Tafuta

Katika Ujumbe wa Papa wa Amani 2026 Papa anasema: Katika Ujumbe wa Papa wa Amani 2026 Papa anasema:  (@Vatican Media)

Ujumbe wa Siku ya Amani 2026:“Amani iwe Nanyi,ziamshwe dhamiri”

Katika Ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Siku ya 59 ya Amani Duniani unaoongozwa na kauli mbiu:"Amani iwe nanyi nyote.Kuelekea amani isiyo na silaha inayoondoa Silaha,” analaani vikali mbio za silaha zinazoendelea duniani,huku matumizi ya kijeshi yakiongezeka kwa 9.4% mwaka 2024.Papa anawahimiza waamini kuwa na taadhari dhidi ya unyonyaji wa dini kwa kidizisha utaifa,vita na migogoro ya silaha:"kutumia jina la Mungu katika vita ni kufuru.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu leo XIV ametoa Uchambuzi mkali, lakini unaofariji kwa matumaini yanayojitokeza, katika ujumbe wake wa Siku ya 59 ya Amani Duniani, itakayo adhimishwa tarehe 1 Januari 2026, kwa ujumbe uliochapishwa tarehe 18 Desemba 2025 ukiongozwa na kauli mbiu: “Amani iwe nanyi nyote. Kuelekea amani isiyo na silaha na amani inayoondoa silaha.” Ikumbukwe haya yalikuwa ni maneno yake ya kwanza kabisa mara tu alipojionesha katika Ulimwengu, katika siku ya kuchuguliwa kwake mnamo Mei 8, akiwa mbele ya dirisha la kutolea Baraka mjini Vatican.

Katika ujumbe wa Papa Leo XIV anaandika kuwa “Amani iwe nanyi: ni salamu ya zamani ambayo leo hii kila siku katika tamaduni nyingi, katika usiku wa Pasaka ilijaza nguvu mpya katika midomo  ya Yesu Mfufuka: “Amani iwe nanyi”(Yh 20,19.20). Ni Neno lake ambalo halitoi matashi mema tu, bali kutimiza mabadiliko ya mwisho,  kwa yule anayepokea, na kwa hiyo hali halisi yote.  Papa Leo  anabainisha  kuwa,  kwa njia hiyo Wafuasi wa Mitume wanatoa sauti kila siku na katika ulimwenguni kote kwenye mapinduzi ya kimya zaidi. “Amani iwe nanyi.” Tangu usiku ule wa uchaguzi wangu kama Askofu wa Roma, nilipenda kuingiza salamu hii katika tangazo la pamoja. Na ninatamani kurudia tena: hii ndiyo amani ya Kristo Mfufuka, amani isiyo na silaha na amani inayoondoa silaha, nyenyekevu na vumilivu. Inakuja kutoka kwa Mungu. Mungu ambaye anapenda bila kulazimisha.

Amani ya Kristo aliyefufuka

Mchungaji Mwema, anayetoa uhai wake kwa ajili ya kundi na ana kondoo wengine ambao si wa zizi hili(taz.Yh. 10:11,16), ni Kristo, amani yetu, ambaye ameshinda kifo na kubomoa kuta za mgawanyiko zinazotenganisha ubinadamu (taz. Efe. 2:14). Uwepo wake, zawadi yake na ushindi wake vinaendelea kung'aa kupitia uvumilivu wa mashahidi wengi ambao kupitia wao kazi ya Mungu huendelea duniani, ikionekana zaidi na kung'aa katika giza la nyakati zetu. Tofauti kati ya giza na nuru si tu taswira ya kibiblia inayoelezea maumivu ya uzazi ya ulimwengu mpya unaozaliwa; pia ni uzoefu unaotusumbua na kutuathiri katikati ya majaribu tunayokabiliana nayo katika hali zetu za kihistoria.

