Tafuta

2026.04.13 Papa katika Mnara wa Mashahidi huko Maqam Echahid, Nchini Algeria 2026.04.13 Papa katika Mnara wa Mashahidi huko Maqam Echahid, Nchini Algeria  (@Vatican Media)

Ziara ya Papa Leo XIV nchini Algeria:Mungu anatamani amani!

Baba Mtakatifu alitembelea Maqam Echahid,katika Mnara wa Ukumbusho wa Mashahidi wa Algeria,huko Algiers,kituo cha kwanza katika Ziara yake ya kitume barani Afrika,na kutoa ujumbe wa matumaini kwa ulimwengu ulioharibiwa na migogoro:Haki itashinda dhuluma kila wakati.Papa Leo XIV alikumbuka kwamba utajiri wa kweli kwa watu ni kumpenda Mungu na aina zingine za utajiri hudanganya na kukatisha tamaa na kuishia kuharibu moyo na kusababisha wivu,ushindani na migogoro.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya kufika nchini Algeria ikiwa ni  Ziara yake ya barani Afrika, Baba Mtakatifu alipokelewa kwa shangwe na baadaye alikwenda kwenye Mnara wa mashahidi wa Ulgeria na kutoa hotuba yake ya kwanza. Akianza hotuba hiyo, Papa alisema “Amani iwe nanyi nyote!  As-salamu alaykom! Ninashukuru Mungu kwa kunipatia uwezekano  wa kutembelea nchi yenu kama Mfuasi wa Mtume Petro, baada ya kufanya  safari mbili tayari,  wakati uliopita, kama Mtawa wa Kiagostino. Na hasa lakini kama ndugu ambaye anawajiwakilisha mbele yenu, kwa shauku ya kuweza kupyaisha katika mkutano huu mafungamano ya upendo ambayo yanakaribia mioyo yetu.

Hotuba ya Papa katika mnara wa ukumbusho wa mashahidi
Hotuba ya Papa katika mnara wa ukumbusho wa mashahidi   (@Vatican Media)

Kwa kuwatazama ninyi nyote, Papa  Leo XIV aliongeza ninaona watu wa nguvu na kijana ambao tayari nilikuwa na namna ya kufanya uzoefu wa kurudia ukarimu na udugu. Katika moyo wa Algeria, urafiki, imani, mshikamano  sio maneno kiurahisi tu, bali ni thamani ambayo inajali na kutoa thamani na mshikamano hai wa pamoja. Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa,  Algeria ni nchi Kubwa, kuanzia na Historia yake ndefu, na tajiri ya tamaduni, hasa nyakati za Mtakatifu Agostino na kabla ya hapo. Historia moja ya uchungu  ambayo hata iliwekwa na kipindi cha vurugu, ambacho lakini shukrani kwa roho adimu ambayo inajitambulisha, na ambayo ninahisi sasa hapa,ilitambua kushinda kwa ujasiri na uaminifu.

Ziara ya Papa leo nchini Algeria

Papa Leo XIV alisema kuwa, “ kusimama kwenye Mnara huu ni heshima ya historia, na ya moyo wa watu ambao walipambania uhuru, hadhi na ukuu wa Taifa hili”. Katika eneo hilo,  Papa alisema “tukumbuke kuwa Mungu anatamani kila Taifa amani: amani ambayo si ukosefu wa mgogoro, lakini kielelezo cha haki na hadhi. Na amani hii, ambayo inaruhusu kwenda kukutana na wakati ujao kwa moyo uliopatanishwa, inawezakana tu kwa kuwa na msamaha. Papa Leo XIV aliendelea, mapambano ya kweli ya uhuru yatakuwa hatimaye kushinda tu ikiwa itaweza kupatisha amani katika mioyo.

“Ninnajua jinsi ilivyo ngumu kusamehe, Papa aliongeza “lakini mbali na hayo, wakati migogoro inaendelea kuongezeka ulimwenguni kote, haiwezekani kuongeza kiburi kwa kiburi,   kwa vizazi na vizazi. Wakati ujao ni wa wanaume na wanawake wa amani. Hatimaye haki itashinda daima dhidi ya ukosefu wa haki na kama ilivyo vurugu, mbali na kila ujuujuu, hautakua na neno la mwisho. Kwa kusisitiza zaidi Papa  alisema  jinsi ambavyo nchi hiyo ilivyo njia panda ya tamaduni na dini kuheshimiana kunawakilisha njia kwa sababu watu wanaweza kutembea pamoja.  Algeria inaweza kuwa na nguvu za mzizi yake na matumaini ya vijana wake kuendelea kutoa mchangao wenye msimamo na mazungumzo ya jumuiya za mataifa na juu ya mipaka ya Mediteranea.

Hotuba ya I ya Papa huko Algeria
Hotuba ya I ya Papa huko Algeria   (@Vatican Media)

Kila watu uhifadhi urithi mmoja wa historia, tamaduni na imani. Hata Algeria ina utajiri huu, ambao ulisaidiwa kwa kutembea katika nyakati ngumu na kuendelea kuelekeza wakati ujao.  Urithi huo, na imani kwa Mungu inachua nafasi kuu: hiyo inaangazia maisha ya watu, inasaidia familia na kuhuishwa na maana ya udugu. Watu wanaopenda Mungu wanao utajiri wa kweli, na watu wa Algeria wanahifadhi kito hicho katika hazina. Papa alisema kuwa,  “Ulimwengu wetu unahitaji  waamini wa namna hiyo, wanaume na wanawake wa imani, wenye kiu ya haki na ya umoja. Kwa njia hiyo mbele ya ubinadamu unaotamani udugu na maridhiano, ni zawadi kubwa na jitihada ya baraka ya kujitangaza kwa nguvu na kuwa daima pamoja, ndugu kati yetu na wana wa Mungu!

Wanaokwenda kutafuta aina zingine za utajiri hudanganya na kukatisha tamaa" na mara nyingi kwa bahati mbaya wanaishi kupasuka moyo wa binadamu na kusabisha wivu, ushindani na migogoro, Yesu  anarudia tena kutoa swali alilouliza miaka elfu mbili iliyopita: “Ni faida gani  mtu akiupata ulimwengu wote, na kupteza  nafsi yake? (Mt 16,26). Swali msingi kwa wote,  watu waliokufa hapa tunawaheshimu, walitoa jibu hai, “ walipoteza maisha yao, lakini kwa maana nyingine, wakitoa kwa upendo wa maisha ya watu. Historia yao iwasaidie watu wa Algeria na watu wote katika safari yetu: kwa sababu uhuru wa kweli usirithi tu, bali uchague kila siku.

Hotuaba ya Papa katika Mnara wa ukumbusho huko Algiers
Hotuaba ya Papa katika Mnara wa ukumbusho huko Algiers   (@Vatican Media)

Kabla ya kumaliza , Papa Leo XIV aliomba  ahitimishe kwa kurudia maneno ya Yesu kwa mitume wake ambayo yanaitwa  hotuba ya Mlimani au Heri: Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao. Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika. Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi. Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa. Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.  Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao( Mt 5,4-10).Papa aliwashukuru ukarimu na kwamba Mungu awabariki.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

13 Aprili 2026, 12:14