Tafuta

Papa Leo XIV,Sali na Papa Aprili 2026:kwa ajili ya Mapadre katika mgogoro

Katika Nia ya Maombi ya kila mwezi ya Papa,kwa mwezi Aprili2026,Papa Leo XIV anaombea Mapadre wenye mgogoro kiroho:“Wewe unatambua mapambano yao na majeraha,upyaishe ndani mwao,uhakika wa upendo wako usio na masharti.Wasijisikie kama maafisa au mashujaa wapweke,badala yake wana wapendwa,mitume wanyenyekevu na wenye thamani na wachungaji wanaosaidiwa na sala ya watu.”

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 31 Machi 2026 ametoa sala yake kwa njia ya video kwa mwezi wa Aprili 2026 “kwa ajili ya Mapadre walioko kwenye mgogoro wa kiroho,” inayochapishwa na Mtandao wa Nia za sala ya Papa Kimataifa. Katika sala hiyo Papa anasali: “Kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu Amina. Bwana Yesu, Mchungaji mwema na msindikizaji katika safari,leo ninakukabidhi mapadre wote, hasa wale ambao wanapitia vipindi vya migogoro ya kiroho, wakati upweke unawaelemea, mashaka yanagubika moyo na uchovu utafikiri ni wa nguvu zaidi ya tumaini.”

Wasijisikie kama maafisa au mashujaa wapweke

Baba Mtakatifu Leo XIV  anaendelea kusali kwa Bwana kuwa, “ Wewe unatambua mapambano yao na majeraha, upyaishe ndani mwao, uhakika wa upendo wako usio na masharti. Wasijisikie kama maafisa au mashujaa wapweke, badala yake ni wana wapendwa, mitume wanyenyekevu na wenye thamani, na wachungaji wanaosaidiwa na sala ya watu wako.

Tufundishe kuwatunza mapadre wetu

Baba Mwema, utufundishe kama Jumuyia ya kuwatunza mapadre wetu: kwa kuwasikiliza bila kuwahukumu, kuwashukuru bila kudai ukamilifu, kushirishana nao utume wa kiubatizo wa kutangaza Ufalme kwa ishara na maneno, na kuwasindikiza na ukaribu na sala ya kweli.  Tufanye tutambua kuwasaidia wale ambao mara nyingi wanatusaidia.

Wasipoteze imani kwako,wala furaha ya kutumia Kanisa”

Papa Leo XIV anaendelea “Roho Mtakatifu, uwashe upya katika mioyo ya mapadre furaha ya Injili. Uwasaidia wao urafiki safi, mitandao ya usaidizi kidugu, kuwa na ucheshi kidogo wakati mambo yanakwenda kinyume na matarajio, na neema daima  ya kugundua tena uzuri wa wito wao. Na wasipoteze kamwe imani Kwako, wala furaha ya kutumikia Kanisa,  bali kwa moyo mnyenyekevu na mkarimu. Amina.” Anahitimisha Sala hiyo.

SALA YA PAPA MWEZI APRILI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

 

31 Machi 2026, 15:07