Ili kushinda giza, ni muhimu kuona nuru na kuiamini. Huu ni wito ambao wanafunzi wa Yesu wanaalikwa kuishi kwa njia ya kipekee na ya upendeleo; lakini pia hupata njia yake katika kila moyo wa mwanadamu. Amani ipo; inataka kukaa ndani yetu. Ina nguvu ya upole ya kuelimisha na kupanua uelewa wetu; inapinga na kushinda vurugu. Amani ni pumzi ya milele: huku tukilia kwa uovu kwamba "Inatosha," kwa amani tunanong'oneza "Milele," katika upeo huu Aliyefufuka ametuongoza. Tukiungwa mkono na imani hii, hata katikati ya kile ambacho Papa Francisko alikiita "vita vya tatu vya dunia vilivyomegeka vipande vipande," wapatanishi wanaendelea kupinga kuenea kwa giza, wakisimama kidete kama walinzi usiku.

Ujumbe wa Papa wa Siku ya Amani 2026 mwendelezo wa mawazo ya upapa wake

Cha kusikitisa kuna kusahau nuru

Baba Mtakatifu Leo XIV  aidha anabainisha kuwa cha kusikitisha, inawezekana pia kusahau nuru. Wakati hii inatokea, tunapoteza hisia zetu za uhalisia na kujisalimisha kwa mtazamo wa sehemu na uliopotoka wa ulimwengu, ulioharibiwa na giza na hofu. Wengi leo huita "uhalisia" masimulizi hayo yasiyo na tumaini, yaliyopofushwa kwa uzuri wa wengine na yaliyosahau neema ya Mungu, ambayo hufanya kazi kila wakati katika mioyo ya wanadamu, ingawa yamejeruhiwa na dhambi. Mtakatifu Agostino aliwahimiza Wakristo kujenga uhusiano usiovunjika na amani, ili kwa kuithamini kwa undani mioyoni mwao, waweze kuangaza joto lake linalong'aa karibu nao.

Akihutubia Jumuiya yake, aliandika: "Ikiwa mnataka kuwavuta wengine kwenye amani, kwanza iweni nayo ninyi wenyewe; iweni imara katika amani ninyi wenyewe. Ili kuwachoma wengine, ni lazima mwali uwake ndani yenu." Kaka na dada wapendwa, iwe tuna kipawa cha imani au tunahisi tunakosa, hebu tujifungulie kwa amani! Tuipokee na kuitambua, badala ya kuamini kuwa haiwezekani na kwamba hatuwezi kuifikia. Amani ni zaidi ya lengo tu; ni uwepo na safari. Hata wakati iko hatarini ndani yetu na karibu nasi, kama mwali mdogo unaotishiwa na dhoruba, ni lazima tuilinde, bila kusahau majina na historia za wale walioishuhudia. Amani ni kanuni inayoongoza na kufafanua chaguo zetu. Hata katika maeneo ambapo kifusi tu kinabaki, na kukata tamaa kunaonekana kuepukika, bado tunapata watu ambao hawajasahau amani. Kama vile jioni ya Pasaka Yesu aliingia mahali ambapo wanafunzi wake walikuwa wamekusanyika kwa hofu na kukata tamaa, vivyo hivyo amani ya Kristo aliyefufuka inaendelea kupita milango na vizuizi katika sauti na nyuso za mashahidi wake. Zawadi hii inatuwezesha kukumbuka wema, kuutambua kama ushindi, kuuchagua tena, na kufanya hivyo pamoja.

Amani isiyo na silaha

Baba Mtakatifu Leo anaendelea kutafakari kuwa, muda mfupi kabla ya kukamatwa, katika wakati wa kujiamini sana, Yesu aliwaambia wale waliokuwa pamoja naye: “Amani nawaachieni; amani yangu nawapa. Siwapi kama ulimwengu utoavyo.” Na mara moja akaongeza: “Mioyo yenu isifadhaike, wala msiogope” (Yh 14:27). Dhiki na hofu yao hakika ilihusiana na vurugu ambayo ingempata mapema. Lakini, kwa undani zaidi, Injili hazifichi ukweli kwamba kilichowasumbua wanafunzi ni jibu lake lisilo la vurugu: njia ambayo wote, Petro wa kwanza kati yao, waliipinga; lakini Bwana aliwaomba wafuate njia hii hadi mwisho. Njia ya Yesu inaendelea kusababisha wasiwasi na hofu. Anarudia kwa uthabiti kwa wale ambao wangemtetea kwa nguvu: “Rudisha upanga wako alani mwake” (Yohana 18:11; tazama Mt. 26:52). Amani ya Yesu aliyefufuka haina silaha, kwa sababu yake ilikuwa mapambano yasiyo na silaha katikati ya hali halisi za kihistoria, kisiasa na kijamii. Wakristo lazima kwa pamoja watoe ushuhuda wa kinabii kwa jambo hili jipya, wakikumbuka mikasa ambayo mara nyingi wamekuwa washiriki. Mfano mkuu wa Hukumu ya Mwisho unawaalika Wakristo wote kutenda kwa huruma katika ufahamu huu (taz. Mt. 25:31-46).

