Tafuta

Papa Leo XIV kwa Parokia ya Moyo Mtakatifu:”kuwa mwali wa mwanga

Papa Leo XIV akiwa katika ziara ya Kichungaji katika Parokia ya Moyo Mtakatifu ,Roma,Februari 22 katika mahubiri:"Wanadamu wako huru kutambua na kukumbatia utofauti wa Muumba,ambaye anatambua na kukumbatia utofauti wa viumbe."Parokia yao imeitwa kuchukua jukumu la uhalisia,kuwa chachu ya Injili katika jamii ya wenyeji,kuwa ishara ya ukaribu na upendo.Na aliwashukuru Wasalesiani kwa kazi isiyochoka na kuhimiza kuendelea kuwa mwali wa mwanga wa matumaini.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV, alitimiza ziara yake ya Pili ya Kichungaji kati ya Tano ambazo anatarajia kuzitimiza kuelekea Pasaka ya Bwana, katika Jimbo lake Kuu Roma, Dominika tarehe 22 Februari 2026 katika Parokia ya Basilika ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, mita chache nyuma ya Kituo kikubwa cha Usafiri wa Treni, Termini - Roma. Baada ya Makaribisho kwenye Ua wa Basilika na Maneno yake ya kwanza  kwanza, Baba Mtakatifu alianza misa saa 3.00 kamili ambapo baada ya masomo na Injili alianza tafakari yake. "Siku chache zilizopita, kwa ibada ya Jumatano ya Majivu, tulianza safari yetu ya Kwaresima. Kwaresima ni msimu mkali wa kiliturujia, unaotupatia fursa ya kugundua upya utajiri wa Ubatizo wetu, kuishi kama viumbe vilivyofanywa upya kikamilifu kutokana na Umwilisho, kifo, na Ufufuko wa Yesu. Somo la Kwanza na Injili, ambayo tumesikia hivi punde, katika mazungumzo kati yetu, hutusaidia kugundua upya zawadi ya Ubatizo kama neema inayokumbatia uhuru wetu.

Mahubiri ya Papa
Mahubiri ya Papa   (@Vatican Media)

Papa Leo aliendelea kusema kuwa "Simulizi la Mwanzo linaturudisha katika hali yetu kama viumbe, ambavyo havijaribiwi sana na katazo, kama inavyoaminika mara nyingi, bali na uwezekano: uwezekano wa uhusiano. Kwa hivyo wanadamu wako huru kutambua na kukumbatia utofauti wa Muumba, " anatambua na kukumbatia utofauti wa viumbe. Ili kuzuia uwezekano huo, nyoka anaashiria dhana kwamba anaweza kufuta tofauti zote kati ya viumbe na Muumba, akiwashawishi mwanamume na mwanamke kwa udanganyifu wa kuwa kama Mungu. Shetani anawasukuma kumiliki kitu ambacho, kama anavyosema, Mungu anataka kuwakataa, ili kuwaweka daima katika hali ya kuwapunguza thamani. Picha hii kutoka Mwanzo ni kazi bora isiyopitwa na kitu inayowakilisha mchezo wa kuigiza wa uhuru.

Waamini katika basilika
Waamini katika basilika   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu akijikita na Injili alisema " Injili inaonekana kujibu tatizo la zamani: je, ninaweza kutambua maisha yangu kikamilifu kwa kusema "ndiyo" kwa Mungu? Au, ili kuwa huru na mwenye furaha, ni lazima nijikomboe kutoka Kwake? Mandhari ya majaribu ya Kristo hatimaye yanashughulikia swali hili la kusisimua. " Inatuongoza kugundua ubinadamu wa kweli wa Yesu ambaye, kama Katiba ya Mtaguso Gaudium et Spes inavyofundisha, inamfunulia mwanadamu mwenyewe: "Katika fumbo la Neno Aliyefanyika Mwili, fumbo la mwanadamu linaonekana wazi kweli" (GS, 22). Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa hakika, tunamwona Mwana wa Mungu ambaye, akipinga mitego ya Adui wa kale, anatuonesha mtu mpya, mtu huru, ufunuo wa uhuru unaotokana na kusema "ndiyo" kwa Mungu. Ubinadamu huu mpya huzaliwa kutoka kwenye kisima cha ubatizo. Na kwa hivyo, hasa katika Kipindi hiki cha Kwaresima, tunaitwa kugundua upya neema ya Ubatizo, kama chanzo cha uzima kinachokaa ndani yetu na kinachotusindikiza kwa nguvu kwa heshima kubwa kwa uhuru wetu.

