Tafuta

Pd.Pasolini:Wakristo waweke silaha zao chini na kuamini Msalaba

Katika mahubiri ya Ibada Kuu ya Mateso ya Bwana,iliyoongozwa na Papa Leo XIV katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro,mhubiri wa Nyumba ya Kipapa alionesha jinsi Yesu alivyoiga mfano wa Mtumishi wa Bwana kutoka nabii Isaya akianzisha mantiki mpya katika historia.Katika wakati ulioraruliwa na chuki na vurugu,Wakristo waweke silaha zao chini na kutumaini Msalaba.Katika duniani iliyo na vita tujifunze kutoka kwa Kristo kutolipiza mabaya tuliyoyapata."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tunaishi katika ulimwengu ambapo sauti ya Mungu haiongoi tena safari ya pamoja ya wanadamu kama ilivyokuwa hapo awali. Sio kwa sababu sauti ya Mungu imefifia, lakini kwa sababu mara nyingi imekuwa sauti moja kati ya nyingi, ikizimwa na maneno mengine yanayoahidi usalama, maendeleo, na ustawi. Katika vita, katika migawanyiko, katika majeraha yanayoashiria mahusiano yetu yote, uovu unaendelea kuenea kwa sababu kila mara hupata mtu aliye tayari kuulipa na kuuzidisha. Kutoka kwake Kristo aliyefufuliwa Msalabani, wanadamu badala yake hujifunza mantiki mpya kabisa: Yesu alivunja mnyororo huu, akikaribisha yaliyompata na kutambua ndani yake alama ya upendo na huduma aliyokabidhiwa maishani mwake.

Ibada ya Ijumaa Kuu
Ibada ya Ijumaa Kuu   (@VATICAN MEDIA)

Haya yalikuwa kiini cha mahubiri yaliyotolewa na Padre Roberto Pasolini,OFMCap, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa, wakati wa Maadhimisho ya Ibada kuu ya  Mateso ya Bwana,  siku ya Ijumaa Kuu, jioni tarehe 3 Aprili 2026, siku ya kipekee katika siku tatu Kuu za Juma Kuu katika mwaka,  ili kukumbusha siku ile ambayo Bwana alitupenda hadi mwisho wa maisha yake. Mama Kanisa huadhimisha Ibada Kuu ya Mateso ya Bwana, ambayo kwa kawaida, ina sehemu tatu: Ibada ya Neno, ikifikia kilele katika kuimba Mateso; Kuabudu Msalaba; na kupokea Komunyo Takatifu. Misa ilioongozwa na Baba Mtakatifu Leo XIV katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kwa kuudhuliwa na makardinali, maaskofu, mapadre na waamini watu wa Mungu.

Ibada ya Ijumaa Kuu
Ibada ya Ijumaa Kuu   (@Vatican Media)

Kufunguliwa kwa Liturujia kwa ukimya

Liturujia ilifunguliwa, katikati ya ukimya wa kusanyiko ndani ya Kanisa, kwa maandamano na Papa mwenyewe, na baada ya kufika na kulala kifudifudi kwa sekunde chache za ukimya chini. Baada ya somo refu la Mateso, Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa, Padre Pasolini, OFMCap, alianza mahubiri yake akikumbusha kwamba katika siku hii takatifu, liturujia inatualika kutafakari Mateso ya Bwana, na kusema kwamba Msalaba wa Kristo una hatari ya kutoeleweka ikiwa tutauona kama ukweli wa pekee, kama tukio la ghafla na lisiloelezeka, lakini badala yake ni sehemu ya juu zaidi ya safari. Kiukweli, ni utimilifu wa maisha ambayo Yesu alijifunza kusikiliza na kukaribisha sauti ya Baba, akijiruhusu kuongozwa na upendo mkuu.