Kwa kufanya hivyo, watapata ndugu na dada kando yao ambao, kwa njia tofauti, wamesikiliza maumivu ya wengine na kujiweka huru ndani kutokana na udanganyifu wa vurugu. Ingawa watu wengi leo wana mioyo iliyo tayari kwa amani, mara nyingi hushindwa na hisia kubwa ya kutokuwa na nguvu mbele ya ulimwengu unaozidi kutokuwa na uhakika. Mtakatifu Agostino alikuwa tayari ameelezea kitendawili hiki maalum: "Si vigumu kuwa na amani; labda, ni vigumu zaidi kuisifu. Kuisifu amani, tunaweza kugundua kuwa hatuna kipaji kinachohitajika; tunatafuta mawazo sahihi na kupima maneno yetu. Lakini kuwa na amani, iko pale, karibu, na tunaweza kuimiliki bila juhudi." Tunapoichukulia amani kama wazo la mbali, tunaacha kushtushwa inapokataliwa, au hata vita vinapopiganwa kwa jina lake. Tunaonekana kukosa "mawazo sahihi," maneno yaliyofikiriwa vizuri na uwezo wa kusema kwamba amani iko karibu. Wakati amani si ukweli unaoishi, unaokuzwa na kulindwa, basi uchokozi huenea katika maisha ya nyumbani na ya umma.

Mahusiano kati ya raia na watawala

Katika mahusiano kati ya raia na watawala, inaweza hata kuchukuliwa kuwa kosa kutojiandaa vya kutosha kwa vita, kutojibu mashambulizi, na kutorudisha vurugu kwa vurugu. Zaidi ya kanuni ya ulinzi halali, mantiki kama hiyo ya makabiliano sasa inatawala siasa za kimataifa, ikizidisha ukosefu wa utulivu na kutotabirika siku hadi siku. Si bahati mbaya kwamba wito unaorudiwa wa kuongeza matumizi ya kijeshi, na chaguzi zinazofuata, zinawasilishwa na viongozi wengi wa serikali kama jibu linalofaa kwa vitisho vya nje. Wazo la nguvu ya kuzuia nguvu za kijeshi, hasa kuzuia nyuklia, linategemea kutokuwa na mantiki kwa mahusiano kati ya mataifa, yaliyojengwa sio juu ya sheria, haki na uaminifu, bali juu ya hofu na utawala kwa nguvu. "Kwa hivyo," kama Mtakatifu Yohane XXIII alivyoandika tayari katika siku zake, "watu wanaishi katika hofu ya kila wakati. Wanaogopa kwamba wakati wowote dhoruba inayokuja inaweza kuwaangukia kwa vurugu za kutisha. Na wana sababu nzuri za hofu yao, kwani hakika hakuna ukosefu wa silaha kama hizo.

