Tafuta

Papa Leo XIV: Walei watu wa Mungu washuhudie haki na amani Ulimwenguni!

Papa Leo XIV ameendeleza na mzunguko wa Katekesi kuhusu hati ya Mtaguso ya Lumen gentium,Aprili 1,kwa kujikita na mada:asili ya watu wa kimasiha kuwa "siyo kundi lisilo na umbo,bali jumuiya iliyo na muundo,inayoishi kutokana na uhusiano kati ya Mapadre na Walei.Kanisa linapaswa kuwa la kirafiki na walei wanapaswa kushuhudia amani na haki.Akiwasalimu waamini wa lugha ya Kiarabu, aliwaalika kuwaombea waathiriwa wasio na hatia wa vita.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Jumatano tarehe 1 Aprili 2026, tukiwa katika Juma Kuu Takatifu kuelekea Mateso, kifo na Ufufuko wa Bwana, Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea na Katekesi yake, kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican. Katika mzunguko wa Katekesi yake ambaye ambapo alijikita  na mada: "Mawe Hai katika Kanisa na Mashahidi Duniani: Walei katika Watu wa Mungu," ulikuwa ni mwendelezo wa  hati za Mtaguso wa Pili wa Vatican hasa katiba ya kidogma Lumen gentium.

Katekesi ya Papa Leo XIV Aprili 1,2026
Katekesi ya Papa Leo XIV Aprili 1,2026   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu alianza na salamu za asubuhi kwa wote, kaka na dada na kuendelea: “Tunaendelea na safari yetu ya kutafakari Kanisa kama ilivyowasilishwa kwetu katika Katiba ya Mtaguso  Lumen Gentium (LG). Leo tuzungumzia sura ya nne, ambayo inazungumzia Walei. Sote tunakumbuka kile ambacho Papa Francisko alipenda kurudia: "Walei kwa urahisi ni idadi kubwa ya Watu wa Mungu. Katika huduma yao ni wachache: wahudumu waliowekwa wakfu" (Wosia wa Kitume Evangelii Gaudium, 102).“

Kuna wokovu mmoja, tumaini na upendo usiogawanyika

Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa "Sehemu hii ya Hati inatafuta kuelezea vyema asili na utume wa walei,, Papa Leo XIV aliongeza “ baada ya karne nyingi ambapo walifafanuliwa tu kama wale ambao si sehemu ya mapadre  au watu waliowekwa wakfu.” Kwa sababu hiyo,  Papa Leo XIV alipenda kusoma tena kifungu kizuri sana kinachoelezea ukuu wa hali ya Kikristo: "Kwa hivyo watu wamoja waliochaguliwa naye kwamba, kuna 'Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja' (Efe 4:5). "Wajumbe wanashiriki hadhi ya pamoja kupitia kuzaliwa upya katika Kristo, neema ya pamoja ya kuasiliwa kama watoto, wito wa pamoja wa ukamilifu; kuna wokovu mmoja tu, tumaini moja, na upendo usiogawanyika" (LG, 32).

Utume huu umeanzishwa wapi na unajumuisha nini?

Kabla ya tofauti yoyote katika huduma au hali ya maisha, Mtaguso unathibitisha usawa wa wote waliobatizwa. Katiba haitaki tusahau kile ambacho tayari ilithibitisha katika sura kuhusu Watu wa Mungu, yaani, kwamba hali ya watu wa kimasiha ni hadhi na uhuru wa watoto wa Mungu (taz LG, 9). Kwa kawaida, kadiri karama inavyokuwa kubwa, ndivyo kujitolea sana kunavyokuwa. Kwa sababu hiyo, Papa alieleza kuwa Mtaguso, pamoja na hadhi, pia unasisitiza utume wa walei katika Kanisa na Ulimwenguni. Lakini utume huu umeanzishwa wapi na unajumuisha nini? Maelezo yenyewe ya walei ambayo Mtaguso unatupatia,  inatuambia hivi: "Kwa neno 'walei' linamaanisha Wakristo wote waaminifu [...] ambao, waliojumuishwa katika Kristo kwa ubatizo na kufanywa kuwa Watu wa Mungu, wamekuwa washiriki kwa njia yao wenyewe katika huduma ya kikuhani, unabii, na ufalme wa Kristo. Wanatekeleza, kwa njia yao wenyewe, utume wa watu wote Wakristo katika Kanisa na katika ulimwengu" (LG, 31).