Ibada ya Ijumaa Kuu
Ibada ya Ijumaa Kuu   (@Vatican Media)

Mtumishi wa ajabu ambaye kupitia kwake Mungu analeta wokovu kwa ulimwengu

Padre Pasolini alisema kuwa  wakati wa siku za Juma Takatifu, liturujia imetuongoza kusikiliza kile kinachoitwa "Nyimbo za Mtumishi wa Bwana," maandishi ya kishairi ambapo nabii Isaya anaelezea umbo la Mtumishi wa ajabu ambaye kupitia kwake Mungu analeta wokovu kwa ulimwengu kutoka katika uovu na dhambi. Padre  Pasolini alikumbusha  kwamba katika wimbo wa kwanza, Mtumishi anatambulishwa kama mtu aliyeitwa na Bwana kutekeleza kufumbua 'macho ya vipofu' na kuwatoa 'wafungwa kutoka kifungoni, na kutoka gerezani wale wanaoishi gizani, lakini kufanya hivyo kwa njia sahihi, bila vurugu na upole mwingi.

Mtumishi lazima awe mtafutaji wa uzima katikati ya giza la uovu

Padre Pasolini alisisitiza,  Mtumishi lazima awe mtafutaji wa uzima katikati ya giza la uovu, na kwamba utume kama huo si rahisi kuukubali. Katika wimbo wa pili, Mtumishi, baada ya kujitahidi kutimiza utume wake, anapata hisia kali kwamba juhudi zake zote za kutenda mema zimekuwa bure, akifikiri kwamba mema yaliyopandwa hayaonekani kuzaa matunda. Ni mgogoro ambao, mapema au baadaye, unamfikia mtu yeyote ambaye amechagua kumfuata Bwana: hisia ya kwenda kwenye mizunguko, ya kutofika popote, ya kubaki mwaminifu kwa kitu ambacho hakitoi matokeo yanayoonekana. Lakini kiukweli, ni hisia tu, Ndugu Pasolini alisisitiza, 

Ibada ya Ijumaa Kuu
Ibada ya Ijumaa Kuu   (@Vatican Media)

Ukatili waliomtendea Mtumishi ni mkali sana 

Katika wimbo wa tatu, Mtumishi anatambua kwamba wale anaotaka kuwasaidia wanajibu kwa uadui, hasira, na hata vurugu. Hata hivyo, mhubiri alisema, Mtumishi anaendelea katika njia iliyoonyeshwa na Bwana bila kukimbia. Katika wimbo wa nne, Padre Pasolini alionya, jambo la kushangaza linatokea. Ukatili waliomtendea Mtumishi ni mkali sana kiasi kwamba unaharibu uso wake, na kumfanya asitambulike...Lakini hasa katika njia hiyo, amejifunza kutorudisha uovu bali anaopokea.

Yesu, alivunja mnyororo 

Baada ya kutafakari kila moja ya nyimbo hizi, Padre Pasolini alitoa ukumbusho wenye nguvu kwamba Yesu hakusikiliza nyimbo hizi tu, bali alizitafsiri na kuziishi kikamilifu. Kwa imani kamili katika mapenzi ya Baba, Bwana, alibadilisha kusulubiwa kwake kuwa tukio la wokovu.” Alionesha masikitiko kwamba ulimwengu unapokabiliwa na uovu unajua njia mbili tu, ile ya kujisalimisha kwa uovu au kulipiza kisasi kwamba, "Tunaona hili kila mara: katika vita, katika migawanyiko, katika majeraha yanayoashiria mahusiano yetu." Yesu, alivunja mnyororo huu si kwa kujilazimisha kwa nguvu zaidi, bali kwa kupokea kile kilichompata, pamoja na matukio makubwa ya Mateso.

Ibada ya Ijumaa Kuu
Ibada ya Ijumaa Kuu   (@VATICAN MEDIA)

Vita havikomi,dhuluma huongezeka na walio dhaifu zaidi hubeba gharama

Kwa njia hiyo, kwa kutembea Njia ya Msalaba, Kristo, alijifunza utii mgumu zaidi: ule wa kumpenda mwingine, hata wakati mwingine akionekana kama adui. Padre Pasolini alibainisha kwamba “tunaishi katika ulimwengu ambao sauti ya Mungu haiongoi tena njia ya pamoja ya ubinadamu kama ilivyokuwa hapo awali. Vita havikomi, dhuluma huongezeka, na walio dhaifu zaidi hubeba gharama.” Lazima kuchaguzi kwenda kinyume na sasa na kufuata mfano wa Bwana. Kwa njia hiyo ni kana kwamba neno au wimbo unaounganisha unaoweza kuongoza ubinadamu kuelekea ulimwengu wa haki na udugu zaidi haupo. Na bado, hasa katika hali hii, jambo la kushangaza linaweza kuonekana: umati wa watu kimya ambao huchagua kusikiliza sauti tofauti, ambayo wengine wanaitambua wazi kama mapenzi ya Mungu, huku wengine wakiiona kama wito wa kina na usioepukika wa dhamiri.