Changamoto si uwekezaji wa kiuchumi bali pia mabadiliko ya sera za elimu

Ingawa ni vigumu kuamini kwamba mtu yeyote angethubutu kuchukua jukumu la kuanzisha mauaji na uharibifu mbaya ambao vita vitaleta, hakuna ubishi kwamba moto huo unaweza kuanzishwa kwa bahati nasibu na hali isiyotarajiwa." Zaidi ya hayo, ikumbukwe kwamba matumizi ya kijeshi duniani yaliongezeka kwa 9.4% mwaka  2024 ikilinganishwa na mwaka uliopita, ikithibitisha mwenendo wa miaka kumi iliyopita na kufikia jumla ya dola bilioni 2718 (au 2.5% ya Pato la Taifa la kimataifa). Zaidi ya hayo, majibu ya changamoto mpya yanaonekana kuhusisha sio tu uwekezaji mkubwa wa kiuchumi katika uundaji upya, lakini pia mabadiliko katika sera za elimu. Badala ya kukuza utamaduni wa kumbukumbu unaohifadhi ufahamu uliopatikana kwa shida wa karne ya ishirini na mamilioni ya waathiriwa, sasa tunaona kampeni za mawasiliano na programu za elimu,  katika shule, vyuo vikuu na kwenye vyombo vya habari,  zinazoeneza mtazamo wa vitisho na kukuza wazo la ulinzi na usalama tu. Na bado, "wale wanaopenda amani kweli pia huwapenda maadui wa amani." Kwa hivyo Mtakatifu Agostino alishauri kutotumia madaraja au kuendelea kulaumiwa, bali kupendelea kusikiliza na, inapowezekana, kushiriki katika majadiliano na wengine.

Miaka sitini ya Mtaguso wa II wa Vatican

Miaka sitini iliyopita, Mtaguso wa Pili wa Vatican ulihitimishwa kwa ufahamu mpya wa hitaji kubwa la mazungumzo kati ya Kanisa na ulimwengu wa kisasa. Hasa, Katiba ya Gaudium na Spes ilielekeza umakini kwenye mageuzi ya vita: “Hatari za kipekee kwa vita vya kisasa zinajumuisha ukweli kwamba zinawaweka wale wanaomiliki silaha zilizotengenezwa hivi karibuni katika hatari ya kufanya uhalifu kama huu na, kwa msururu usioweza kuepukika wa matukio, ya kuwahimiza watu kufanya vitendo viovu zaidi. Ili kuepuka uwezekano wa hili kutokea wakati wowote ujao, maaskofu wa dunia walikusanyika pamoja kuwasihi kila mtu, hasa viongozi wa serikali na washauri wa kijeshi, kuzingatia bila kukoma majukumu yao makubwa mbele za Mungu na mbele ya jamii nzima ya wanadamu. Tukirejea wito  wa Mababa wa Baraza, na tukizingatia mazungumzo kuwa njia bora zaidi katika kila ngazi, lazima tukubali kwamba maendeleo zaidi ya kiteknolojia na utekelezaji wa kijeshi wa akili unde(AI) vimezidisha janga la migogoro ya silaha.

Tabia vya viongozi wa kisiasa na kijeshi kukwepa uwajibikaji

Kuna hata tabia inayoongezeka miongoni mwa viongozi wa kisiasa na kijeshi ya kukwepa uwajibikaji, kwani maamuzi kuhusu maisha na kifo yanazidi "kukabidhiwa" kwa mashine. Hii inaashiria usaliti usio wa kawaida na uharibifu wa kanuni za kisheria na kifalsafa za ubinadamu ambazo ni msingi na kulinda kila ustaarabu. Ni muhimu kukemea viwango vikubwa vya maslahi ya kiuchumi na kifedha ya kibinafsi ambayo yanaendesha Mataifa katika mwelekeo huu; lakini hilo pekee halingetosha, isipokuwa pia tuamshe dhamiri na mawazo muhimu.

Waraka wa  Fratelli Tutti unamwasilisha Mtakatifu Francis wa Assisi kama mfano wa mwamko kama huo: "Katika ulimwengu wa wakati huo, uliojaa minara ya ulinzi na kuta za ulinzi, miji ilikuwa ukumbi wa vita vya kikatili kati ya familia zenye nguvu, hata umaskini ulipokuwa ukienea mashambani kote. Lakini hapo Francis aliweza kukaribisha amani ya kweli moyoni mwake na kujiweka huru kutokana na hamu ya kutumia mamlaka juu ya wengine. Akawa mmoja wa maskini na akajitahidi kuishi kwa amani na wote.” Hii ni simulizi ambayo tumeitwa kuendelea nayo leo hii, na hiyo ina maana ya kuunganisha nguvu ili kuchangia amani isiyo na kikomo, amani inayotokana na uwazi na unyenyekevu wa kiinjili.