Katekesi ya Papa Aprili 1,2026
Katekesi ya Papa Aprili 1,2026   (@Vatican Media)

Kwa sababu ya Ubatizo, wamini walei hushiriki katika ukuhani uleule wa Kristo

Kwa hivyo, Papa Leo XIV  aliendelea kufafanua kuwa,  watu watakatifu wa Mungu si wingi usio  na umbo, bali ni mwili wa Kristo, au, kama Mtakatifu Agostino alivyosema, Christus totus: ni jumuiya iliyojengwa kiumuundo kamili, kwa sababu ya uhusiano wenye matunda kati ya aina mbili za ushiriki katika ukuhani wa Kristo: ukuhani wa pamoja wa waamini na ukuhani wa kihuduma (taz LG, 10). Papa Leo XIV, alisisitiza kwamba “kwa sababu ya Ubatizo, wamini walei hushiriki katika ukuhani uleule wa Kristo. Hakika, "Yesu Kristo, kuhani mkuu wa milele, anataka kuendelea na ushuhuda wake na huduma yake pia kupitia walei; kwa hivyo anawahuisha kwa Roho wake na huwasukuma bila kukoma kufanya kila kazi njema na kamilifu" (LG, 34).” Tunawezaje kutokumbuka, katika suala hilo, Mtakatifu Yohane Paulo II na Wosia wake wa Kitume Christifideles laici (Desemba 30, 1988), Papa Leo XIV alibainisha. “Ndani yake, alisisitiza kwamba "Mtaguso,  pamoja na urithi wake tajiri wa mafundisho, kiroho, na kichungaji, umetoa kurasa nzuri sana kuhusu asili, hadhi, hali ya kiroho, utume, na wajibu wa waamini walei.

Mababa wa Mtaguso,wakirudia wito wa Kristo,waliwaita waamini wote walei,kufanya kazi katika shamba la mizabibu

Mababa wa Mtaguso, wakirudia wito wa Kristo, waliwaita waamini wote walei, wanaume na wanawake, kufanya kazi katika shamba lake la mizabibu" (Kifungu n.2). Kwa njia hiyo, Papa Leo XIV alikumbusha  Mtangulizi wake, kwamba ,“alizindua upya utume wa walei, ambao Mtaguso ulikuwa umeweka katika Hati maalum, ambayo  Papa alisisitiza kwamba ataijadili hapo baadaye. Uwanja mkubwa wa utume wa walei haupo tu kwa Kanisa, bali umeenea hadi ulimwenguni. Hakika, Kanisa lipo popote ambapo watoto wake wanakiri na kushuhudia Injili: mahali pa kazi, katika jamii ya kiraia, na katika mahusiano yote ya kibinadamu, popote pale ambapo, kwa chaguo zao, wanaonesha uzuri wa maisha ya Kikristo, ambayo yanatarajia hapa na sasa haki na amani ambayo itakamilika katika Ufalme wa Mungu.

Katekesi ya Papa Aprili 1, 2026
Katekesi ya Papa Aprili 1, 2026   (@VATICAN MEDIA)

Dunia inahitaji "kujazwa na roho ya Kristo na kufikia lengo lake kwa ufanisi zaidi katika haki, upendo, na amani

Baba Mtakatifu Leo XIV alisisitiza kuwa, “Dunia inahitaji "kujazwa na roho ya Kristo na kufikia lengo lake kwa ufanisi zaidi katika haki, upendo, na amani"(Lumen Gentium, 36). Na hili linawezekana tu kwa mchango, huduma, na ushuhuda wa walei! Ni mwaliko wa kuwa Kanisa "linalotoka nje" ambalo Papa Francisko alizungumzia: Kanisa lililofanyika mwili katika historia, lililo wazi kila wakati kwa utume, ambalo sote tumeitwa kuwa wanafunzi wa kimisionari, mitume wa Injili, mashahidi wa Ufalme wa Mungu, wabebaji wa furaha ya Kristo tuliyekutana naye! Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alisema “Kaka  na dada, Pasaka tunayojiandaa kusherehekea ifanye upya ndani yetu neema ya kuwa, kama Maria Magdalene, kama Petro na Yohane, mashahidi wa Mfufuka!”

Makundi ya mahujaji katika katekesi ya Papa Leo Aprili 1
Makundi ya mahujaji katika katekesi ya Papa Leo Aprili 1   (@Vatican Media)

Sala kwa ajili ya waathiriwa wasio na hatia katika vita

Baba Mtakatifu Leo katika salamu zake akiwaelekea wanauzungumza lugha ya kiarabu, aliwaalika kusali kwa ajili ya wagonjwa, maskini na waathiriwa wote wasio na hatia wa vita.” Kristo, kupitia Ufufuko wake, awape kila mtu amani na faraja. Bwana awabariki nyote na awalinde daima kutokana na uovu wote!”

Katekesi ya Papa Aprili 1,2026
Katekesi ya Papa Aprili 1,2026   (@Vatican Media)
KATEKESI PAPA 1 APRILI 2026

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

01 Aprili 2026, 12:26