Misa ya Papa
Misa ya Papa   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV kadhalika alisisitiza kuwa kwanza kabisa, Sakramenti yenyewe ina nguvu, kwa sababu kile inachotoa hakizuiliwi na nafasi na wakati wa ibada, bali ni neema inayoambatana na maisha yetu yote kila wakati, ikidumisha ufuasi wetu wa Kristo. Lakini Ubatizo pia una nguvu kwa sababu unatuweka katika safari mpya kila mara, kwani neema ni sauti ya ndani inayotuhimiza kufuata Yesu, ikitukomboa uhuru wetu ili upate utimilifu katika upendo wa Mungu na jirani. Kwa hivyo tunaelewa asili ya uhusiano wa Ubatizo, ambayo inatuita kuishi katika urafiki na Yesu na, hivyo, kuingia katika ushirika wake na Baba. Uhusiano huu uliojaa neema pia unatuwezesha kupata uzoefu wa ukaribu wa kweli na wengine, uhuru ambao, tofauti na kile ambacho shetani anapendekeza kwa Yesu, sio kutafuta nguvu za mtu mwenyewe, bali ni upendo wa kujitoa unaotufanya sote kuwa kaka  na dada. Hakika, Mtakatifu Paulo anasema: "Hakuna Myahudi wala Mgiriki, hakuna mtumwa wala huru, hakuna mwanamume wala mwanamke; kwa maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu" (Gal 3:28).

Misa katika Basilika ya Moyo Mtakatifu wa Yesu
Misa katika Basilika ya Moyo Mtakatifu wa Yesu   (@Vatican Media)

Papa aliendelea kudaduvua  katika mahubiri kwa waamini kwamba Papa Leo XIII alimwomba Mtakatifu Yohane Bosco kujenga Kanisa walilokuwamo siku hiyo: "Alikuwa ameelewa umuhimu wa mahali hapa, karibu na Kituo cha Termini na katika makutano ya kipekee ya jiji, yaliyokusudiwa kuwa muhimu zaidi baada ya muda." Kwa sababu hii, marafiki hao wapendwa, Papa alisisitiza katika kukutana nao siku hiyo “naona ndani yenu uwepo maalum wa ukaribu, yaani mbele ya changamoto za eneo hili. Hakika, kuna wanafunzi wengi vijana wa chuo kikuu hapa, wasafiri wanaokuja na kwenda kazini, Wahamiaji wanaotafuta ajira; wakimbizi vijana ambao, kutokana na mpango wa Wasalesiani, wamepata fursa ya kukutana na wenzao wa Italia na kutekeleza mipango ya ujumuishaji katika makao makuu yaliyo karibu; na kisha kuna kaka na dada zetu ambao hawana makazi na hupata makazi katika vituo vya Caritas kwenye Via Marsala," papa alisisitiza.

Papa akibariki
Papa akibariki   (@Vatican Media)

Katika mita chache tu, mtu anaweza kugusa utata wa wakati wetu: mtazamo wa kutojali wa wale wanaoondoka na kufika na starehe zote, na wale ambao hawana paa; uwezekano mwingi wa mema na vurugu zilizoenea; hamu ya kufanya kazi kwa uaminifu na biashara haramu ya dawa za kulevya na ukahaba. Parokia yao  imeitwa kuchukua jukumu la uhalisia huu, kuwa chachu ya Injili katika jamii ya wenyeji, kuwa ishara ya ukaribu na upendo. Papa amewashukuru Wasalesiani  kwa kazi isiyochoka wanayofanya kila siku, na anawahimiza kila mtu kuendelea kuwa mwali mdogo wa mwanga na tumaini hapa hapa. Ameomba Maria Msaada wa Wakristo atusaidie kila wakati katika safari yetu, akitufanya tuwe imara wakati wa majaribu, ili tupate uzoefu kamili wa uhuru na udugu wa watoto wa Mungu."

Il Papa e, sullo sfondo, la stazione di Roma Termini

Maneno haya yanahusiana na yale ya Papa, ambaye aliwaalika jumuiya kuwa "chachu ya Injili katika unga wa eneo hilo." Misa iliadhimishwa, miongoni mwa wengine waliokuwapo ni Kardinali Baldo Reina, mMakamu wa Papa Jimbo Kuu la  Roma; na Kardinali Giuseppe Versaldi, mkuu mstaafu wa Baraza la Kipapa la Elimu ya Katoliki; Gambera wa Wasalesia, Padre Fabio Attard; na mkuu wa Wasalesiani  Italia ya Kati, Padre Roberto Colameo; na  Padre Javier Ortiz Rodriguez wa Parokia. Na ni wa mwisho aliyemhutubia Papa, akimpatia Picha ya Mchungaji Mwema na  kumshukuru kwa ziara yake ya kichungaji, ambayo, anatumaini, itakuwa dawa ya "majeraha ya kijamii" yanayoathiri ujirani, lakini pia "kuanzisha upya mpango wa kichungaji ambao ni kama treni ya mwendo kasi iliyojaa amani, matumaini, na kujitolea kwa Kikristo kujenga jumuiya, na kuwafikia kila mtu.

MISA PAROKIA YA M.M. WA YESU

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

22 Februari 2026, 11:31