“Amani ya kuondoa silaha”

Wema ni kuondoa silaha. Labda hii ndiyo sababu Mungu alikua mtoto. Fumbo la Umwilisho, ambalo hufikia mteremko wake wa ndani kabisa hata kwenye ulimwengu wa wafu, huanzia tumboni mwa mama kijana na hufunuliwa kwenye hori huko Bethlehemu. “Amani duniani,” Malaika huimba, wakitangaza uwepo wa Mungu asiye na ulinzi, ambaye ndani yake wanadamu wanaweza kujigundua kama wanapendwa tu kwa kumtunza (taz.Lk 2:13-14). Hakuna kitu chenye uwezo wa kutubadilisha kama mtoto. Labda ni mawazo ya watoto wetu na ya wengine ambao ni dhaifu sawa, ambayo hugusa moyo (taz. Matendo 2:37). Katika suala hili, mtangulizi wangu mtukufu aliandika kwamba “udhaifu wa binadamu una uwezo wa kutufanya tuwe na ufahamu zaidi kuhusu kile kinachodumu na kinachopita, kile kinacholeta uhai na kile kinachoua.

Kuna haja ya kusimamisha mbio za silaha na kuziondoka kabisa

Baba Mtakatifu anaandika kuwa labda kwa sababu hii, mara nyingi huwa tunakataa mapungufu yetu na kuepuka watu dhaifu na waliojeruhiwa: wana uwezo wa kuhoji mwelekeo tuliouchagua, kama watu binafsi na kama jamii.” Yohane XXIII alikuwa papa wa kwanza kutetea "upunguzaji wa silaha shirikishi," ambao unaweza kupatikana tu kupitia upya wa moyo na akili. Katika Waraka wa Pacem in Terris, aliandika: "Kila mtu lazima atambue kwamba, mchakato huu wa kupunguza silaha uweze kuwa kamili na timilifu, na kufikia roho za watu haiwezekani kama hakuna kusimamisha mbio za silaha, au kupunguza silaha, au na hili ndilo jambo kuu, hatimaye kuziondoa kabisa. Kila mtu lazima ashirikiane kwa dhati katika juhudi za kuondoa hofu na matarajio ya vita kutoka akilini mwetu. Lakini hii inahitaji kwamba kanuni za msingi ambazo amani inategemea katika ulimwengu wa leo zibadilishwe na nyingine tofauti kabisa, yaani, utambuzi kwamba amani ya kweli na ya kudumu miongoni mwa mataifa haiwezi kuwa na umiliki sawa wa silaha bali tu katika kuaminiana.

Vita vya kisiasa, kubariki utaifa na kuhalalisha vurugu

Na tuna uhakika kwamba hili linaweza kupatikana, kwani ni jambo ambalo si tu kwamba linaamriwa na akili ya kawaida, bali lenyewe ndilo linalotamanika zaidi na lenye matunda mazuri zaidi.” Huduma muhimu ambayo dini lazima zitoe kwa wanadamu wanaoteseka ni kujilinda dhidi ya jaribu linaloongezeka la kutumia hata mawazo na maneno kwa silaha. Tamaduni kubwa za kiroho, pamoja na sababu sahihi, zinatufundisha kutazama zaidi ya uhusiano wa damu au ukabila, zaidi ya vyama vinavyokubali wale tu walio sawa na kuwakataa wale walio tofauti. Leo, tunaona kwamba hili haliwezi kuchukuliwa kirahisi. Kwa bahati mbaya, imekuwa jambo la kawaida zaidi kuivuta lugha ya imani katika vita vya kisiasa, kubariki utaifa, na kuhalalisha vurugu na mapambano ya silaha kwa jina la dini.

