Tafuta

Mafungo ya Kiroho ya Papa Leo XIV na Curia Romana. Mafungo ya Kiroho ya Papa Leo XIV na Curia Romana.  (@Vatican Media)

Mafungo ya Kiroho:"Tumtukuze Mungu na mengineyo ni ya ziada"

Katika tafakari ya 10 ya Kwaresima kwa ajili ya Papa Leo XIV na Curia Romana,Ijumaa asubuhi,Februari 27,Askofu Erik Varden,Mtawa na Askofu wa Trondheim nchini Norway,aliendeleza sura ya Mtakatifu Bernard kuhusu kuzingatia na barua kwa Papa Eugenio III ambaye Mtakatifu alimwalika azungukwe na wahudumu wema,wanyofu,wapenda amani na umoja ili kuhakikisha utawala bora unaonufaisha Kanisa ulimwenguni.Tunachapisha mhutasari wa tafakari yake.

Vatican News.

Mtakatifu Bernard aliandika kitabu kilichojitolea kuhusu "Mazingatio." Kilikuwa kitabu kilichouzwa sana, kikisambazwa sana kuliko kazi zake zingine. Hili linaweza kuonekana kuwa la ajabu, kwa kuwa maandishi hayo kimsingi ni barua iliyotumwa  kwa mtu maalum katika nafasi ya kipekee. Bernard alikiandika kwa ajili ya Mtawa mwenzake, mtawa wa Italia anayeitwa Bernardo dei Paganelli, ambaye, tayari alikuwa Padre wa Kanisa la Pisa, na alijiunga Monasteri ya Clairvaux mwaka 1138 na mnamo 1145, Paganelli akachaguliwa kuwa  Papa Eugenio III. Tafakari ilishughulikia ukweli unaojulikana tayari. "Mazingatio"  hutafuta ukweli katika mambo ya kibinadamu yanayoweza kutegemewa, ambapo inaweza kuwa vigumu kutambua. Unaweza kufafanuliwa kama "mawazo yaliyojitolea kabisa, au mvutano wa roho, katika kutafuta ukweli." Kwa kuzingatia matatizo ya Kanisa, Bernard haitoi tiba za kitaasisi; badala yake, anamshauri Eugene azungukwe na watu wema: kadiri huduma kuu za Kanisa zinavyosimamiwa vyema, ndivyo faida itakavyokuwa kubwa kwa Kanisa ulimwenguni kote.

Washirika wenye uadilifu,walio tayari kutii na wenye subira

Sifa ambazo Bernard anamwomba atafute na kukuza ni halali wakati wote: wanahitajika washirika  "wenye uadilifu uliothibitishwa, walio tayari kutii, wenye subira na wapole; […] wa imani thabiti ya Kikatoliki, waaminifu katika huduma; wapenda maelewano, amani na umoja; […] wenye busara katika ushauri, […] werevu katika utawala, […], wanyenyekevu katika usemi." Watu kama hao "wanapenda na kufurahia sala na huweka tumaini lao ndani yake kuliko hekima au kazi zao wenyewe; kuingia kwao ni bila kelele, kuaga kwao bila fahari." Kwa kadiri Kanisa linavyofanya kazi kwa maneno haya, litaakisi mpangilio wa uongozi wa Malaika. Yeyote anayezingatia hilo ataona mara moja dhamira yake kuu: kumpatia Mungu utukufu.


"Mungu ni baraka kuu kwa upendo wake anatamani kushiriki umungu wake nasi"

Ili kuzingatia mahitaji ya kidunia kwa usahihi, ni lazima tutafute, kupitia hayo, yaliyo juu. Bernard anamwambia Eugene, kwa njia yoyote ile "kwenda uhamishoni: kufikiria kwa njia hii ni kurudi katika nchi ya mtu." Bernard aliuliza: Mungu ni nani? Utashi wa Mwenyezi, wema wa ukarimu, akili isiyobadilika. Mungu ni "baraka kuu" ambaye, kutokana na upendo, anatamani kushiriki umungu wake nasi. Alituumba ili tumtamani, anatupanua ili tumpokee, anatuhesabia haki ili tumstahili. Anatuongoza katika haki, anatuumba katika ukarimu, anatuangazia maarifa, anatuhifadhi kwa ajili ya kutokufa. Chochote kingine ambacho maaskofu wanapaswa kujishughulisha nacho, na kuna mengi, ukweli huu lazima uzingatiwe kwanza. Kwa njia hii, kuzingatia kwao mambo ya vitendo pia kutaangaziwa, kupangwa, kubarikiwa, na kuzaa matunda.

"Askofu lazima awe na kanuni, Mtakatifu na rafiki wa Bwana Harusi"

Askofu, kulingana na Bernard, lazima awe na kanuni, Mtakatifu, na mkaidi, lakini pia anapaswa kuwa rafiki wa Bwana harusi na kufurahia kushiriki urafiki huo na wengine. Mara nyingi Agostino   alielezea Shughuli ya  uaskofu kama (una sarcina, il fagotto del legionario)yaani kifurushi cha jeshi.  Ni taswira ya kikatili kiasi, iliyobuniwa na mtu anayefahamu ukiwa na hofu ya kufanya kampeni katika jangwa la Afrika Kaskazini. Hata hivyo, Agostino anaendelea kubuni mada aliyoiweka mwenyewe. Ingawa mzigo wa kichungaji unaonekana kutisha, unatisha tu ikiwa tutashindwa kutambua ni nani anayeweka mzigo mabegani mwetu. Kwa maana si kitu kingine ila kushiriki katika nira tamu ya Kristo mwenyewe, ambaye anatufanya tugundue kwamba msalaba tuliokabidhiwa unang'aa na mwepesi, na kwamba kuushiriki ni chanzo cha furaha. Perduc sarcinam tuam quia levis est si diligis gravis si odisti- yaani “Beba mzigo wako hadi mwisho”( dice Agostino in un sermone) yaani Agostino anasema katika mahubiri. “Ukiupenda, utakuwa mwepesi; ukiuchukia, utakuwa mzito,”( “Ee Yesu mwema,” aliandika Bernard katika kitabu chake cha” Maisha ya Mtakatifu Malakia wa Ireland: “yako, ni amana tuliyokabidhiwa; yako ni hazina iliyofichwa tuliyo nayo, itakayorudishwa utakapoipata tena.”

Mhutasari wa tafakari ya Askofu Erik Vardes:https://coramfratribus.com/life-illumined/on-consideration/#article

MAFUNGO YA PAPA 10

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

27 Februari 2026, 11:56