Tafuta

2026.02.22 Papa akutana na watoto katika ziara yake ya kichungaji ya Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu. 2026.02.22 Papa akutana na watoto katika ziara yake ya kichungaji ya Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Tunaishi historia si ya zamani tu,bali tunaandika historia ya upendo!

Asanteni kwa ukaribisho wenu na furaha hii,ambayo,ikiwa ni siku ya Bwana,Dominika,inakumbusha siku ya Ufufuko,furaha ya tumaini letu.Na ingawa Dominika ya kwanza ya Kwaresima ni wakati wa maandalizi,wa uongofu,huu pia ni wakati wa furaha,kwa sababu sote tunajua kwamba Bwana anataka kutupokea,anataka kutukaribisha, kama Parokia hii!Ni maneno ya joto ya Papa Leo XIV kwa waamini wa Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu,Roma kabla ya Misa Takatifu Dominika Februari 22.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ukarimu wa kukaribishwa huyeyusha itifaki baridi ya kutojali kwa juu juu inayopenya mifupa na moyo. Kwa hivyo, wakati wa ziara ya Kichungaji  katika parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Castro Pretorio mnamo tarehe 19  Januari 2014, Papa Francisko alielezea ukaribu wa busara na ujasiri unaoweza kupita hata hofu halali, ya jumuiya katikati ya Roma ambayo kila siku huwafikia wale wanaoishi kwenye "pembezoni"mwa  kituo kikubwa, cha Rome Termini, ambacho huwaahidi kuondoka lakini huzuia matamanio yao. Tarehe 22 Februari 2026  Papa Leo XIV aliwasili katika Parokia hiyo hiyo tena  kwa ziara ya pili kati ya tano za kichungaji ambazo Papa mwenyewe atazitimiza kwa Jumuiya za Parokia za Jimbo lake kuelekea Pasaka ya Bwana.

Papa akiwasalimia waamini
Papa akiwasalimia waamini   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XIV aliwasili baada kidogo ya saa 2.15 asubuhi na kuwasalimia waamini nje ya Kanisa kabla ya kuanza misa  takatifu saa 3.00 asubuhi. Papa alianza kusema kuwa “ Habari za asubuhi na Dominika  njema nyote! Habari za asubuhi! Ni kwa jinsi gani ilivyo nzuri!  Na asanteni kwa ukaribisho wenu na furaha hii, ambayo, ikiwa ni siku ya Bwana, Dominika, inakumbusha siku ya Ufufuko, furaha ya tumaini letu. Na ingawa Dominika ya kwanza ya Kwaresima ni wakati wa maandalizi, wa uongofu, huu pia ni wakati wa furaha, kwa sababu sote tunajua kwamba Bwana anataka kutupokea, anataka kutukaribisha, kama Parokia hii! Ni vizuri sana kuwa mahali ambapo kila mtu anakaribishwa! Asante, asanteni kwa parokia hii! Jina lenyewe: "Moyo wa Yesu," "Moyo Mtakatifu,” linatukumbusha maana ya ishara ya moyo kwetu: ishara ya upendo, hisani,  ya ukarimu huu usio na kikomo wa upendo wa Bwana.

Papa akitoa salamu kabla ya misa
Papa akitoa salamu kabla ya misa   (@Vatican Media)

Na asubuhi hii tunawaona watu kutoka nchi nyingi duniani kote, wote wamekusanyika hapa, wakiwakilisha umoja huu, ushirika, na udugu, kuishi pamoja, ambako Yesu pekee ndiye anayeweza kuwawezesha. Ni upendo wa Yesu, ni huruma yake ndiyo iliyotuita pamoja asubuhi ya leo. Na kwa hivyo mimi pia ninasema: "Asante, Bwana, asante, na karibu kwenye sherehe hii!"