Waamini lazima wakanushe kikamilifu, zaidi ya yote kwa ushuhuda wa maisha yao, aina hizi za kufuru zinazolikufuru jina takatifu la Mungu. Kwa hivyo, pamoja na vitendo, ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kukuza sala, hali ya kiroho, na mazungumzo ya kiekumene na ya kidini kama njia za amani na kama lugha za kukutana ndani ya mila na tamaduni. Ulimwenguni kote, inatarajiwa kwamba "kila jamii iwe 'nyumba ya amani,' ambapo mtu hujifunza jinsi ya kupunguza uadui kupitia mazungumzo, ambapo haki inatekelezwa na msamaha unathaminiwa." Sasa zaidi ya hapo awali, ni lazima tuoneshe kwamba amani si utopia kwa kukuza ubunifu wa kichungaji wenye umakini na uhai. Wakati huo huo, hii haipaswi kupunguza umuhimu wa upande wa kisiasa. Wale waliopewa jukumu kubwa zaidi la umma lazima "wafikirie kwa uzito tatizo la kufikia uhusiano zaidi wa kibinadamu kati ya Mataifa ulimwenguni kote. Marekebisho haya lazima yategemee uaminifu wa pande zote, ukweli katika mazungumzo na utimilifu wa uaminifu wa majukumu

Kukosekana kwa usawa wa madaraka duniani

Kila kipengele cha tatizo lazima kichunguzwe, ili hatimaye, hatua ya makubaliano itokee ambayo mikataba ya dhati, ya kudumu, na yenye manufaa inaweza kuanzishwa." Hii ni njia ya kuondoa silaha ya diplomasia, upatanishi na sheria za kimataifa, ambayo cha kusikitisha mara nyingi hudhoofishwa na ukiukwaji unaoongezeka wa mikataba iliyopatikana kwa shida, wakati ambapo kinachohitajika ni kuimarishwa kwa taasisi za kimataifa, sio ugawaji wao wa kisheria. Katika ulimwengu wa leo, haki na utu wa binadamu viko katika hatari kubwa katikati ya kukosekana kwa usawa wa madaraka duniani. Tunawezaje kuishi katika wakati huu wa kuyumba na migogoro, na kujikomboa kutokana na uovu? kuhimiza na kuunga mkono kila mpango wa kiroho, kitamaduni na kisiasa unaoweka matumaini hai, ukipinga kuenea kwa "maneno ya kifo, kana kwamba mienendo inayohusika ni matokeo ya nguvu au miundo isiyojulikana isiyo na utu inayojitegemea mapenzi ya mwanadamu."

Hakika Mungu atajibu na kutimiza ahadi zake

Kwa maana, kama ilivyopendekezwa, "njia bora ya kutawala na kupata udhibiti juu ya watu ni kueneza kukata tamaa na kujiuzulu, hata chini ya kivuli cha kutetea maadili fulani." Kinyume na mkakati huu, lazima tukuze kujitambua katika jamii za kiraia, aina za ushirika unaowajibika, uzoefu wa ushiriki usio wa vurugu, na mazoea ya haki ya kurejesha kwa kiwango kidogo na kikubwa.  Papa Leo XIII alikuwa tayari ameweka wazi hili katika Ensiklika yake Rerum Novarum: “Ufahamu wa udhaifu wake mwenyewe humsukuma mwanadamu kuomba msaada kutoka nje. Tunasoma katika Maandiko: ‘Wawili ni bora kuliko mmoja, maana wana faida kwa jamii yao. Kwa maana wakianguka, mmoja atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua’ (Mhubiri 4:9-10). Na zaidi: ‘Ndugu aliyesaidiwa na ndugu yake ni kama mji imara’ (Mithali 18:19).” Hili na liwe moja ya matunda ya Jubilei ya Matumaini, ambayo imewasukuma mamilioni ya watu kujigundua upya kama mahujaji na kuanza ndani yao wenyewe kuondoa moyo, akili na maisha. Hakika Mungu atajibu hili kwa kutimiza ahadi zake: “Atahukumu kati ya mataifa, atawaamulia watu wa kabila nyingi; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa, wala hawatajifunza vita tena. Enyi nyumba ya Yakobo, njooni, twende katika nuru ya Bwana” (Isa 2, 4-5).

Ujumbe wa Siku ya Amani 2026
18 Desemba 2025, 15:55