Papa Leo XIV na Zelensky kwa Simu:ukaribu kwa Ukraine na msaada wa dharura wa kibinadamu
Vatican News
Siku ya Ijumaa Kuu Takatifu asubuhi, tarehe 3 Aprili 2026, kumekuwa na mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Baba Mtakatifu Leo XIV na Rais Volodymyr Zelensky, wa Ukraine. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu imebainisha kuwa: "Ukaribu na watu wa Ukraine" uliooneshwa na Papa kwa Rais wa Ukraine na hoja iliyotolewa kuhusu hali ya kibinadamu, ambayo alisisitiza, "umuhimu wa kuhakikisha msaada unaohitajika kwa idadi ya watu walioathiriwa na mzozo."
Kuachiliwa kwa Wafungwa na ukomeshwa kwa uadui
Katika taarifa hiyo inasomeka kwamba "zingatio la pamoja kati ya Papa na Zelensky lilikuwa juhudi zinazofanywa za "kukuza, mipango ya kibinadamu, hasa kuhusu kuachiliwa kwa wafungwa." Mwishoni mwa mazungumzo hayo wameonesha, "matumaini yaliyopyaishwa kwa kujitolea na usaidizi wa Jumuiya ya Kimataifa, kukomeshwa kwa uhasama na amani ya haki na ya kudumu kunaweza kupatikana haraka iwezekanavyo."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