Salamu kwa waamini
Salamu kwa waamini   (@Vatican Media)

Papa alisema tena "Pia ninawasalimu jumuiya ya Wasalesian na Masista Wasalesian waliopo hapa. Hebu tufikirie kuhusu historia ya Parokia hii, tukianza na Don Bosco, pamoja na Wasalesiani, na mtangulizi wangu, ambaye pia aliitwa Leo, Leo XIII. Tunaishi historia ambayo si ya zamani tu. Leo tunaandika historia kwa sababu bado tunataka kuishi kwa kutimiza utamaduni huu mzuri wa huduma, upendo, na kufanya kazi na vijana. Ni vizuri sana kuwaona watoto hawa wote hapa! Tuwapigie makofi kwao! Hebu tupate uzoefu wa furaha ya maisha: jinsi gani ilivyo nzuri kuwa hai, kuwa na zawadi hii ya maisha ambayo Bwana anatupatia. Matashi  mema! Dominika njema."Papa alisisitiza.

La stazione Termini e la statua di san Giovanni Paolo II

Kituo cha Termini kuna sanamu kubwa ya Mtakatifu Yohane Paulo II

Hewa baridi inaumiza asubuhi. Kwenye Njia ya Marsala, ukumbi mkubwa unaoelekea kituo umezuiwa, lakini mtiririko wa waamini ulimiminika kwa wingi, ukijaza ua mbele ya Kanisa kuu. Bango la Njano  na nyeupe, rangi za bendera ya Jiji la Vatican, limetundikwa hapa, likisomeka: "Karibu Papa Leo XIV." Likiwa limezungukwa na jopo linalomuonesha Papa mwenyewe mbele na Mtakatifu Yohane Bosco nyuma.

Lo striscione per il Papa

Bango kwa ajili ya Papa: Mtazamo wa kwanza wa waamini unaonesha kuunganishwa kwa "vipingamizi" vilivyopo 

Volontarie del "Banco dei talenti"

Wapo watawa kutoka makundi matatu ya Mashirika wanaohudhuria jumuiya ya parokia mara kwa mara: Binti za Maria Msaada wa Wakristo, Wamisionari Masikini wa Mtakatifu Clara  wa Sakramenti Takatifu, na Wamisionari wa Kristo Aliyefufuka.

Religiose salesiane provenienti dalle Filippine

Watawa Wasalesiani kutoka Ufilippini

Un bambino nel suo giaccone attende l'arrivo del Papa

Watoto wakiwa anamsubiri Papa Leo XIV

Il Papa benedice una futura coppia di sposi

Papa akiwabariki wanandoa wajao (@Vatican Media)

Kibao kimeandikwa: tutaoana je unaweza kutubariki?"

Il Papa tra i bambini della parrocchia

Papa miongoni mwa watoto wa Parokia (@Vatican Media)

Kulikuwa na watoto wa darasa la Pili wa Katekesimu.

Il Papa fa il suo ingresso in basilica

Papa aliingia katika Kanisa Kuu (@Vatican Media)

Hasa katika msimu huu wa Kwaresima, tunaitwa kugundua upya neema ya Ubatizo, kama chanzo cha uzima kinachokaa ndani yetu na kinachotusindikiza kwa heshima kubwa kwa uhuru wetu.

Il Papa e, sullo sfondo, la stazione di Roma Termini

Papa na, nyuma, Kituo cha Treni cha Termini cha Roma (@Vatican Media)

Kiukweli, kuna wanafunzi wengi vijana wa vyuo vikuu, wasafiri wanaokuja na kwenda kwa kazi, wahamiaji wanaotafuta ajira, na wakimbizi vijana ambao wamejikuta katika jengo lililo karibu, kutokana na mpango wa Wasalesiani, fursa ya kukutana na wenzao wa Italia na kutekeleza mipango ya ujumuishaji.

Il Papa saluta i parrocchiani

Papa akiwasalimia wanaparokia (@Vatican Media)

Baada ya misia Papa Leo alikwenda kwenye Kikanisa kidogo na kukutana na Jumuiya ya Wasalesiani na Baraza la Kichungaji kabla ya kurudi Vatican

Il caricabatterie in basilica

Chaja kwenye basilika: Chaja haipo tena. Mtu aliifungua na kuiweka mfukoni mwake. "Nipigie simu baada ya miaka ishirini," aliimba Lucio Dalla. Mtu, huyo  leo, tayari amepiga namba ya simu  hiyo.

SALAMU PAROKIA YA M.M.WA YESU

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

22 Februari 2026, 10:51