha kubwa kutoa kuliko kupokea!
Kuna furaha kubwa kutoa kuliko kupokea!   (ANSA)

Ni katika muktadha wa maadhimisho ya Kipindi cha Majilio, Baba Mtakatifu Leo XIV ametuma salam na matashi mema kwa watoto wadogo Barani Ulaya wanaoshiriki katika Ibada ya Misa Takatifu kipindi hiki cha Majilio; Misa zinazojulikana kitamaduni kama “Rorate caeli desuper." Yaani “Mawingu yamwage kutoka juu” kama sehemu ya maandalizi ya Sherehe za Noeli. Katika kipindi cha mwaka 2025, takribani parokia 3, 500 zinashiriki na kwamba, hii ni fursa pia kwa watoto hawa kujifunza kuhusu maisha na utume wa Papa Leo XIV. Hizi ni Ibada za Misa Takatifu zinazoadhimishwa kwa ajili ya vijana asubuhi na mapema na baadaye jioni.

Majilio ni kipindi kwa waamini kukua katika fadhila ya uvumilivu
Majilio ni kipindi kwa waamini kukua katika fadhila ya uvumilivu   (© Natalia Pieśniewska, Kościół i Hospicjum św. Stanisława BM w Rzymie)

Majilio:waamini kukua katika fadhila ya uvumilivu

Baba Mtakatifu Leo XIV anasema, kipindi hiki cha Majilio ni mwaliko kwa waamini kukua katika fadhila ya uvumilivu na kujikita katika maandalizi ya kukutana na Kristo Yesu, anayekuja kwa waamini wake katika: Sakramenti, Maisha ya Sala pamoja na mahusiano na wengine. Hushiriki wa watoto katika maadhimisho ya Ibada ya Misa Takatifu, huku taa zikiwa zinawaka ni sehemu ya maandalizi ya kila mmoja wao ili imani, tumaini, na upendo viweze kushinda kila siku, hasa wanaposoma na kutafakari Maandiko Matakatifu, kwa kuwasaidia maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa vipaumble vya jamii; kwa kuwafariji wale wanao omboleza na kutafuta fura katika kutoa badala ya kutarajia kupokea. Biblia inatutia moyo kutoa kwa hiari na kwa nia nzuri. Inaonesha kwamba kutoa kwa njia hiyo kunamnufaisha anayepokea na anayetoa pia. Rej. Methali 11:25; Luka 6:38. Kristo Yesu alisema hivi: “Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.” Mdo 20:35. Mpango huu unaotekelezwa na Kanisa Katoliki nchini Poland unakusudia kuwasaidia watoto kumfahamu kwa karibu zaidi Papa Leo XIV, Maisha na Utume wake kama Khalifa wa Mtakatifu Petro.

Majilio Vijana wa Poland
19 Desemba 2025, 14:49