Papa Leo XIV:makampuni ni jumuiya za kibinadamu na za kidugu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV, alikutana na wawakilishi wa Shirika la Washauri wa Kazi, mjini Vatican tarehe 18 Desemba 2025, wakati wa hotuba yake alianza kuonesha furaha ya kukutana nao katika fursa ya Miaka 60 tangu kuwanishwa kwa chama cha Washauri wa Kazi. Juhudi ya kazi yao ni ya thamani na yenye uwajibikaji, inayohitaji umahiri na hisia ya haki. Papa alipenda kuakisi vipengele vitatu vyake ambavyo aliviona kuwa muhimu sana: kulinda hadhi ya binadamu, upatanishi, na kukuza usalama. Katika kipengele cha kwanza, Papa Leo alipenda kutumia maneno ya Papa Francisko kwamba “kufanya kazi sisi tunakuwa watu, ubinadamu wetu unachanua, vijana wanakuwa watu wazima “(Dilexi te, 115). Maneno haya yanatukumbisha kuwa kinii cha maisha yote ya kazi kisiwekwe kamwe katika mtaji, na wala katika sheria za masoko, wala za faida bali watu, familia na wema wao, heshima kwa kwa kila kitu ambacho kinafanya kazi.
Umuhimu huu, unaothibitishwa kila mara na Mafundisho ya Jamii ya Kanisa (taz.Mtakatifu Yohane Paulo II katika Waraka wake wa Centesimus Annus, 3; 5), lazima uzingatiwe katika mipango na mipango yote ya biashara, ili wafanyakazi watambuliwe katika hadhi yao na kupokea majibu halisi kwa mahitaji yao halisi. Kwa mfano, nafikiria hitaji la kukidhi mahitaji ya familia changa na wazazi wenye watoto wadogo, pamoja na umuhimu wa kuwasaidia wale ambao, licha ya kufanya kazi, lazima wawatunze wazee na wagonjwa wa familia. Haya ni mahitaji ambayo hakuna jamii iliyostaarabika kweli inayoweza kumudu kuyasahau au kuyapuuza, na una njia ya kuwasaidia wale wanaojitahidi kuyashughulikia. Leo, katika muktadha ambapo teknolojia na akili unde zinazidi kudhibiti na kushawishi shughuli zetu, ni muhimu kuhakikisha kwamba makampuni yanatambuliwa kwanza kabisa kama jamii za kibinadamu na za kidugu.
Mantiki ya pili ni ni upatanishi. Katika mienendo ya makampuni, kazi yao kwa namna fulani ni kama zipu ya makubaliano kati ya wakuu wa kazi na wafanyakazi, kwa kurahisisha uhusiano muhumu iwe kwa upande wa kufanya kazi vizuri kampuni na kwa ajili ya wema kwa wale wanaofanya kazi. Kama washauri wa ajira, mnasimamia vipengele vya kisheria na kiutawala ambavyo ni muhimu kwa maisha ya wafanyakazi na familia zao, mkisaidia makampuni na wafanyakazi katika masuala ya mikataba, kuajiri, michango, na mambo mengine mengi. Katika jukumu hili, majaribu mawili yanaweza kutokea: kwa upande mmoja, urasimu mwingi katika mahusiano; kwa upande mwingine, umbali na kujitenga na ukweli. Vyote viwili vina madhara, kwa sababu hatimaye, hufanya mazingira ya kampuni kutoweza kuishi, na kuizuia kuwa, kulingana na wito wake wa kweli, ushirikiano wa pamoja(Evangelii gaudium, 218-219).
Papa alikazia kusema :“Kwa hivyo aliwasihi wasiishi taaluma yao kwa kuzingatia mwajiri, kana kwamba mambo mengine yote hayakuwa muhimu sana. Mtakatifu Yohane, katika Barua yake ya Kwanza, anaandika: "Mtu akiwa na mali za dunia, akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamfungia moyo wake, upendo wa Mungu ukaaje ndani yake?"(1 Yh 3:17). Kwa kuzingatia maneno haya, mnapopatanisha washirika wa kijamii, nawasihi mfungue macho yenu kila wakati kwa watu walio mbele yenu, hasa wale walio katika shida na wasioweza kuelezea mahitaji yao na kutetea maslahi yao. Hili ni tendo kubwa la haki na upendo.”
Na kupengele cha mwisho ni kuhamasisha usalama. Katika mapendekezo hayo, Katika suala hili, kazi yao ya kuzuia ajali kupitia mafunzo ya wafanyakazi na kozi za kujikumbusha ni muhimu sana. Ni huduma kwa maisha yao. Papa Leo alikazia kusema kuwa kwa bahati mbaye leo hii ajali nying na vifo vingin(Morti bianche” vinavyotokea katika maeneo ya kazi. Sehemu zinazopaswa kuwa za maisha, mahali ambapo wati wanapitia kila siku yaokwenye sehemu zakazi na kutona nafadi kubwa ya nguvu yao , mata nyingi zinanageuka kuwa maendeo ya vifo na upweke. Papa emependa kuwakumbusha kuwa usalama katika kazi ni kama hewa ya kuvuta. Tunatambua umuhii wake wakati kwabahati mbaya unakosa na damaima tumeisha chelewa.” Heti Kuzuia kuliko kuponya na ndiyo lengo lao lenye thamani ya mchango wa mafunzo. Papa aliwambia kuwa wao wana kazi kubwa. Aliwatia moyo kuhitimisha kwa ari na moyo kwa utambuzi kuwa kaka na dada wengi wanawategemea mchango wao wa kazi ili kufanya kwa utulivu wa kazi zao za kila siku. Papa anawakabidhi kwa Bikira Maria, Mtakatifu Yosefu, Msimamizi wa Wafanyakazi na wakati huo kwao na familia zao, Papa aliwapatia Baraka ya kitume. Nakuwatakia heri ya Noeli Takatifu.
