Tafuta

2026.04.11 Sala ya Rozari kuomba zawadi ya amani. 2026.04.11 Sala ya Rozari kuomba zawadi ya amani.  (@Vatican Media) Tahariri

Wito wa Papa kwa walio kimya wengi wanaochagua amani

Papa Leo XIV aliwataka mabilioni ya watu ulimwenguni kote wanaokataa kujisalimisha kwa ibada ya sanamu ya pesa na madaraka katika saa hii ya kihistoria ya kusisimua kuunganisha nguvu dhidi ya"wazimu wa vita."

Andrea Tornielli

Mbele ya kukakabiliwa na mauaji na vita vinavyosababishwa na ibada ya sanamu ya nguvu ya wale wanaodai hata "kumshawishi" Mungu kuwa upande wao kwa kutoa uhalali wa kidini kwa mauaji ya watu wasio na hatia, Papa Leo XIV aliwaomba watu wengi duniani kote wanaotamani amani, wanaoamini katika amani, wanaomba amani, na kuijenga siku baada ya siku. Alifanya hivyo jioni ya Jumamosi, tarehe 11 Aprili 2026, wakati wa Mkesha wa Sala  aliouitisha ili kuomba kukomeshwa kwa vita vinavyoendelea duniani kote.

Tayari Jumanne, Aprili 7, huko Castel Gandolfo , jambo sawa kama hilo lilitokea mbele ya kikabiliwa na tishio la kuangamiza ustaarabu wa Iran lililotangazwa kwenye mitandao ya kijamii na Rais wa Marekani, ambapo Mrithi wa Petro alikuwa amewaalika raia wa nchi yake kuwasiliana na wajumbe  wa Bunge ili kuomba amani na kusimamisha shambulio kubwa dhidi ya miundombinu ya Iran. Sasa, katika siku ile ile ya maadhimisho ya miaka 63 ya Waraka wa Kitume wa Pacem in terris  wa Papa Yohane  XXIII, Wito huo huo umekuwa wa ulimwengu wote na unaelekezwa kwa "mamilioni, mabilioni ya wanaume na wanawake, wazee kwa vijana, ambao leo hii wanaamini katika amani" na ambao "huponya majeraha na kurekebisha uharibifu ulioachwa na wazimu wa vita."

Papa Leo anatuomba tusikilize hasa sauti za watoto ambao wamewaona wenzao wakifa chini ya mabomu huko Gaza, Iran, Ukraine, na sehemu nyingine nyingi za dunia. Chini ya Juma moja kabla ya sherehe ya Pasaka na usiku wa kuamkia Pasaka katika Makanisa ya Mashariki, akikumbuka ushindi usio na ulinzi wa Mkuu wa Amani, Askofu wa Roma kwa hivyo anategemea tumaini na maombi ya wengi ya kimya kukabiliana na saa ya kushangaza katika historia ambayo ubinadamu unapitia. Anatuomba tuunganishe maombi ya wengi na "uwezekano usio na kikomo wa Mungu" kujaribu kuvunja kile anachokiita "mnyororo wa uovu wa shetani." Maneno ya Papa, ambaye amefanya amani kuwa sifa muhimu ya mafundisho yake, yako wazi katika kutambua mzizi wa vita ambao hatimaye ni wa kishetani na katika kukataa kurudiwa tena kwa "Mungu yu pamoja nasi."

Hapana, Mungu hawezi kuwa pamoja na wale wanaoua raia. Mungu yuko pamoja na wale wanaoteseka, pamoja na wale wanaokufa chini ya kifusi. Kwa maneno mengine yaliyotumiwa na Papa Leo XIV yanashangaza: sala ni "kizuizi kwa ule msongo wa mawazo wa uweza ambao karibu nasi unazidi kutabirika na kuwa mkali," kwa sababu wale wanaosali wanajua mapungufu yao wenyewe na hawaui wala kutishia. Kinyume kabisa cha wale wanaojifanya "wenyewe na nguvu zao wenyewe kuwa sanamu bubu, kipofu, na kiziwi ambayo wanaitoa sadaka kila thamani na kudai kwamba ulimwengu mzima upige goti."

Itakuwa ni makosa kufikiria  mwaliko huu wa maombi kama njia ya kutoroka kiroho. Inaonesha hili katika kifungu kingine kutoka katika tafakari ya Mrithi wa Petro. Baada ya kutaja jukumu la kila mtu la kujenga amani, kukutana, na urafiki kila mahali, Papa Leo XIV anatualika kuamini "katika upendo, kiasi, na siasa nzuri." Siasa ambayo, bila kuzingatia maneno "mazungumzo" na "majadiliano" kuwa yasiyofaa, hatimaye yanafuata makubaliano ya amani ya kudumu. 

TAHARIRI TOERNIELLI -SALA PAPA
Sala ya kuomba zawadi ya amani tarehe 11 Aprili 2026

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

11 Aprili 2026, 20:10