Tafuta

Papa Leo XIV anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema, kuungana pamoja naye katika mkesha wa kuombea amani duniani utakaofanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumamosi, tarehe 11 Aprili 2026, Papa Leo XIV anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema, kuungana pamoja naye katika mkesha wa kuombea amani duniani utakaofanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumamosi, tarehe 11 Aprili 2026,   (AFP or licensors)

Papa Leo XIV: Mwaliko wa Kushiriki Mkesha wa Sala Kuombea Amani Duniani

Papa Leo XIV anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema, kuungana pamoja naye katika mkesha wa kuombea amani duniani utakaofanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumamosi, tarehe 11 Aprili 2026, Majira ya Saa 12:00 Jioni kwa saa za Ulaya, sawa na Saa 1:00 kwa Saa za Afrika Mashariki na Kati katika Mkesha wa Dominika ya Huruma ya Mungu. Mkesha huu utaongozwa na Baba Mtakatifu Leo XIV na walengwa ni waamini wote!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV katika Salam, Baraka na Ujumbe wake kwa mji wa Roma na Ulimwengu katika ujumla wake, maarufu kama “Urbi et Orbi” Sherehe ya Pasaka, Dominika tarehe 5 Aprili 2026 amesema, Kristo Yesu kwa njia ya mateso, kifo na ufufuko wake amewakirimia walimwengu maisha na uzima wa milele. Yn 14:27. Amani ya Kristo Mfufuka ni ile inayosimikwa katika toba na wongofu wa ndani kwa ajili ya amani, mwaliko kwa waamini na watu wote wenye mapenzi mema, kupaaza sauti zao ili kuwafanya watu wasikie kilio cha sauti ya nyoyo zao. Baba Mtakatifu Leo XIV anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema, kuungana pamoja naye katika mkesha wa kuombea amani duniani utakaofanyika kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumamosi, tarehe 11 Aprili 2026, Majira ya Saa 12:00 Jioni kwa saa za Ulaya, sawa na Saa 1:00 kwa Saa za Afrika Mashariki na Kati katika Mkesha wa Dominika ya Huruma ya Mungu. Mkesha huu utaongozwa na Baba Mtakatifu Leo XIV na walengwa ni waamini na watu wote wenye mapenzi mema. Hakuna ulazima wa kuwa na tiketi ya kuingilia.

Mkesha wa sala Kwa ajili ya kuombea amani duniani
Mkesha wa sala Kwa ajili ya kuombea amani duniani   (AFP or licensors)

Katika maadhimisho ya Sherehe ya Pasaka ya Bwana, anasema Baba Mtakatifu Leo XIV iwe ni fursa ya kuonesha utashi wa kutotaka kutawala, nguvu na mabavu na matokeo yake, wamwombe Kristo Mfufuka aweze kuwakirimia walimwengu amani inayoendelea kusiginwa sehemu mbalimbali za dunia kutokana na vita, chuki na tabia ya kutojali, hali inayowafanya walimwengu kuwa wanyonge mbele ya ubaya na dhambi. Huu ni mwaliko kwa waamini kuweka mbele ya Kristo Mfufuka mateso na mahangaiko ya watu kutoka sehemu mbalimbali za dunia; watu wenye kiu na amani ya kweli, inayoweza kutolewa na Kristo Yesu Mfufuka peke yake. Huu ni mwaliko kwa waamini kujiaminisha mbele ya Kristo Mfufuka kwa kumfungulia nyoyo zao, kwani ni Kristo peke yake anayeweza kufanya yote kuwa ni mapya. Rej Ufu21:5.

Papa Leo XIV anatoa mwaliko wa kuungana naye kusali kwa ajili ya amani
Papa Leo XIV anatoa mwaliko wa kuungana naye kusali kwa ajili ya amani   (@Vatican Media)

Wakati huo huo, Marekani, Israel na Iran zimekubaliana kusitisha mapigano kwa wiki mbili baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kukubaliana na mpango wa vipengele 10 wa Tehran, inayosema sasa itashiriki mazungumzo ya Islamabad kuanzia Ijumaa. Tamko hili lilitolewa na Baraza Kuu la Usalama la Iran, likiwashukuru Wairani kwa uvumilivu na kujitolea kwao muda wote wa kushambuliwa na Israel na Marekani, Tamko hilo lilitolewa muda ule ule ambapo mamilioni ya Wairani walikuwa wamejitokeza kuhami vituo vya umeme, mafuta, majengo ya umma na madaraja, kufuatia kitisho cha Rais Trump kwamba angeliamuru kuripuliwa kwa maeneo hayo!