Papa Leo XIV
Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

 Uovu hauna neno la mwisho

Padre Pasolini aliendelea kusema kuwa,  baadhi huchagua kusikiliza wimbo huu. Na hawa ni wanaume na wanawake wa kawaida ambao hutembea, wakati mwingine bila hata kutambua, njia sawa na Mtumishi wa Bwana. Hawafanyi matendo ya ajabu lakini, Wanaamka tu kila siku na kujaribu kufanya maisha yao kuwa kitu ambacho hakiwatumikii wao wenyewe bali na wengine. Ni kutokana nao kwamba uovu hauna neno la mwisho na historia haiishii katika vurugu. Umati huu unashuhudia kwamba nyimbo za Mtumishi huyo, ambaye Mungu anapendezwa naye zinaendelea kusikika katika moyo wa mwanadamu, zikimsubiri  mtu tu aliye tayari kuzitafsiri kuwa alama halisi ya maisha ya mtu mwenyewe, hata wakati hii ina maana ya kubeba msalaba wenyewe."

Alama ya Msalaba imekabidhiwa kwetu

Enzi zile  kama ilivyokuwa na leo hii, ulimwengu unahitaji kuokolewa kutokana na vurugu za uovu, kutoka katika dhuluma inayoua, kutoka katika migawanyiko inayodhalilisha. Lakini wokovu huu hautashuka kutoka juu, wala hauwezi kuhakikishwa na maamuzi ya kisiasa, kiuchumi, au kijeshi, badala yake ulimwengu unaokolewa kila mara na wale walio tayari kukumbatia nyimbo za Mtumishi wa Bwana kama jinsi wanavyoishi maisha yao,” alisisitiza Padre Pasolini. Hili, ndilo Bwana Yesu alifanya alipokubali mapenzi ya Baba kwa uzito, akiyakumbatia kama “alama” ya kutekelezwa hadi mwisho, kwa vilio vikubwa na machozi, na jioni hii, alama ya Msalaba imekabidhiwa kwetu pia,” alibainisha Mhubiri wa Nyumba ya Kipapa.  

Tunaweza kuipokea bure ikiwa tutakubali kwamba hakuna hali ngumu ambayo haiwezi kukabiliwa, hakuna mtu mwenye hatia ambaye lazima tumnyooshee kidole, hakuna adui anayeweza kutuzuia kumpenda na kumtumikia. Mhubiri wa Papa alisisitiza kuwa badala yake, ni lazima tugundue. Kuna sisi pekee, ambao  kwa kuchagua kutorudisha uovu, kwa kubaki wavumilivu katika majaribu, kwa kuamini mema hata wakati giza linaonekana kumeza kila kitu, tunaweza kuwa watumishi ambao Bwana anataka kuwatumia kuleta wokovu kwa ulimwengu."

Yesu Kristo umetukomboa kwa Msalaba wako Mtakatifu
Yesu Kristo umetukomboa kwa Msalaba wako Mtakatifu   (@Vatican Media)

Sisi Wakristo tumeitwa kuukaribia Msalaba wa

Katika wakati kama wetu, ambao bado umeraruliwa na chuki na vurugu, ambapo hata jina la Mungu linaitwa ili kuhalalisha vita na maamuzi ya kifo, sisi Wakristo tunaitwa kuukaribia msalaba wa Bwana bila woga, kiukweli "kwa ujasiri kamili" (Waebrania 4:16), tukijua kwamba ni kiti cha enzi ambacho tunaketi na kujifunza kutawala pamoja Naye, tukitoa maisha yetu kwa ajili ya kuwahudumia wengine. Tukiweza kudumisha "imara  ungamo letu la imani" (Waebrania 4:14), siku zetu pia zitatoa sauti kwa nyimbo za furaha na mateso, alama hiyo ya ajabu ya msalaba ambayo noti za upendo mkuu zinaweza kutambuliwa, alihitimisha.

Ibada ya Ijumaa Kuu
PAD PASOLINI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

 

03 Aprili 2026, 19:00