Papa Leo XVI:"Mwenendo wenu na uwe kama inavyopaswa Injili ya Kristo"
Vatican News.
Baba Mtakatifu Leo XIV Ijumaa jioni tarehe 27 Februari 2026, mara baada ya Mafungo ya kiroho alipendelea kutoa shukrani zake kwa Askofu Erik Varden, Mtawa na Askofu wa Trondheim nchini Norway, aliyewaongoza katika tafakari hii ya Kipindi cha Kwaresima kuanzia Dominika jioni tarehe 22 Februari. Baba Mtakatifu alisema kuwa “Kabla ya kuhitimisha Juma hili la mafungo ya kiroho na mapumziko, nina furaha, wakati wa baraka hii kuweza kumshukuru mhubiri wetu, ambaye alitusindikiza na kutusaidia katika siku hizi kuishi uzoefu wa kina na wa kiroho, sehemu muhimu sana ya safari yetu ya Kwaresima, kuanzia Dominika na "Majaribu," na kutafakari mfano na ushuhuda wa Mtakatifu Bernard, maisha ya kitawa, na vipengele vingine vingi katika maisha ya Kanisa.”
“Lazima nikubali, Papa aliongeza “ kwamba mimi binafsi nilijikuta nimevutiwa sana na kutafakari wakati fulani. Kwa mfano, asubuhi ya leo, alipozungumzia kuchaguliwa kwa Papa Eugene III na Mtakatifu Bernard, alisema: "Umefanya nini? Mungu akurehemu." Kisha Kanisa hili, nitawambia kulihusu, tarehe 8 Mei, tulipokuwa tumekusanyika hapa kwa ajili ya Maadhimisho ya Misa. Hapo juu kuna maandishi kutoka kwa Barua ya Mtakatifu Paulo kwa Wafilipi, ambayo yanasomeka: "Kwa maana kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida." Papa alisisitiza kuwa “Kwa hivyo, katika muktadha huu na kwa roho hii ya ushirika, sote tumekusanyika pamoja, lakini wakati mwingine tofauti sana, na kukusanyika pamoja katika sala pia, nadhani, ni wakati muhimu sana katika maisha yetu, tukitafakari masuala mengi ambayo ni muhimu kwa maisha yetu na kwa Kanisa.”
Na sina nia ya kupitia Juma zima, bali baadhi ya vipengele ambavyo nakubaliana navyo. Kwa mfano, marejeo ya Mwalimu wa Kanisa John Henry Newman na shairi "Ndoto ya Gerontius," ambapo Newman anatumia kifo na hukumu ya Gerontius kama mwonekano ambao msomaji anaongozwa kutafakari hofu yake ya kifo na hisia yake ya kutostahili mbele za Mungu.” Papa alisisitiza kuwa “Kuna vipengele vingine, kama vile uhuru na ukweli, ambavyo ni muhimu sana katika maisha yetu. Na katika haya yote, jioni hii, nikiwa na tafakari yangu juu ya tumaini na chanzo cha kweli cha tumaini, ambacho ni Kristo, nilirudi kusoma tena Barua kwa Wafilipi.”
Katika mwendelezo wa maandishi yaliyoandikwa hapo juu, ambapo Paulo anasema: "Lakini ikiwa kuishi katika mwili kunamaanisha kazi yenye matunda, sijui nichague lipi. Kwa maana nimepasuka kati ya hivi viwili: Natamani kuondoka duniani nikae na Kristo, jambo ambalo lingekuwa bora zaidi, lakini kwa ajili yenu ni muhimu zaidi nibaki katika mwili. Nikiwa nimeshawishika na hili, najua ya kuwa nitakaa na kuendelea kubaki kati yenu nyote kwa ajili ya maendeleo yenu na furaha katika imani.”
Papa Leo XIV aidha aliongeza “Kisha anasema: “Kwa hiyo, enendeni kwa jinsi inavyostahili Injili ya Kristo.” Tazama: huu ndio mwaliko mwishoni mwa siku hizi za maombi na tafakari, ambazo Neno la Mungu lenyewe linatuambia sote: “Kwa hiyo, enendeni kwa jinsi inavyostahili Injili ya Kristo.” Papa Leo hakuishia hapo bali pia lisema “Kwa niaba ya wote waliopo, basi, ninakushukuru, Askofu Varden, kwa yote uliyotupatia siku hizi. Hekima yako, ushuhuda wako huu na maisha ya kitawa ya Mtakatifu Bernard, utajiri wa tafakari zako, zitabaki kuwa chanzo cha baraka kwetu, cha neema, cha kukutana na Yesu Kristo kwa muda mrefu.”
Shukrani kwa Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia
Kadhalika Papa alitoa shukurani kwa “Pia ningependa, kwa wakati huu, kuwashukuru washirika wa Ofisi ya Maadhimisho ya Liturujia walioandaa vifaa vyote vya sala yetu, pamoja na kwaya, ambayo naamini bado ipo. Asante kwa kutusaidia na muziki, ambao pia ni muhimu sana katika sala yetu.
Muziki unatusaidia kuinua roho zetu kwa Bwana kuliko maneno yetu ambayo hayawezi
Muziki naamini Askofu Varden amesema haya wakati fulani, unatusaidia kuinua roho zetu kwa Bwana zaidi ya maneno ambayo hayawezi,” Kwa kuhitimisha Papa alirudia kutoa tena shukrani nyingi na kwa wote kwa uwepo wao na ushiriki katika siku hizi” na akahitimisha kwa kutoa Baraka yake. “ Jioni njema na Asanteni nyote.”
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