Madhara ya vita kati ya Iran, Israeli na Marekani yameanza kutoa kucha
Madhara ya vita kati ya Iran, Israeli na Marekani yameanza kutoa kucha   (AFP or licensors)

Mapema asubuhi siku ya Jumatano tarehe 8 Aprili 2026 Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ilisema inauunga mkono uamuzi wa Rais Trump wa kusitisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa wiki mbili, lakini ikaonya kwamba uamuzi huo haujumuishi vita vyake nchini Lebanon, ambako hadi sasa zaidi ya watu 1,500 wamepoteza maisha na zaidi ya watu milioni moja wameyakimbia makazi yao. Kwa mujibu wa mpango huo, Iran inataka iendelea kuudhibiti Mlango Bahari wa Hormuz, iendelee na urutubishaji wa madini ya Urani na iondolewe vikwazo vyote vya awali na vya nyongeza. Vile vile, Iran inaitaka Marekani kuondoa vituo vyake vya kijeshi eneo zima la Mashariki ya Kati, kuziachia mali zake zinazoshikiliwa na Marekani na kuwepo kwa Azimio maalum la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuyahalalisha na kuyapa nguvu za kisheria makubaliano hayo. Kwa upande wake Baba Mtakatifu Leo XIV ameonesha kuridhika kwake kutokana na uamuzi uliofanywa na Marekani, Israel na Iran na kwamba, huu ni mwanzo wa kufikia mwisho wa vita huko Mashariki ya Kati, kwani ni kwa njia ya majadiliano tu inawezekana kufikia mwisho wa vita. Majadiliano katika ukweli na uwazi ni chombo madhubuti cha kufikia suluhu ya kudumu ya vita, kinzani na mipasuko inayoendelea kuwaandama walimwengu.

Sala, Majadiliano katika ukweli na uwazi pamoja na diplomasia ni muhimu
Sala, Majadiliano katika ukweli na uwazi pamoja na diplomasia ni muhimu   (2026 Getty Images)

Baba Mtakatifu Leo XIV anasema: Sala na diplomasia ya Kimataifa ni nyenzo muhimu katika kujenga na kudumisha misingi ya haki na amani sehemu mbalimbali za dunia. Baba Mtakatifu anakaza kusema, Jumuiya ya Kimataifa inakabiliana na changamoto ya kuyumba kwa uchumi wa Kimataifa; Ukosefu wa haki na amani huko Mashariki ya Kati kwamba umeanza kuonesha makali yake sehemu mbalimbali za dunia kutokana na mfumuko mkubwa wa bei za nishati ya mafuta. Wakati huo huo, Kardinali Matteo Maria Zuppi, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI, anasema inawezekana kabisa kuwa na matumaini yanayosigana na matumaini, licha ya mateso na maafa makubwa ya watu na mali zao. Kuna kilio kikubwa cha mahangaiko ya watu sehemu mbalimbali za dunia kutokana na vita inayorutubishwa kwa uchu wa fedha na mali hali inayopelekea matumizi mabaya ya rasilimali za dunia. Ni katika muktadha huu, Baraza la Maaskofu Katoliki Italia, CEI linawaalika watu waaminifu wa Mungu nchini Italia kuungana na Baba Mtakatifu Leo XIV kwa ajili ya kushiriki katika mkesha wa kuombea amani duniani. Huu ni wakati wa kusema, “Hapana kwa vita na kamwe watu wasifanye mazoea na vita.”

Papa Leo XIV Kuongoza Mkesha wa Sala kwa ajili ya kuombea amani
Papa Leo XIV Kuongoza Mkesha wa Sala kwa ajili ya kuombea amani   (@Vatican Media)

Kwa upande wao, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio, iliyoanzishwa na Profesa Andrea Riccardi tarehe 7 Februari 1968, yenye Makao yake makuu katika Kanisa kuu la Bikira Maria wa Trastevere mjini Roma, ambayo imeendelea kujipambanua katika mambo makuu matatu: Sala, Maskini, na Amani duniani katika nchi 70 sehemu mbalimbali za dunia. Jumuiya hii imetangaza kushiriki kikamilifu katika Mkesha wa Sala ya Kuombea Amani Duniani tarehe 11 Aprili 2026. Mahali popote pale walipo wanachama wa Jumuiya hii watakutana kusali kwa ajili ya kuombea amani huko: Mashariki ya Kati, Ukraine na katika nchi zile ambazo bado zinasiginwa na vita, vitendo vya kigaidi pamoja na mipasuko ya kijamii.  

Mkesha Kuombea Amani
09 Aprili 2026, 16:09