Tafuta

2026.03.30 Paolo Rudelli, Petar Rajič, Edgar Peña Parra 2026.03.30 Paolo Rudelli, Petar Rajič, Edgar Peña Parra 

Papa afanya uteuzi wa Mabalozi na Mkuu wa Nyumba ya kipapa

Papa amefanya uteuzi wa mabalozi wa Vatican:Aliyekuwa Balozi wa Vatican nchini Colombia,Askofu Mkuu Paolo Rudelli,ameteuliwa kuwa Katibu Msaizidi wa Vatican wa Masuala ya Jumla akichukua nafasi ya Askofu Mkuu Edgar Peña Parra ambaye ametuliwa kuwa Balozi wa Vatican nchini Italia na Jamhuri ya San Marino,akimrithi Askofu Mkuu Petar Rajič ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Nyumba ya Kipapa.

Na Salvatore Cernuzio – Vatican.

Kuanzia Colombia hadi Sekretarieti ya Vatican; kuanzia Sekretarieti ya Vatican hadi Ubalozi wa Vatican nchini Italia, kuanzia Ubalozi nchini Italia hadi Mkuu wa Nyumba ya Kipapa. Ni mizunguko ya uteuzi ndani ya Kiti Kitakatifu ambazo zimechapishwa tarehe 30  Machi 2026.  Papa Leo XIV amemteua Naibu mpya wa Masuala ya Jumla wa Sekretarieti ya Vatican, moja ya nafasi muhimu na nyeti katika vyombo vyote vya Vatican, yaani kijamii ni aina ya "Waziri wa Mambo ya Ndani" wa Jiji la Vatican. Huyu ni Askofu Mkuu Paolo Rudelli, mwenye umeri wa miaka 56 Julai ijayo, na Padre  tangu 1995, aliyewekwa wakfu huko Bergamo na mwenye shahada ya Taalimungu ya maadili, hadi uteuzi wake alikuwa ubalozi wa Vatican nchini Colombia. Alichukua nafasi hiyo mwaka 2023 baada ya kuteuliwa na Papa Francisko , ambaye alimweka wakfu kuwa Askofu mkuu mwaka 2019 na kisha akamtuma, mnamo Januari 2020, kama mwakilishi wake nchini Zimbabwe, akimhamisha kutoka Strasbourg ambapo alikuwa Mwakilishi wa kudumu wa Vativcan  katika Baraza la Ulaya huko Strasbourg.

PAPA TEUZI ZA VATICAN

Uzoefu wa Askofu Mkuu Rudelli katika huduma ya kidiplomasia ya Vatican ulianza zaidi ya miaka ishirini, hadi 2001, kwa usahihi, akiwa na kazi yake katika uwakilishi wa Papa nchini Ecuador na Poland na katika Kitengo cha Masuala ya Jumla cha Sekretarieti ya Vatican. Sasa ataongoza sehemu hii kwa amri ya Papa Leo XIV, katika  uteuzi wake wa pili wa kuwa mkuu katika Sekretarieti ya Vatican,  kufuatia uteuzi wa mwezi Novemba mwaka 2025 wa Mtathmini, Mtaalimungu kutoka Nigeria Monsigno Anthony Onyemuche Ekpo, ambaye hapo awali alikuwa katibu msaidizi wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha  Maendeleo  Fungamani ya Binadamu.

Katika makao makuu yaliyoko Via Po

Askofu Mkuu  Rudelli anamrithi Askofu Mkuu Edgar Peña Parra wa Venezuela, ambaye Papa Leo XIV pia alimteua kuwa Balozi wa Vatican  nchini Italia na Jamhuri ya San Marino. Pia alikuwa Papa Francisko  aliyemteua Askofu Mkuu  Peña Parra kama mnamo tarehe 15 Agosti 2018, akimwita kutoka Msumbiji. Tangu 2015, alikuwa ameongoza Balozi za Vatican nchi  ya Afrika Mashariki, pia akishiriki katika kundi la upatanisho ili kurejesha amani kati ya serikali ya kitaifa na chama cha siasa cha upinzani. Akiwa amezaliwa mwaka  1960, mwanadiplomasia mkongwe mwenye uzoefu nchini Kenya, Yugoslavia, Honduras, na Mexico, na baadaye mwakilishi wa Papa nchini Pakistani, Askofu Mkuu Peña Parra alikuwa Mmarekani wa pili wa Kilatini kushikilia wadhifa huo baada ya Kardinali  Leonardo Sandri wa Argentina.

Kuongoza Nyumba ya Kipapa

Kuanzia Jumatatu tarehe 30 Machi, anakuwa mjumbe wa Nyumba ya Njia ya Po, ambayo tangu 2024 imekuwa ikiongozwa na Askofu Mkuu Petar Rajič, wa Bosnia ambaye pia aliteuliwa Baba Mtakatifu Lro XIV kama Mkuu mpya wa Nyumba ya Kipapa. Nafasi hii imekuwa wazi tangu 2023, wakati Askofu Mkuu Georg Gänswein alipomaliza muhula wake na baadaye akateuliwa kuwa Balozi katika Mataifa ya Kibaltic (Latvia, Estonia, na Lithuania). Nchi zile zile ambapo Rajič mwenyewe aliwahi kuwa Balozi tangu 2019, kabla ya kufika Italia mwaka 2024. Kwa hivyo, Askofu Mkuu atasimamia kazi ya  Ukuu Uenyekiti wa Nyumba ya Kipapa, chombo cha Curia kinachohusika na utaratibu wa ndani na usimamizi wa kila siku wa maisha ya Papa, ikiwa ni pamoja na kupanga mikutano na Katekesi  zilizopangwa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

30 Machi 2026, 12:29