Mafungo ya kiroho:Uongofu wa kushangaza na haki ya huruma ya Mungu!
Na Angella Rwezaula - Vatican.
Askofu Erik Varden, Mtawa wa Shirika la Cistercian na Askofu wa Jimbo la Trondheim, nchini Norway, katika tafakari yake pili ya Mafungo ya Kiroho ya Kwaresima kwa Papa Leo XIV na Washirika wake wa karibu wa Curia Romana iliyofanyika asubuhi tarehe 23 Februari 2026, katika Kanisa la Paulina, mjini Vatican. Mada ya tafakari ya kwanza ya asubuhi ilijikita na: "Mtakatifu Bernard, Mtaalamu wa Mawazo," ambapo alibainisha kwamba: "Mafundisho ya Mtakatifu Bernard wa Clairvaux kuhusu uongofu yanatokana na "mapambano ya kibinafsi na kujifunza kutochukulia kirahisi, kwamba njia ya mtu huwa ndiyo sahihi kila wakati, ikifundishwa kutokana na uzoefu, majeraha na changamoto za kuhoji dhana ya mtu na kushangazwa na haki ya huruma ya Mungu."
Askofu Varden alifafanua kuwa Bernard, ni "msaidizi bora kwa yeyote anayefanya safari ya Kwaresima kutoka katika ubinafsi na kiburi katika hamu ya kufuata ukweli wa nafsi huku akiweka mtazamo wake kwenye upendo wa Mungu unaoakisi yote."Hapa unaweza kupata tafakari nzima ya Askofu Varden: (Qui la sintesi integrale della meditazione di monsignor Varden.
![]()
Papa Leone XIV ascolta la meditazione di monsignor Varden (@Vatican Media)
Shirika la Cistercian:Ubunifu na mageuzi
Askofu Mcistercian alifafanua kwamba, Bernard alijitokeza katika harakati za karne ya XII kwa karama yake kubwa na uwezo wake wa kufanya kazi, lakini hakuwa mwanzilishi wa Shirika hilo: Yeye alifika katika Abasia ya Cîteaux mnamo mwaka 1113, akiwa na umri wa miaka 23, akiwa na kundi la wenzake thelathini. Shirika la Cîteaux, lililoanzishwa mnamo 1098 na Mmonaki Mbenediktini, Robert de Molesme, "ilikuwa uvumbuzi na mageuzi," alikumbusha Askofu Varden. Waanzilishi waliita nyumba yao Monasteri mpya(novum monasterium) Mpango, alifafanua, ambao "haukuwa kimsingi mmenyuko dhidi ya kitu au mtu na tunamshukuru Mungu kwa hilo, kwa sababu mipngo mingine ya upinzani mapema au baadaye hupotea."
Bernard: mnyenyekevu, mkarimu, na rafiki mwaminifu
Akiwa na ujasiri katika uamuzi wake mwenyewe, Bernard mara nyingi alikuwa mnyumbulifu "katika kufuata taratibu fulani ambazo vinginevyo alidai kuzifuata," lakini maono yake kuhusu mahitaji ya Kanisa "wakati mwingine yalimsukuma kuchukua misimamo mikali," akiwa na "roho kali ya upendeleo." Lakini, mhubiri huyo alisisitiza, kuwa "hakuwa mnafiki." Badala yake, alikuwa "mnyenyekevu wa kweli, aliyejitolea kwa Mungu, mwenye uwezo wa wema mwororo, rafiki mwaminifu, awezaye kuwa rafiki wa maadui wa zamani, na shahidi mwenye nguvu ya upendo wa Mungu. Alikuwa, na bado, mtu wa kuvutia."
![]()
Tafakari ya Askofu Erik Varden, Mmnonaki na Askofu wa Norway(@Vatican Media)”.
Mtakatifu Bernard na Thomas Merton
Baadaye Askofu huyo alibainisha juu ya "kufanana kwa tabia" kati ya Bernard wa Clairvaux na Thomas Merton, mwandishi wa Marekani na Mtawa wa Kitrappist ambaye alijitoa hasa kwa mada za Uekumeni, mazungumzo kati ya dini, amani, na haki za kiraia. Kwa Askofu Varden, Bernard hakupata "umeme" wa akili wa Merton, kama alivyouita Dom James Fox, Abate wa Gethsemani, huko Kentucky, "lakini pia ulikuwa asili isiyobadilika ambayo ilikuwa na ilibidi isawazishe mivutano mikubwa." "Merton alimkasirisha Fox kwa mawazo yake, maono yake, na msisitizo wake," mhubiri alielezea, "lakini Fox alijua kwamba Merton alikuwa mkweli." Alihitimisha kwamba mafundisho ya Bernard kuhusu uongofu "yanatokana na utamaduni wa kibiblia usio na kifani na dhana za kitaalimungu zilizofikiriwa vizuri."
Tafakari mpya alasiri 23 hadi Februari 27
Askofu Varden atajikita na: "Mtakatifu Bernard wa Mawazo"na alasiri Februari 26. Jioni saa 11.00, mada ya tafakari itakuwa: "Msaada wa Mungu." Kutakuwa na tafakari mbili hadi Februari 27: saa 3:00 asubuhi, ikitanguliwa na Masifu, na saa 11:00 jioni, Ibada ya Ekaristi na kuabudu. Mada zingine ni pamoja: kuwa huru; fahari ya ukweli; elfu moja wataanguka; "Nitamtukuza;" malaika wa Mungu; na kuzingatia, kumalizia na tafakari ya mwisho inayozingatia "Kuwasilisha Tumaini."
![]()
Papa Leo na wahudumu wake wa karibu wa Curia Romana wakifutilia tafakari za Mafungo kutoka kwa Askofu Varden(@Vatican Media).
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
