Tafuta

Papa Leo XIV:Mashahidi Afrika walijibu hatuwezi kuishi bila Ekaristi!

Tukio la kutokewa kwa Yesu kwa Tomaso linalotufanya kutafakari juu ya kukutana kwetu na Yesu Mfufuka.Siku ya nane,yaani ya kila Dominika,Kanisa linatualika kufanya kama mitume wa kwanza.Ziara ya Papa barani Afrika.Ni kwa njia ya Ekaristi ambapo hata mikono yetu inageuka kuwa mikono ya Mfufuka.Atusaidie kufanya hivyo Mwenyeheri Bikira Maria.Haya yamo kwenye tafakari ya Papa Leo IV kwa waamini na mahujaji waliofika katika sala ya Malkia wa Mbingu,Dominika Aprili 12.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Siku moja kabla ya kuanza ziara yake ya Tatu ya Kitume, kwenda barani Afrika, inayoanza tarehe 13 hadi 23 Aprili 2026, kwa kutembelea nchi ya Algeria, Cameroon, Angola na Guinea ya Ikweta, Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza tafakari yake,  Dominika ya Pili ya Pasaka, ambayo Mama Kanisa anaadhimisha Huruma ya Mungu, tarehe 12 Aprili 2026. Akiugeukia umati wa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Papa akiwa juu ya Dirisha la Jumba la Kitume alisema: “Wapendwa kaka na dada,Dominika njema na tena Pasaka Njema! Papa aliendelea, "Leo ni Dominika ya Pili ya Pasaka, iliyowekwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kwa ajili ya Huruma ya Mungu, katika Injili tunasoma kutokea kwa  Yesu Mfufuka kwa Tomaso (Yh 20,19-31).Tukio hilo lilitokea siku nane baada ya Pasaka, wakati Jumuiya  ilikuwa imeungana na ni hapo ambapo Tomaso alikutana na Mwalimu na kamualika atazame ishala za misumari na kuweka mikono yake kwenye jeraha la ubavu wake na kuamini(Yh 20, 27)."

Waamini wengi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Aprili 12
Waamini wengi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Aprili 12   (@Vatican Media)

Tukio  linalotufanya kutafakari juu ya kukutana kwetu na Yesu Mfufuka

Papa Leo XIV alibainisha kuwa “Ni tukio  linalotufanya kutafakari juu ya kukutana kwetu na Yesu Mfufuka. Ni wapi pa kumpata? Jinsi gani ya kumtambua? Namna gani ya kuamini? Mtakatifu Yohane anayesimula tukio, anatupatia maelekezo sahihi: Tomaso anakutana naye katika siku ya nane, katika Jumuiya iliyoungana, na kumtambua kupitia  ishara za sadaka yake. Kutokana na  uzoefu huu ndiyo kusadiki kwake imani, ambayo ni kubwa zaidi ya Injili Nne akisema: Bwana wangu na Mungu wangu (Yh 20, 29). “Hakika siyo rahisi daima kuamini. Haikuwa kwa Tomaso na hata  kwetu sisi. Imani inahitaji kumwilishwa na kusaidiwa.

siku ya nane, yaani ya kila dominika, Kanisa linatualika kufanya kama mitume wa kwanza

Kwa sababu hiyo katika siku ya nane, yaani ya kila dominika, Kanisa linatualika kufanya kama mitume wa kwanza; kuunganika na kuadhimisha pamoja Ekaristi.” Katika hiyo tunasikia Neno la Yesu, tunasali, tunasadiki imani yetu, tunashirikishana zawadi za Mungu katika upendo, aliongeza "tunatoa maisha yetu  katika muungano wa Sadaka ya Kristo, tunamwilishwa kwa Mwili wake na Damu yake, ili baadaye kwa kwa mara nyingine  tuwe mashuhuda wa Ufufuko wake, kama inavyoeleza mwishoni  mwa Misa yaani mwaliko wa  kutumwa kwenye utume(KKK 1332).Misa ya kila Dominika ni muhimu kwa maisha ya kikristo. "

Muonekano wa umati mkubwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Angelus
Muonekano wa umati mkubwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa ajili ya Angelus   (@Vatican Media)

Ziara ya Papa katika nchi ya Mashahidi huko Afrika-Abitene

Papa Leo XIV alieleza juu ya ziara yake  ya Kitume kwamba:“ Kesho nitasafiri kwenye ziara ya Kitume barani Afrika, na hasa zaidi  kwa baadhi ya Mashahidi wa Kanisa la Kiafrika, wa Karne ya Kwanza na Mashahidi wa Abitene, ambapo katika hilo walituachia ushuhuda mzuri sana. Mbele ya kujisadaka na kuokoa maisha kwa kukataa kuacha kuadhimisha misa, walijibu kwamba hawawezi kuishi bila kuadhimisha siku ya Bwana. Na  hapo ndipo kunakuwa na kumwilishwa na kukuza imani yetu. Hapo ndipo kuna jitihada zetu,  licha ya vikwazo, kwa neema ya Mungu zinaenea kama tendo la viungo vya mwili mmoja, Mwili wa Kristo katika kutimiza mpango mmoja mkubwa wa wokovu ambao unakumbatia ubinadamu wote.

Papa aliongoza tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana Aprili 12,2026
Papa aliongoza tafakari na Sala ya Malaika wa Bwana Aprili 12,2026   (@Vatican Media)

Ni kwa njia ya Ekaristi ambapo hata mikono yetu inageuka kuwa mikono ya Mfufuka

Ni kwa njia ya Ekaristi ambapo hata kwa mikono yetu inageuka kuwa mikono ya mfufuka, shuhuda wa uwepo wake,  wa huruma yake, wa amani yake, katika ishara za kazi, za sadaka, za ugonjwa,  za kupita kwa miaka, yaani uzee, ambapo mara nyingi  zimeacha alama, kama vile katika upole wa kubembelezwa, kukumbatiwa, ishara ya upendo. Kwa kuhitimisha, Papa Leo alielezea kwamba katika ulimwengu ambao unahitaji sana amani, hii inatubidisha zaidi kuliko hapo awali kuwa waangalifu na waaminifu katika mkutano wetu wa kiekaristi na Yesu Mfufuka, ili kuanza tena safari kama mashuhuda wa upendo na wabebaji wa upatanisho. Atusaidie kufanya hivyo Mwenyeheri Bikira Maria, kwa sababu, akiwa wa kwanza aliamini bila kuona.

TAFAKARI YA PAPA WAKATI WA MALKIA WA MUNGU

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

12 Aprili 2026, 11:30