Tafuta

 "Kiukweli,kila vita ni jeraha linalosababisha familia nzima ya wanadamu kupata kifo,uharibifu na maumivu yanayoumiza vizazi." "Kiukweli,kila vita ni jeraha linalosababisha familia nzima ya wanadamu kupata kifo,uharibifu na maumivu yanayoumiza vizazi."  (ANSA)

Papa Leo XIV:Amani ni hitaji la dharura,libadilishwe kuwa maamuzi yenye uwajibikaji

Mara baada ya sala ya Malaika wa Bwana,Papa Leo XIV,alirudia wito kwa nguvu kuwa silaha zinyamazishwe na mabomu yasitishwe."Na usitishaji mapigano ufikiwe bila kuchelewa na mazungumzo yaimarishwe,"Papa alisema,ni miaka minne baada ya kuanza kwavita dhidi ya Ukraine.Amani haiwezi kuahirishwa, alisisitiza:"Kiukweli,kila vita ni jeraha lililokumba familia nzima ya wanadamu;huacha nyuma kifo,uharibifu,na maumivu ambayo yanaumiza vizazi."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 22 Februari 2026, Baba Mtakatifu akiwageukia waamini wengi waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro Mjiuni Vatican, alitoa wito wa nguvu kuhusiana na vita vinavyoendelea ulimwenguni kote. Papa alisema "Miaka minne sasa imepita tangu kuanza kwa vita dhidi ya Ukraine. Moyo wangu bado unaomboleza hali hiyo kubwa mbele ya macho ya kila mtu: Je, ni waathiriwa wangapi, ni maisha na familia ngapi zilizovunjika, ni uharibifu kiasi gani, ni mateso kiasi gani yasiyoelezeka! Kwa kweli, kila vita ni jeraha lililosababishwa kwa familia nzima ya wanadamu: huacha nyuma kifo, uharibifu, na mkondo wa maumivu unaowaumiza vizazi. Amani haiwezi kuahirishwa: ni hitaji la dharura, ambalo lazima lipate nafasi mioyoni na kutafsiriwa kuwa maamuzi yenye uwajibikaji."

Wito wa kusitisha mapigano

kwa kuopngeza Papa alisisitiza "Kwa sababu hiyo, ninarudia wito wangu kwa nguvu: silaha ziwe kimya, mabomu yaache yasimame, kusitisha mapigano kufikiwe bila kuchelewa, na mazungumzo yaimarishwe ili kufungua njia ya amani. Ninawaalika kila mtu kujiunga katika maombi kwa ajili ya watu wa Ukraine wanaoteseka na kwa ajili ya wote wanaoteseka kwa sababu ya vita hivi na kila mgogoro duniani, ili zawadi ya amani iliyosubiriwa kwa muda mrefu iangaze siku zetu."

Salamu kwa mahujaji

Kwa kugeukia umati huo mkubwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, papa alisema "Na sasa ninawasalimu nyote, waamini wa Roma na mahujaji kutoka Italia na nchi mbalimbali. Ninawabariki kwa moyo mkunjufu Masista Wafanyakazi wa Yesu katika kumbukumbu ya miaka mia moja ya kuanzishwa kwa Taasisi yao. Ninawasalimu Shule ya Mtakatifu Yosefu Calasanz huko Prievidza, Slovakia; na ninawatia moyo vyama vilivyojitolea kushughulikia magonjwa adimu pamoja."

Bado Papa aliendelea na salamu zake: "Ninawasalimu kundi la Utume wa Maombi la Biella, waamini wa Nicosia, Castelfranco Veneto, na Dekania ya Melegnano; walipata kipaimara wa Boltiere, watoto wa Jumuiya ya Wachungaji ya Mtakatifu Maria Maddalena huko Milano, na Skauti wa Tarquinia." Na hatimaye aliwatakia "Dominika Njema na safari njema ya Kwaresima."

Mara baada ya sala

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

22 Februari 2026, 13:14