Mafungo ya Kiroho,Varden:Amani ya Kikristo,"sharti la jamii iliyobadilishwa"
Vatican News
Askofu Erik Varden, Mtawa wa Shirika la Cistercian, wa Jimbo la Trondheim, nchini Norway, alitoa tafakari yake ya kwanza ya Mafungo ya Kiroho ya Kwaresima kwa ajili ya Papa Leo XIV na Curia Romana yaliyofunguliwa alasiri, Dominika tarehe 22 Februari 2026, katika Kanisa la Paulina kwenye Jumba la Kitume, mjini Vatican, kwa mada: "Kuingia katika Kwaresima. Askofu alibainisha kwamba: "Amani ya Kikristo si ahadi ya maisha rahisi; ni sharti la jamii iliyobadilishwa."
Hasira, kikwazo kwa uwepo wa Roho ndani yetu
Mbele ya Papa Leo XIV, Makardinali wanaoishi Roma, na wakuu wa mabaraza ya Kipapa ya Curia Romana, Askofu wa Norway aliendeleza mada ya "Kuangazwa na Utukufu Uliofichwa, ambapo alisema kwamba, Kanisa "linaingiza amani katika programu yetu ya Kwaresima, na kwamba ni wakati wa kuelezea msimamo mkali wa amani ya Kikristo, mizizi yake katika zawadi ya haki na ujasiri ya nafsi, huku tukijikumbusha sisi wenyewe na wengine, ukweli wa maneno ya Mtakatifu Yohane Climaco kuwa: 'Hakuna kikwazo kikubwa zaidi kwa uwepo wa Roho ndani yetu kuliko hasira.'" Hii ni amani "ambayo ulimwengu hauwezi kutoa," na ambayo "inashuhudia uwepo wa Yesu ndani yetu kila wakati." Na Askofu huyo alikumbusha kwamba "uaminifu kwa mfano na amri za Kristo ni alama ya uhalisi wa Kikristo."
![]()
Wakati wa Tafakari ya Askofu Erik Varden (@Vatican Media)
Kwaresima inatuweka mbele ya mambo muhimu
Kwaresima,alielezea Askofu Varden, inatuweka katika mambo msingi. "Inatuleta kwenye nafasi ya kimwili na ya mfano iliyoachiliwa kutoka kwa yale yasiyo ya muhimu. Mambo yanayotukengeusha, hata yale mazuri, yanawekwa kando kwa muda." Ni wakati wa vita halisi vya kiroho, ambapo Kanisa "halipunguzi mwaliko wa kupambana dhidi ya maovu na tamaa mbaya: lugha yake ni 'Ndiyo, ndiyo,' 'Hapana, hapana,' si 'sasa hivi,' 'sasa hivi.'" Na unatupatia, mwanzoni mwa mapambano ya Kwaresima, "wimbo unaoleta amani, kama wimbo wa kipindi hiki." Ni "tractus," wimbo ambao ni mzito kwa zaidi ya miaka elfu moja ya liturujia ya Kiroma ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresima, unatumika kabla ya kusoma Injili ya majaribu ya Kristo jangwani.
![]()
Picha ya Kikanisa cha Paulina wakati wa Tafakari iliyoongozwa na Varden (@Vatican Media)
Mtakatifu Bernardo na wimbo Mkuu wa Zaburi ya 90
Wimbo ambao, mhubiri ameuchambua katika kutafakari kwake, "unarudia karibu maandishi yote ya Zaburi ya 90, wa Qui habitat." Mtakatifu Bernard, wakati wa Kwaresima ya 1139, aliongeza, alihubiri mfululizo wa mahubiri kumi na saba kuhusu Wimbo Mkuu wa Qui habitat kwa watawa wake. Katika kutafakari kwake, Askofu Vadren alielezea "maana ya kuishi katika neema tunapopambana na uovu, kutetea mema, kutetea ukweli, na kufuata njia ya kutoka utumwani kuelekea nchi ya ahadi, bila kupotoka kwenda kulia au kushoto, tukibaki na amani, tukijua kwamba chini ya kile ambacho wakati mwingine kinaweza kuonekana kama kutembea kwenye ukingo wa wembe 'kuna mikono ya milele.'" Kwa kifupi, anatualika kujitolea kwa shauku mpya "kwa ufuasi uliojaa upendo na uwazi," alihitimisha.
Tafakari zijazo hadi tarehe 27 Februari
Kama ilivyokuwa imepangwa, baada ya tafakari ya kwanza Dominika 22 Febrari, na kuanzia Jumatatu tarehe 23 hadi Februari 27, kutakuwa na tafakari mbili ya: saa 3:00 asubuhi, baada ya masifu na saa 11:00 jioni, kwa kuabudu Ekaristi na Masifu ya jioni. Baada ya tafakari ya kwanza ya Dominika, mbili zaidi zimepangwa kufanyika kuhusu Mtakatifu Bernard: "Mtaalamu wa Mawazo, " asubuhi ya tarehe 23 Februari na "Mtakatifu Bernard Mtaalamu wa Ukweli" alasiri ya tarehe 26 Februari. Mada zingine zinahusu msaada wa Mungu; kuwa huru; fahari ya ukweli; elfu wataanguka; "Nitamtukuza"; malaika wa Mungu;juu ya kuzingatia, na kumalizia na tafakari ya mwisho kuhusu "Kuwasilisha Tumaini."
![]()
Askofu Varden (wa kwanza kulia)wakati wa masifu ya jioni kabla ya tafakari.(@Vatican Media)
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
