Wito wa Papa Leo XIV:Ni wajibu wa kimaadili kuwalinda rai na athari mbaya za vita!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Dominika ya II ya Pasaka, ambayo ni ya huruma ya Mungu, tarehe 12 Aprili 2026, Baba Mtakatifu Leo XIV akiwageukia waamini na mahujai waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, alieleza kuwa, "Leo Makanisa mengi ya Mashariki yanasherehekea Pasaka kulingana na kalenda ya Julian. Kwa jumuiya hizo zote, ninatoa matashi yangu ya dhati ya amani, katika ushirika wa imani katika Bwana Mfufuka. Ninawasindikiza kwa maombi mazito zaidi kwa wale wanaoteseka kwa sababu ya vita, hasa watu wapendwa wa Ukraine. Mwanga wa Kristo ulete faraja kwa mioyo iliyoteseka na kuimarisha tumaini la amani. Jumuiya ya kimataifa isipoteze kamwe mtazamo wa mkasa wa vita hivi! Pia niko karibu zaidi na watu wapendwa wa Lebanon katika siku hizi za maumivu, hofu, na tumaini lisiloshindika kwa Mungu.
Wito wa kusitisha mapigano na kutafuta suluhisho
Papa Leo aliendelea, “Kanuni ya ubinadamu, iliyoandikwa katika dhamiri ya kila mtu na kutambuliwa katika sheria za kimataifa, inahusisha wajibu wa kimaadili wa kuwalinda raia kutokana na athari mbaya za vita. “Ninatoa wito kwa pande zinazopigana kusitisha mapigano na kutafuta suluhisho la amani haraka.”
Vita nchini Sudan vyaingia mwaka wa tatu
Jumatano ijayo inaadhimisha miaka mitatu tangu kuanza kwa mgogoro wa umwagaji damu nchini Sudan. Jinsi gani watu wa Sudan wanavyoteseka, waathiriwa wasio na hatia wa mkasa huu usio wa kibinadamu! Ninarudia wito wangu wa dhati kwa pande zinazopigana kunyamazisha silaha zao na kuanza, bila masharti, mazungumzo ya dhati yanayolenga kukomesha vita hivi vya mauaji ya kidugu haraka iwezekanavyo.
Salamu mbali mbali kwa mahujaji
Papa aliwakaribisha warumi na wote mahujaji, hasa waamini waliosherehekea Dominika ya Huruma ya Mungu katika Madhabahu ya Roho Mtakatifu huko Sassia. Salamu pia kwa Musikverein Kleinraming, wa Jimbo la Linz nchini Austria, na Waamini walifika kutoka Poland, na kama ilivu vijana na Chuo cha Mtakatifu Jean de Passy wa Paris na wale wa mataifa mbali mbali ya Harakati ya Wafocolari. Salamu za Papa pia ziliwaendea wanahija wa Jumuyia ya Mtakatifu Benedikto Po na Wanakipaimara wa Mtakatifu Malaika Mkuu wa Romagna na Mtakatifu Vito.
Ziara ya Kitume
Papa alikumbusha jinsi ambavyo atasafiri: “ Kesho nitaondoka kwa Ziara ya kitume ya siku kumi kwenda nchi nne za Afrika: Algeria, Cameroon, Angola, na Guinea ya Ikweta. Ninawaomba tafadhali mnisindikize na maombi yenu. Asante! Dominika Njema.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
